bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 34
Jeremiah 34
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 33
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 35 →
1
Hili ndilo neno lililomjia Yeremia likitoka kwa Bwana, Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, na vikosi vyake vyote na watu wa nchi zote za kifalme, mkono wake ulizozitawala, hayo makabila yote walipopiga vita, wauteke Yerusalemu na miji yake yote, likawa la kwamba:
2
Hivi ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyosema: Nenda kumwambia Sedekia, mfalme wa Yuda, ukimwambia: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Utaniona, nikiutia mji huu mkononi mwa mfalme wa Babeli, auteketeze kwa moto!
3
Nawe hutaopoka mkononi mwake, kwani utakamatwa, utiwe mkononi mwake, nawe utaonana na mfalme wa Babeli macho kwa macho, atasema na wewe kinywa kwa kinywa, nawe utakwenda Babeli.
4
Lisikie tu neno lake Bwana, wewe Sedekia, mfalme wa Yuda! Haya ndiyo, Bwana anayokuambia:
5
Utakufa na kutulia; kama baba zako waliokuwa wafalme wa kwanza, waliokuwa mbele yako, walivyowashiwa mioto, ndivyo, watakavyokuwashia nawe mioto wakikuombolezea kwamba: E Bwana! Kwani hili ndilo neno, nililolisema mimi; ndivyo, asemavyo Bwana.
6
Mfumbuaji Yeremia akamwambia Sedekia, mfalme wa Yuda, maneno haya yote mle Yerusalemu,
7
vikosi vya mfalme wa Babeli walipoupigia Yerusalemu vita, wauteke pamoja na miji yote ya Yuda iliyosalia, ndiyo Lakisi na Azeka; kwani hiyo ndiyo iliyosalia katika miji ya Yuda iliyokuwa yenye maboma.
8
Hili ndilo neno lililomjia Yeremia likitoka kwa Bwana hapo, mfalme Sedekia alipokwisha kuagana na watu wote waliokuwamo Yerusalemu kuwatangazia watumwa ukombozi,
9
kila mtu amwachilie mtumwa wake na kijakazi wake walio wa Kiebureo, akiwapa ruhusa, wajiendee tu, tena mtu asimtumikishe tena mwenziwe kazi za kutumwa katika nchi ya Yuda.
10
Wakayasikia wakuu wote nao watu wote walioingia katika agano hilo la kwamba: Kila mtu ampe mtumwa wake na kijakazi wake ruhusa, wajiendee tu, asiwatumikishe tena kazi za kitumwa; nao walipoyasikia, wakawapa ruhusa, wajiendee tu.
11
Lakini walipokwisha kufanya hivyo wakawarudia, wakawarudisha watumwa na vijakazi, waliowapa ruhusa, wajiendee tu, wakawashurutisha tena kuwa watumwa na vijakazi.
12
Kwa hiyo neno la Bwana likamjia Yeremia likitoka kwa Bwana kwamba:
13
Hivi ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyosema: Mimi nilifanya Agano na baba zenu siku ile, nilipowatoa katika nchi ya Misri nyumbani, mlimokuwa watumwa, kwamba:
14
Mwisho wa miaka saba, kila mtu akiwa na ndugu yake wa Kiebureo aliyenunuliwa nawe, sharti umpe ruhusa, atoke kwako, ajiendee tu. Akutumikie miaka sita, kisha sharti umpe ruhusa, atoke kwako, ajiendee tu! Lakini baba zenu hawakunisikia, wala hawakuyatega masikio yao.
15
Nanyi mmefanya leo tena yanyokayo machoni pangu, kila mtu akimtangazia mwenziwe ukombozi, mkaagana hivyo usoni pangu katika Nyumba hii inayoitwa kwa Jina langu.
16
Lakini mkawarudia, mkalitia Jina langu uchafu mkiwarudisha kila mtu mtumwa wake na kijakazi wake, mliowapa ruhusa, wajiendee roho zao zilikotaka, mkawashurutisha kuwa tena watumwa na vijakazi wenu.
17
Kweli hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Hamkunisikia mkimtangazia kila mtu ndugu yake na mwenzake ukombozi. Kwa hiyo ndivyo, asemavyo Bwana: Mtaniona nikiwatangazia ukombozi na kuwaitia panga na magonjwa mabaya na njaa, nitawatoa ninyi, mtupwe huko na huko katika nchi zote zenye wafalme huku nchini.
18
Nao waume waliolivunja agano wasipoyatimiza maneno ya hilo agano, walilolifanya usoni pangu, nitawatoa kuwa kama ndama ya tambiko, waliyoikata vipande viwili, kisha huipitia katikati.
19
Wakuu wa nchi ya Yuda nao wakuu wa Yerusalemu nao wakuu wa nyumba za mfalme nao watambikaji nao watu wote wa nchi hii waliovipitia vipande vya ndama ya tambiko katikati,
20
hao wote nitawatia mikononi mwa adui zao namo mikononi mwao wanaozitafuta roho zao, nayo mizoga yao itakuwa chakula cha ndege wa angani na cha nyama wa porini.
21
Naye Sedekia, mfalme wa Yuda, nao wakuu wake nitawatia mikononi mwao adui zao namo mikononi mwao wanaozitafuta roho zao namo mikononi mwa vikosi vya mfalme wa Babeli, vilivyotoka kwenu kwenda zao.
22
Ndivyo, asemavyo Bwana: Mtaniona nikiwaagiza na kuwarudisha penye mji huu, waupigie vita, wauteke, wauteketeze kwa moto; nayo miji ya Yuda nitaitoa kuwa mapori tu, pasikae mtu.
← Chapter 33
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 35 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52