bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 28
Jeremiah 28
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 27
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 29 →
1
Ikawa mwaka uleule, ufalme wa Sedekia, mfalme wa Yuda, ulipoanzia, katika mwezi wa tano wa mwaka wa nne, ndipo, mfumbuaji Hanania, mwana wa Azuri wa Gibeoni, aliponiambia Nyumbani mwa Bwana machoni pao watambikaji napo pao wote wa ukoo huu kwamba:
2
Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema kwamba: Nimeyavunja makongwa ya mfalme wa Babeli.
3
Bado miaka miwili ndipo, mimi nitakapovirudisha mahali hapa vyombo vyote vya Nyumba ya Bwana, Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, alivyovichukua mahali hapa na kuvipeleka Babeli.
4
Naye Yekonia, mwana wa Yoyakimu, mfalme wa Yuda, nayo mateka yote ya Yuda waliokwenda Babeli mimi nitawarudisha mahali hapa, kwani nitayavunja makongwa ya mfalme wa Babeli; ndivyo, asemavyo Bwana.
5
Mfumbuaji Yeremia akamwambia mfumbuaji Hanania machoni pao watambikaji napo pao watu wote wa ukoo huu waliosimama katika Nyumba ya Bwana,
6
akasema mfumbuaji Yeremia: Amin, na yawe hivyo! Bwana na ayafanye hivyo akiyatimiza maneno yako, uliyoyafumbua, akivirudisha mahali hapa vyombo vya Nyumba ya Bwana nayo mateka yote toka Babeli!
7
Lisikie tu neno hili, ninalolisema masikioni mwako, namo masikioni mwa watu wote wa ukoo huu:
8
Wafumbuaji waliokuwa mbele yangu na mbele yako toka siku za kale walifumbulia nchi nyingi, hata nchi zenye wafalme wakuu vita na mabaya na magonjwa yauayo yatakayokuja.
9
Lakini mfumbuaji anayefumbua mambo ya kutuliza roho atajulikana hapo, lile neno lake mfumbuaji litakapotimia, ya kuwa ni mfumbuaji, Bwana aliyemtuma kweli.
10
Ndipo, mfumbuaji Hanania alipoiondoa miti ya kongwa shingoni pake Yeremia, akaivunja.
11
Kisha Hanania akasema, watu wote wa ukoo huu wakimtazama, kwamba: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Hivi ndivyo, nitakavyoyavunja makongwa ya Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, shingoni pa mataifa yote, miaka miwili itakapopita. Kisha mfumbuaji Yeremia akashika njia kwenda zake.
12
Neno la Bwana likamjia Yeremia, mfumbuaji Hanania alipokwisha kuivunja miti ya kongwa shingoni pake mfumbuaji Yeremia, likamwambia:
13
Nenda kumwambia Hanania haya: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Miti ya kongwa, uliyoivunja, ni ya miti tu; lakini mahali pao umeweka miti ya kongwa iliyo ya chuma.
14
Kwani hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema: Makongwa ya chuma nimetia shingoni pao haya mataifa yote, wamtumikie Nebukadinesari, mfalme wa Babeli; watamtumikia kweli, nao nyama wa porini nimempa.
15
Basi, mfumbuaji Yeremia akamwambia mfumbuaji Hanania: Sikia, Hanania! Bwana hakukutuma, nawe umewaegemeza watu wa ukoo huu mambo ya uwongo.
16
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema kweli: Utaniona, nikikutuma kuondoka huku nchini, mwaka huu wewe utakufa, kwani umewakataza watu kumtii Bwana.
17
Mfumbuaji Hanania akafa mwaka uleule katika mwezi wa saba.
← Chapter 27
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 29 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52