bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 22
Jeremiah 22
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 23 →
1
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Shuka kwenda nyumbani mwa mfalme wa Yuda, uliseme mle neno hili,
2
kwamba: Sikia, mfalme wa Yuda, ukikaliaye kiti cha kifalme cha Dawidi, wewe na watumishi wako nao walio wa ukoo wako mnaoingia humu malangoni!
3
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Fanyeni yaliyo sawa yaongokayo! Waponyeni walionyang'anywa na kuwatoa mikononi mwa wakorofi! Wageni nao waliofiwa na wazazi na wajane msiwaonee, wala msiwakorofishe! Wala damu zao wasiokosa msizimwage mahali hapa!
4
Kwani kama mtalifanya kweli neno hili, wataingia malangoni mwa nyumba hii wafalme wanaokikalia kiti cha kifalme cha Dawidi, wanaopanda magari na farasi, wao wenyewe na watumishi wao na watu wao.
5
Lakini msipoyasikia maneno haya, basi, nimejiapia mwenyewe, nyumba hii itakuwa mavunjiko; ndivyo, asemavyo Bwana.
6
Kwani hivi ndivyo, Bwana anavyoisemea nyumba ya mfalme wa Yuda: Kwangu wewe u kama Gileadi ulio mlima mkubwa wa Libanoni; kweli nitakugeuza kuwa nyika yenye miji isiyokaa watu.
7
Nitajichagulia waangamizaji wako, kila mtu na mata yake, waikate miangati yako iliyochaguliwa, waitupe motoni!
8
Wamizimu wengi watakapopapitia penye mji huu wataulizana mtu na mwenziwe: Kwa sababu gani Bwana ameufanyizia mji huu mkubwa mambo kama hayo?
9
Nao watu watawajibu: Ni kwa sababu wameliacha Agano la Bwana Mungu wao, wakaangukia miungu mingine na kuitumikia.
10
Msimlilie mfu, wala msimwombolezee! Ila mmlilie sana yeye aliyekwenda! Kwani hatarudi tena, wala hataiona tena nchi, alikozaliwa.
11
Kwani hivi ndivyo, Bwana anavyosema kwa ajili ya Salumu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, aliyempokea baba yake ufalme, akatoka mahali hapa: Hatarudi huku tena!
12
Kwani mahali, walipomhamishia, ndipo, atakapofia, asiione tena nchi hii.
13
Yatampata aijengaye nyumba yake kwa njia isiyoongoka, navyo vyumba vyake vilivyomo kwa njia isiyo sawa; huzitumia kazi za mwenziwe bure tu asipompa mshahara wake.
14
Anasema: Nitajijengea nyumba kubwa yenye vyumba vipana, nitavitobolea madirisha, nitavipigilia juu mbao za miangati, kisha nitavipaka rangi nyekundu.
15
Je? Ufalme wako ni kushindana na miangati? Je? Baba yako hakula, hakunywa? Lakini amefanya yaliyo sawa yaongokayo; ndipo, alipopata kukaa vema.
16
Akatengenezea wanyonge na wakiwa mashauri yao; ndipo, alipopata kukaa vema; huko siko kunijua? ndivyo, asemavyo Bwana.
17
Kwani hakuna mengine, macho yako na moyo wako yanayoyatazamia, ni njia tu za kupata, nazo za kumwaga damu zao wasiokosa, nazo za kukorofisha, nazo za kupenyezewa, uyafanye mambo hayo.
18
Kweli hivi ndivyo, Bwana anavyosema kwa ajili ya Yoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda: Hawatamwombolezea kwamba: A ndugu yetu! A umbu letu! Wala hawatamwombolezea kwamba: A bwana! A mwenye utukufu!
19
Atazikwa, kama punda anavyozikwa, akikokotwa na kutupwa nje kwenye malango ya Yerusalemu.
20
Panda Libanoni, ulie! Nako Basani zipaze sauti zako! Nako toka Abarimu vilio vyako visikilike! Kwani wote waliokupenda wamepondwa.
21
Nilikuambia neno, ulipokuwa umetulia vema, ukajibu: Sisikii! Hii ndiyo njia yako tangu ujana wako, kwani hukuisikia sauti yangu.
22
Upepo utawachunga wachungaji wako wote, nao waliokupenda watakwenda kufungwa; ndipo, utakapoona soni na kuiva uso kwa ajili ya ubaya wako wote.
23
Unakaa kama ndege ya Libanoni katika tundu kwenye miangati; lakini utapaswa na kuhurumiwa, machungu yatakapokujia yatakayokuwa kama uchungu wa mzazi.
24
Ndivyo, asemavyo Bwana: Hivyo, nilivyo Mwenye uzima, kama wewe Konia, mwana wa Yoyakimu, mfalme wa Yuda, ungekuwa pete yenye muhuri mkononi pangu pa kuume, ningekuondoa kwa nguvu,
25
nikakutia mikononi mwao waitafutao roho yako namo mikononi mwao, unaowaogopa sana, namo mikononi mwa Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, namo mikononi mwa Wakasidi.
26
Tena wewe na mama yako aliyekuzaa nitawabwaga katika nchi nyingine isiyo yenu ya kuzaliwa; ndiko, mtakakofia.
27
Lakini katika nchi hii, wanayoitunukia rohoni mwao, hawatarudi huku.
28
Je? Huyu mtu Konia siye chungu kinachowaziwa si kitu, kinachovunjwa tu? Siye chombo kisichopendwa? Mbona yeye nao walio kizazi chake wamebwagwa na kutupwa katika nchi, wasiyoijua?
29
E nchi, nchi, nchi, lisikie Neno lake Bwana!
30
Ndivyo, Bwana anavyosema: Mwandikeni mtu huyu kuwa pasipo watoto, kuwa mtu asiyejipatia mema siku zake zote, hata katika kizazi chake hamna mtu atakayejipatia kukikalia kiti cha kifalme cha Dawidi na kuwatawala Wayuda tena.
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 23 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52