bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 27
Jeremiah 27
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 26
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 28 →
1
Katika mwanzo wa ufalme wa Yoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, neno hili likamjia Yeremia likitoka kwake Bwana kwamba:
2
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Jitengenezee kamba na kongwa, uzitie shingoni pako!
3
Kisha uzitume kwa mfalme wa Edomu na kwa mfalme wa Moabu na kwa Mfalme wa wana wa Amoni na kwa mfalme wa Tiro na kwa mfalme wa Sidoni, ukizitia mikononi mwa wajumbe wanaokuja Yerusalemu kwa Sedekia, mfalme wa Yuda!
4
Uwaagize, wawaambie mabwana wao kwamba: Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema, navyo ndivyo, mtakavyowaambia mabwana wenu:
5
Mimi nilizifanya nchi na watu na nyama wa porini walioko katika nchi kwa nguvu yangu iliyo kuu na kwa mkono wangu uliokunjuka, nikampa anyokaye machoni pangu.
6
Sasa mimi nimezitia nchi hizi zote mkononi mwa Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, aliye mtumishi wangu; hata nyama wa porini nimempa, wamtumikie.
7
Mataifa yote yatamtumikia yeye na mwanawe na mjukuu wake, mpaka zitakapotimia siku za nchi yake; ndipo, mataifa yenye watu wengi na wafalme wakuu watakapomtumikisha naye.
8
Itakuwa, taifa au ufalme utakaokataa kumtumikia Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, na kuzitia shingo zao katika makongwa ya mfalme wa Babeli, watu wa taifa hilo nitawapatiliza kwa panga na kwa njaa na kwa magonjwa mabaya.
9
Kwa hiyo ninyi msiwasikie wafumbuaji wenu wala waaguaji wenu wala ndoto zenu wala waganga wenu wala watazamaji wenu wanaowaambia kwamba: Hamtamtumikia mfalme wa Babeli!
10
Kwani huwafumbulia yenye uwongo, kusudi wawatoe katika nchi yenu na kuwapeleka katika nchi ya mbali, nami niwatupe ninyi, mwangamie.
11
Lakini watu wa taifa litakalotia shingo zao katika makongwa ya mfalme wa Babeli, wamtumikie, nitawatuliza katika nchi yao, wailime wakikaa kwao; ndivyo, asemavyo Bwana.
12
Kisha nikamwambia Sedekia, mfalme wa Yuda, maneno haya yote ya kwamba: Zitieni shingo zenu katika makongwa ya mfalme wa Babeli, mmtumikie yeye na watu wake wote, mpate kukaa!
13
Kwa sababu gani mnataka kufa, wewe nao walio ukoo wako, kwa panga na kwa njaa na kwa magonjwa mabaya, kama Bwana alivyosema kwa ajili ya taifa litakalokataa kumtumikia mfalme wa Babeli?
14
Msiyasikie maneno ya wafumbuaji wanaowaambia kwamba: Msimtumikie mfalme wa Babeli! Kwani hao huwafumbulia yenye uwongo.
15
Ndivyo, asemavyo Bwana: Sikuwatuma, nao hufumbua katika Jina langu yenye uwongo, kusudi niwatupe ninyi, mwangamie ninyi na wafumbuaji waliowafumbulia ninyi.
16
Nao watambikaji na watu wote wa ukoo huu nikawaambia kwamba: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Msiyasikie maneno ya wafumbuaji wenu wanaowafumbulia kwamba: Mtaona, vyombo vya Nyumba ya Bwana vikirudishwa toka Babeli sasa bado kidogo tu! Kwani hao huwafumbulia yenye uwongo.
17
Msiwasikie! Ila mtumikieni mfalme wa Babeli, mpate kukaa! Kwa nini mji huu ugeuke kuwa mavunjiko?
18
Kama ndio wafumbuaji, kama Neno la Bwana liko kwao, na wamwombe Bwana Mwenye vikosi, vyombo vilivyosalia katika Nyumba ya Bwana namo nyumbani mwa mfalme wa Yuda namo Yerusalemu visiende Babeli!
19
Kwani hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema kwa ajili yao: Zile nguzo na bahari na vilingo na vyombo vyote vilivyosalia humu mjini,
20
kweli Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, hakuvichukua alipomhamisha Yekonia, mwana wa Yoyakimu, mfalme wa Yuda, toka Yerusalemu kwenda Babeli pamoja na wakuu wote wa Yuda na wa Yerusalemu;
21
lakini hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema kwa ajili ya vyombo vilivyosalia Nyumbani mwa Bwana namo nyumbani mwa mfalme wa Yuda namo Yerusalemu:
22
Vitapelekwa Babeli; ndiko, vitakakokuwa mpaka siku ile, nitakapowapatiliza; ndivyo, asemavyo Bwana. Ndipo, mtakapovileta huku na kuvirudisha mahali hapa.
← Chapter 26
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 28 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52