bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 20
Jeremiah 20
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 21 →
1
Mtambikaji Pashuri, mwana wa Imeri, aliyekuwa msimamizi mkuu wa Nyumba ya Bwana, akamsikia Yeremia, alipoyafumbua maneno yale.
2
Ndipo, Pashuri alipompiga mfumbuaji Yeremia, akamfunga kwa mikatale iliyokuwa kwenye lango la juu la Benyamini katika Nyumba ya Bwana.
3
Kulipokucha Pashuri akamfungua Yeremia tena katika mikatale; ndipo, Yeremia alipomwambia: Bwana hatakuita tena jina lako Pashuri, ila Magori-Misabibu (Kitisho po pote).
4
Kwani hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Utaniona, nikikutoa kuwa kitisho kwako wewe nako kwao wote wakupendao, maana wataangushwa kwa panga za adui zao, nayo macho yako yataviona! Nao Wayuda wote nitawatia mkononi mwa mfalme wa Babeli, atawahamisha kwenda Babeli akiwapiga kwa upanga.
5
Nazo mali zote za mji huu nitazitoa, na mapato yao yote na vitu vyao vyote vyenye kiasi kikubwa na vilimbiko vyote vya mfalme wa Yuda, nitavitia mikononi mwa adui zao, wavipokonye, wavichukue na kuvipeleka Babeli.
6
Wewe Pashuri nawe nao wote wakaao nyumbani mwako mtakwenda kwa kutekwa, utafika Babeli, utakufa huko, utazikwa huko wewe na wapenzi wako wote, uliowafumbulia maneno ya uwongo.
7
Bwana umenishinda, nami nimeshindika; umenishika kwa nguvu, ukaniweza. Ninachekwa mchana kutwa, wote wananifyoza.
8
Kwani ninaposema ninalia; sina budi kutangaza ukorofi na upotovu, kwani Neno la Bwana hunipatia kutukanwa na kufyozwa mchana kutwa.
9
Kwa hiyo nilisema: Sitamkumbuka, wala sitasema tena katika Jina lake, basi, ikawa moyoni mwangu kama moto uwakao kwa kufungiwa katika mifupa yangu, nikashindwa kuuvumilia, sikuweza kabisa.
10
Kwani nimesikia wengi, wakinong'onezana kwamba: Anatishwa po pote, mchongeeni! Nasi na tumchongee! Hiyo ni njama yao wote walio rafiki zangu, hunivizia, nianguke, kwamba: Labda atashindwa, tumweze nasi, tupate kujilipiza kwake.
11
Lakini Bwana yuko pamoja nami kama mpiga vita mwenye nguvu; kwa hiyo wanikimbizao watajikwaa, wasiniweze, watapatwa na soni kabisa, kwani hawaerevuki, soni zao zitakuwa za kale na kale, hazitasahauliwa.
12
Wewe Bwana unajaribu mwongofu, unayaona mafigo na moyo; na nione, jinsi unavyowalipiza kisasi, kwani nimekusukumia wewe shauri langu.
13
Mwimbieni Bwana! Mshangilieni Bwana! Kwani huiponya roho ya mkiwa mikononi mwao wafanyao mabaya.
14
Siku niliyozaliwa iwe imeapizwa! Siku, mama yangu aliyonizaa, isibarikiwe!
15
Awe ameapizwa naye mtu aliyempasha baba yangu habari kwamba: Umezaliwa mtoto wa kiume! akamfurahisha.
16
Mtu huyo na awe kama ile miji, Bwana aliyoiangamiza pasipo kugeuza moyo! Asubuhi na asikie vilio, tena makelele, jua linapofika kichwani,
17
kwa kuwa hakunifisha tumboni mwa mama; hivyo mama angalikuwa kaburi langu, hiyo mimba yake ingalikuwa ya siku zote.
18
Mbona nilitoka tumboni kuona masumbufu na machungu, siku zangu zikamalizika, nikipatwa na soni tu?
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 21 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52