bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 37
Jeremiah 37
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 36
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 38 →
1
Sedekia, mwana wa Yosia, akawa mfalme mahali pake Konia, mwana wa Yoyakimu, aliyemweka Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, kuwa mfalme wa Yuda.
2
Yeye na watumishi wake na watu wa nchi yake hawakuyasikia maneno ya Bwana, aliyoyasema kwa kumtumia mfumbuaji Yeremia.
3
Mfalme Sedekia akamtuma Yukali, mwana wa Selemia, na Sefania, mwana wa mtambikaji Masea, kwenda kwa Yeremia kumwambia: Tuombee kwake Bwana Mungu wetu!
4
Kwani Yeremia alikuwa akiingia, tena akitoka kwa watu, hawakumfunga katika nyumba ya kifungo.
5
Ndipo, vikosi vya Farao vilipotoka Misri; Wakasidi waliousonga Yerusalemu walipousikia uvumi wao, wakaondoka hapo Yerusalemu.
6
Neno la Bwana likamjia mfumbuaji Yeremia kwamba:
7
Hivi ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyosema: Haya ndiyo, mmwambie mfalme wa Yuda aliyewatuma kwangu kuniuliza: Tazama! Vikosi vya Farao vilivyotoka kwao kuja kuwasaidia wamekwisha kurudi katika nchi yao ya Misri.
8
Lakini Wakasidi watarudi, waupigie mji huu vita; nao watauteka na kuuteketeza kwa moto.
9
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Msijidanganye wenyewe na kusema: Wakasidi wataondoka kwetu kwenda zao! Kwani hawatakwenda.
10
Kwani kama mngevipiga vikosi vyote vya Wakasidi wanaopigana nanyi, wakasalia kwao watu wenye vidonda tu, wangeinuka kila mtu katika hema lake, wauteketeze mji huu kwa moto.
11
Ikawa, vikosi vya Wakasidi vilipoondoka Yerusalemu kwa kuvikimbia vikosi vya Farao,
12
ndipo, Yeremia naye alipotoka Yerusalemu kwenda katika nchi ya Benyamini, alichukue fungu lake lililoko kule kwa watu wa huko katikati.
13
Alipofika penye lango la Benyamini, kulikuwako mkuu wa walinzi, jina lake Iria, mwana wa Selemia, mwana wa Hanania, akamkamata mfumbuaji Yeremia kwamba: Utawaangukia Wakasidi wewe!
14
Yeremia akajibu: Ni uwongo! Mimi siwaangukii Wakasidi, lakini hakumsikia; ndipo, Iria alipomkamata Yeremia na kumpeleka kwa wakuu.
15
Wakuu wakamtolea Yeremia ukali, wakampiga; kisha wakamtia kifungoni nyumbani mwa mwandishi Yonatani, kwani walikuwa wakiitumia kuwa nyumba ya kifungo.
16
Hivi ndivyo, Yeremia alivyoingia katika ile nyumba yenye mashimo yaliyochimbuliwa upande wa ndani chini; ndimo, Yeremia alimokaa siku nyingi.
17
Kisha mfalme Sedekia akatuma kumchukua; mfalme akamwuliza nyumbani mwake penye njama kwamba: Liko neno lililotoka kwa Bwana? Yeremia akasema: Liko; kisha akamwambia: Utatiwa mkononi mwa mfalme wa Babeli.
18
Yeremia akamwuliza mfalme Sedekia: Nimekukosea nini au watumishi wako au watu wa ukoo huu, mkinitia kifungoni?
19
Wako wapi wafumbuaji wenu waliowafumbulia kwamba: Mfalme wa Babeli hatafika kwenu wala katika nchi hii?
20
Sasa sikiliza, bwana wangu mfalme, nayo malalamiko yangu na yakuangukie usoni: Usinirudishe nyumbani mwa Yonatani, nisife mle!
21
Mfalme Sedekia alipotoa amri, wakamfunga Yeremia tena uani penye kifungo, akapewa kila siku mkate wa ngano uliotoka huko, wachoma mikate wanakokaa, mpaka mikate ilipotoweka mjini. Ndivyo, Yeremia alivyopata kukaa uani penye kifungo.
← Chapter 36
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 38 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52