bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 29
Jeremiah 29
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 28
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 30 →
1
Haya ndiyo maneno ya barua ya mfumbuaji Yeremia, aliyoiandika Yerusalemu kwenda kwao wazee waliosalia kwao waliotekwa na kwa watambikaji na kwa wafumbuaji na kwa watu wote wa ukoo huu, Nebukadinesari aliowateka Yerusalemu na kuwapeleka Babeli.
2
Mfalme Yekonia na mama yake walipokwisha kutoka Yerusalemu pamoja na wakuu wa nyumba ya mfalme na wakuu wa Yuda na wa Yerusalemu na mafundi wa seremala na wahunzi,
3
ndipo, alipoitia mikononi mwao Elasa, mwana wa Safani, na Gemaria, mwana wa Hilkia; hawa ndio, Sedekia, mfalme wa Yuda, aliowatuma kwenda Babeli kwa Nebukadinesari, mfalme wa Babeli. Akawaandikia:
4
Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyowaambia mateka yote, niliowatoa Yerusalemu, wapelekwe Babeli:
5
Jengeni nyumba, mkae! Limeni mashamba, mle mazao yao!
6
Oeni wanawake, mzae watoto wa kiume na wa kike! Nao wana wenu wa kiume wapatieni wanawake, nao wana wenu wa kike mwaoze waume, wazae watoto wa kiume na wa kike, mwe wengi huko, msipunguke!
7
Utafuteni utengemano wa ule mji, niliowahamishia ninyi! Uombeeni kwa Bwana! Kwani unapotengemana, nanyi mtapata kutengemana.
8
Kwani hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema: Wasiwadanganye wafumbuaji walioko kwenu katikati wala waaguaji wenu! Wala msizisikie ndoto zenu, mnazoziota!
9
Kwani hao huwafumbulia maneno yenye uwongo katika Jina langu, sikuwatuma; ndivyo, asemavyo Bwana.
10
Kwani hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Kwanza sharti miaka 70 ipite huko Babeli; ndipo, nitakapowatokea, niwatimizie lile neno langu jema la kwamba: Nitawarudisha mahali hapa.
11
Kwani ndivyo, asemavyo Bwana: Mimi ninayajua mawazo, ninayowawazia, kuwa mawazo ya kuwaponya, siyo ya kuwaponza, nipate kuwapa huko nyuma myangojeayo.
12
Mtakaponiita mkiendelea kunilalamikia, nitawasikia.
13
Mtakaponitafuta, mtaniona; mtakaponitafuta kwa mioyo yote,
14
nitawaonekea, nitawafungua mafungo yenu, niwakusanye na kuwatoa kwenye mataifa yote na mahali po pote, nilipowahamishia; ndivyo, asemavyo Bwana.
15
Kwani ninyi husema: Bwana ametuinulia wafumbuaji huku Babeli.
16
Kwani hivi ndivyo, Bwana anavyosema kwa ajili ya mfalme anayekaa katika kiti cha kifalme cha Dawidi na kwa ajili ya watu wote wa ukoo huu wanaokaa humu mjini walio ndugu zenu, wasiotoka pamoja nanyi kwenda kuhamishwa;
17
hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Wataniona, nikituma kwao panga na njaa na magonjwa mabaya, nikiwageuza kuwa kuyu zitapishazo, zisizolika kwa ubaya wao.
18
Nitawakimbiza kwa panga na kwa njaa na kwa magonjwa mabaya, nitawatoa, watupwe huko na huko katika nchi zote zenye wafalme huku ulimwenguni, waapizwe kwa kustukiwa, wazomelewe na kutukanwa kwenye mataifa yote, nitakakowatupa,
19
kwa kuwa hawakuyasikia maneno yangu; ndivyo, asemavyo Bwana. Mimi nilituma kwao watumishi wangu walio wafumbuaji pasipo kuchoka kila kulipokucha, lakini hamkusikia; ndivyo, asemavyo Bwana.
20
Lakini ninyi lisikieni Neno la Bwana, ninyi mateka yote, niliowatoa Yerusalemu na kuwatuma kwenda Babeli!
21
Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema kwa ajili ya Ahabu, mwana wa Kolaya, na kwa ajili ya Sedekia, mwana wa Masea, waliowafumbulia katika Jina langu mambo ya uwongo: Mtaniona, nikiwatia mkononi mwa Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, awaue machoni penu.
22
Nako kwao ndiko, mateka yote ya Wayuda walioko Babeli watakakochukua kiapo cha kwamba: Bwana na akufanyizie kama Ahabu na kama Sedekia, mfalme wa Babeli aliowachoma motoni!
23
Kwa kuwa wamefanya yasiyofanywa kwao Waisiraeli, wakifanya ugoni na wanawake wa wenzao, wakasema neno la uwongo katika Jina langu, nami sikuwaagiza neno, Mimi ninayajua haya, ninayashuhudia.
24
Kwa ajili ya Semaya wa Nehelamu utasema kwamba:
25
Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema kwamba: Umetuma barua katika jina lako kwa watu wote wa ukoo huu waliomo Yerusalemu na kwa mtambikaji Sefania, mwana wa Masea, na kwa Yerusalemu na kwa watambikaji wote, za kwamba:
26
Bwana amekuweka kuwa mtambikaji mahali pa mtambikaji Yoyada, mwe wasimamizi Nyumbani mwa Bwana kuwaangalia wote wenye wazimu nao wajiwaziao kuwa wafumbuaji, uwafunge mikatale na mapingu.
27
Mbona sasa hukumkaripia Yeremia wa Anatoti anayewafumbulia ninyi?
28
Kwa sababu hii ametuma kwetu Babeli barua ya kwamba: Siku ni nyingi bado, jengeni nyumba, mkae! Limeni mashamba, mle mazao yao!
29
Mtambikaji Sefania alipoisoma barua hii masikioni pa mfumbuaji Yeremia,
30
ndipo, neno la Bwana lilipomjia Yeremia kwamba:
31
Tuma barua kwa mateka yote kwamba: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema kwa ajili ya Semaya wa Nehelamu: Kwa kuwa Semaya amewafumbulia ninyi, nami sikumtuma, akawaegemeza mambo ya uwongo,
32
kwa hiyo Bwana anasema haya: Mtaniona, nikimpatiliza Semaya wa Nehelamu na kizazi chake: hatapata mtu wa mlango wake atakayekaa kwao wa ukoo huu, wala atakayeyaona yale mema, nitakayowafanyizia wao walio ukoo wangu, kwani amewakataza watu kumtii Bwana; ndivyo, asemavyo Bwana.
← Chapter 28
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 30 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52