bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 33
Jeremiah 33
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 32
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 34 →
1
Neno la Bwana likamjia Yeremia mara ya pili, alipokuwa amefungwa bado uani penye kifungo, la kwamba:
2
Hivi ndivyo, anavyosema Bwana aliye mwenye kuvifanya, anavyovitengeneza, avitimize, Bwana ni Jina lake.
3
Niite! ndipo, nitakapokujibu, nikuambie mambo makuu yaliyo magumu, usiyoyajua.
4
Kwani hivi ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyosema kwa ajili ya nyumba za mji huu na kwa ajili ya nyumba za wafalme wa Yuda zilizobomolewa, zitumike kujenga maboma ya kuzuilia panga;
5
akasema hata kwa ajili yao waliokuja kupigana na Wakasidi, lakini wakawapatia tu watu wengi wa kuwaua, ndio wao, niliowapiga kwa makali yangu yaliyowaka moto, ndio wao, niliowaficha uso wangu, watu wa mji huu wasiuone kwa ajili ya mabaya yao.
6
Mtaniona, nikiwapatia uzima na uponya; nitawaponya, kisha nitawafunulia mfuriko wa utengemano ulio wa kweli.
7
Nitayafungua mafungo ya Wayuda na mafungo ya Waisiraeli, nitawajenga, wawe, kama walivyokuwa mwanzo.
8
Nitawaeua, maovu yote, waliyonikosea, yawatoke, nikiwaondolea hayo maovu yao yote, waliyonikosea na kunitengua.
9
Ndipo, jina lake huo mji litakapokuwa la kunifurahisha kwa kunisifu na kunitukuza kwenye mataifa yote ya huku nchini, kwani watayasikia mema yote, mimi niliyowafanyizia, nao watastuka na kutetemeka kwa ajili ya hayo mema yote na kwa ajili ya huo utengemano wote, nitakaowapatia mimi.
10
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Ninyi mnapaita mahali hapa Penye mavunjiko, kwa kuwa hapana mtu wala nyama, lakini hapa napo penye miji ya Yuda na penye barabara za Yerusalemu zilizo peke yao, kwa kuwa hapana mtu wala apitaye wala akaaye wala hapana nyama,
11
ndipo, patakaposikilika tena sauti za vicheko na sauti za furaha, hata sauti za wachumba wa kiume na wa kike, tena sauti zao wasemao: Mshukuruni Bwana Mwenye vikosi, ya kuwa Bwana ni mwema! Ya kuwa upole wake ni wa kale na kale! Watavileta vipaji vyao vya kumshukuru katika Nyumba ya Bwana, kwani nitayafungua mafungo ya nchi hii, iwe, kama ilivyokuwa mwanzo.
12
Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Mahali hapa palipo Penye mavunjiko, kwa kuwa hapana mtu wala nyama, napo penye miji yake yote patakuwa tena na malisho ya wachungaji, wanapowapumzisha kondoo wao.
13
Katika miji iliyoko milimani, namo katika miji iliyoko mbugani, namo katika miji iliyoko upande wa kusini, hata katika nchi ya Benyamini na pande zote za Yerusalemu, namo katika miji ya Yuda makundi ya kondoo yatapita tena yakichungwa na mikono yao wanaowahesabu; ndivyo, Bwana anavyosema.
14
Ndivyo, asemavyo Bwana: Mtaona, siku zikija, nitakapolitimiza lile neno jema, nililowaambia walio wa mlango wa Isiraeli nao walio wa mlango wa Yuda!
15
Siku zile za wakati ule zitakapotimia, ndipo, nitakapomchipuzia Dawidi chipuko lenye wongofu, naye atafanya katika nchi hii yaliyo sawa yaongokayo.
16
Siku zile ndipo, nchi ya Yuda itakapookolewa, nao mji wa Yerusalemu utakaa salama, nalo jina, utakaloitwa ni hili: Bwana ni wongofu wetu.
17
Kwani hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Kwao wa Dawidi hatakoseka mtu atakayekaa katika kiti cha kifalme cha mlango wa Isiraeli.
18
Hata kwao watambikaji na Walawi hatakoseka mtu wa kutumikia usoni pangu, kama ni kuteketeza ng'ombe za tambiko au kuvukiza vipaji vya tambiko au kuyatengeneza matoleo ya tambiko ya kila siku.
19
Neno la Bwana likamjia Yeremia kwamba:
20
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Hamwezi kulivunja agano langu la mchana wala agano langu la usiku, pasiwe mchana wala usiku panapopasa.
21
Vilevile agano langu, nililoliagana na mtumishi wangu Dawidi, halitawezekana kuvunjwa asiwe na mwanawe atakayetawala na kukaa katika kiti chake cha kifalme, wala wasipatikane Walawi walio watambikaji wa kunitumikia.
22
Kama vikosi vya mbinguni visivyohesabika, tena kama mchanga wa baharini usivyopimika, ndivyo, nitakavyowafurikisha walio wa kizazi cha mtumishi wangu Dawidi kuwa wengi, hata Walawi wanaonitumikia.
23
Neno la Bwana likamjia Yeremia kwamba:
24
Hukusikia, watu hawa wa huku wanavyosema kwamba: Koo mbili, Bwana alizozichagua, amezitupa? Kwa hiyo huwabeza walio ukoo wangu, wasiwe taifa tena machoni pao.
25
Lakini hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Agano langu la mchana na la usiku liko, nayo maongozi ya mbinguni na ya nchini yako, hayaondoki.
26
Vilevile sitawatupa walio wa kizazi cha Yakobo na cha Dawidi, wala sitaacha kuchukua katika kizazi chake watakaowatawala walio wa kizazi cha Aburahamu na cha Isaka na cha Yakobo, kwani nitayafungua mafungo yao nitakapowahurumia.
← Chapter 32
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 34 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52