bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 23
Jeremiah 23
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 24 →
1
Yatawapata wachungaji wanaowaangamiza na kuwatawanya kondoo, niliowapa kuwachunga! ndivyo, asemavyo Bwana.
2
Hivi ndivyo kweli, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyosema kwa ajili ya wachungaji. Ninyi mnaowachunga walio ukoo wangu, mmewatawanya kondoo wangu na kuwakimbiza, hamkuwaangalia; mtaniona, nikiwapatilizia ubaya wa matendo yenu; ndivyo, asemavyo Bwana.
3
Nami nitawakusanya masao ya kondoo wangu na kuwatoa katika nchi zote, nilikowaendesha na kuwakimbiza, Nitawarudisha katika makao yao, wazae, wawe wengi tena.
4
Kisha nitawawekea wachungaji, wawachunge; hawataogopa tena, wala hawatastuka, wala hawatapotea hata mmoja wao; ndivyo, asemavyo Bwana.
5
Ndivyo, asemavyo Bwana: Mtaona, siku zitakapokuja, nikimwinulia Dawidi chipuko lenye wongofu, naye atakuwa mfalme ajuaye vema kutawala, maana atafanya katika nchi yaliyo sawa yaongokayo.
6
Yuda ataokolewa katika siku zake, naye Isiraeli atakaa salama. Jina lake, watakalomwita, ni hili: Bwana ni wongofu wetu!
7
Ndivyo, asemavyo Bwana: Mtaona kweli, siku zikija, watakapoacha kuapa wakisema: Hivyo, Bwana alivyo Mwenye uzima aliyewatoa wana wa Isiraeli katika nchi ya Misri,
8
ila wataapa wakisema: Hivyo, Bwana alivyo Mwenye uzima aliyewaleta wazao wa mlango wa Isiraeli akiwatoa katika nchi ya upande wa kaskazini na katika nchi zote, nilikowaendesha na kuwakimbiza; ndipo, watakapokaa huku katika nchi yao.
9
Kwa wafumbuaji. Moyo wangu umevunjika kifuani mwangu, mifupa yangu yote ikatetemeka; nikawa kama mlevi au kama mtu ashindwaye na mvinyo, nilipoyasikia yaliyotoka kwake Bwana, hayo maneno yake matakatifu kwamba:
10
Nchi hii imezaa wazinzi, kwa hiyo nchi hii inakaa matanga kwa kuapizwa, mbuga za nyikani zimekauka, kwa kuwa ni mabaya, wanayoyakimbilia, nayo nguvu yao siyo ifaayo.
11
Kwani nao wafumbuaji pamoja na watambikaji ni wapotovu, namo Nyumbani mwangu nimeuona ubaya wao; ndivyo, asemavyo Bwana.
12
Kwa sababu hii njia yao itakuwa inateleza, penye giza watateleza na kuanguka hapohapo, kwani nitawaletea mabaya, ndio mwaka wa kupatilizwa kwao; ndivyo, asemavyo Bwana.
13
Hata kwa wafumbuaji wa Samaria nimeona upumbavu, wakifumbua kwa nguvu ya Baali, wakawapoteza nao walio ukoo wangu wa Isiraeli.
14
Lakini kwa wafumbuaji wa Yerusalemu nimeona mastusho: huzini, huendelea na kudanganya, huitia mikono ya wabaya nguvu, wasiuache kila mtu ubaya wake, wote pia wameniwia kama Wasodomu, nao wakaao humo kama Wagomora.
15
Kwa hiyo Bwana Mwenye vikosi anasema hivyo kwa ajili ya wafumbuaji: Mtaniona, nikiwalisha majani machungu na kuwanywesha maji yenye sumu! Kwani kwa wafumbuaji wa Yerusalemu kumetoka upotovu, ukaziingia nchi zote.
16
*Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Msiyasikie maneno ya wafumbuaji wanaowafumbulia maneno wakiwaegemeza mambo yaliyo ya bure tu! Huyasema, waliyoyaona mioyoni mwao, hawasemi yaliyotoka kinywani mwa Bwana.
17
Huwaambia wanibezao: Bwana amesema: Mtakaa na kutengemana! Kila mtu aufuataye ushupavu wa moyo wake humwambia: Hakuna kibaya kitakachowafikia!
18
Kwani yuko nani aliyesimama penye njama ya Bwana, akimwona au akilisikia neno lake? Yuko nani aliyeliangalia Neno lake, akilisikia?
19
Mtakiona kimbunga cha Bwana, hata makali yenye moto, yakitoka kwake, nao upepo wa chamchela wenye nguvu utawaangukia vichwani wao wasiomcha Mungu.
20
Ukali wake Bwana hautatulia, mpaka ukiyafanya na kuyatimiza mawazo ya moyo wake; siku za mwisho mtayatambua haya.
21
Sikuwatuma wafumbuaji hawa, nao hupiga mbio; sikuwaambia neno, nao hufumbua.
22
Kama wangalikuwa wamesimama penye njama yangu, wangeyasema maneno yangu masikioni pao walio ukoo wangu, wangewarudisha wabaya katika njia zao, wauache ubaya wa matendo yao.
23
Ndivyo asemavyo Bwana: Je? Mimi ni Mungu akaaye karibu tu? Si Mungu akaaye hata mbali?
24
Ndivyo, asemavyo Bwana: Kama mtu anajificha mafichoni, mimi sitamwona? Si mimi azijazaye mbingu na nchi? ndivyo, asemavyo Bwana.
25
Nimeyasikia, wafumbuaji waliyoyasema, wakifumbua maneno ya uwongo katika Jina langu wakisema: Nimeota! Nimeota!
26
Hivyo vitakuwa mpaka lini mioyoni mwao wafumbuaji wafumbuao uwongo tu, walio wafumbuaji wa udanganyifu wa mioyo yao?
27
Huwaza, ya kuwa watawasahaulisha walio ukoo wangu Jina langu kwa ajili ya ndoto zao, wakizisimuliana kila mtu na mwenziwe, kama baba zao walivyolisahau Jina langu kwa ajili ya Baali.
28
Mfumbuaji aliyeota na asimulie ndoto! Naye aliyelisikia Neno langu na aliseme Neno langu, lilivyo kweli! Kumvi na mpunga ziko na fungu gani lililo lao pamoja? ndivyo, asemavyo Bwana.
29
Ndivyo, asemavyo Bwana: Neno langu si kama moto au kama nyundo ipasuayo miamba?*
30
Ndivyo, asemavyo Bwana: Mtaniona kweli, nikiwajia wafumbuaji, kwa kuwa wanaliiba Neno langu kila mtu kwa mwenziwe!
31
Ndivyo, asemavyo Bwana: Mtaniona, nikiwajia wafumbuaji, kwa kuwa huzitumia ndimi zao za kusema: Asema!
32
Ndivyo, asemavyo Bwana: Mtaniona, nikiwajia wafumbuaji wa ndoto za uwongo. Huzisimulia walio ukoo wangu, wakawapoteza kwa uwongo wao na kwa mambo yao makuu, nami sikuwatuma, wala sikuwaagiza neno, nao walio wa ukoo huu hawawafalii kitu hata kidogo; ndivyo, asemavyo Bwana.
33
Kama watakuuliza walio wa ukoo huu au mfumbuaji au mtambikaji kwamba: Tamko zito la Bwana ni nini? ndipo, utakapowajibu: Hili ndilo tamko zito la Bwana, akisema: Nitawabwaga ninyi! ndivyo, asemavyo Bwana.
34
Lakini mfumbuaji na mtambikaji nao walio wa ukoo huu watakaolitumia neno hilo la kwamba: Tamko zito la Bwana, mtu huyo nitampatiliza pamoja na mlango wake.
35
Hivyo ndivyo, mtakavyoulizana mtu na mwenziwe, hata mtu na ndugu yake kwamba: Bwana amejia nini? au: Bwana amesema nini?
36
Tamko zito la Bwana wasilitaje tena! Kama wanalitaja, basi, kila mtu neno lake litamgeukia kuwa tamko zito, kwani ninyi huyageuza maneno ya Mungu aliye Mwenye uzima, aliye Bwana Mwenye vikosi, Mungu wetu.
37
Hivi ndivyo, utakavyomwuliza mfumbuaji kwamba: Bwana amejibu nini? au: Bwana amesema nini?
38
Lakini mkisema: Tamko zito la Bwana, basi, itakuwa hivyo, Bwana alivyosema: Kwa kuwa mnalisema neno hilo la kwamba: Tamko zito la Bwana, nami nilituma kwenu kuwakataza, msiseme: Tamko zito la Bwana!
39
basi, mtaniona, nikiwaacha kabisa na kuwabwaga ninyi pamoja na mji huu, niliowapa ninyi na baba zenu, mtoke usoni pangu.
40
Hivyo nitawatia soni za kale na kale na matusi ya kale na kale yasiyosahaulika.
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 24 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52