bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 38
Jeremiah 38
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 37
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 39 →
1
Sefatia, mwana wa Matani, na Gedalia, mwana wa Pashuri, na Yukali, mwana wa Selemia, na Pashuri, mwana wa Malkia, wakayasikia yale maneno, Yeremia aliyowaambia watu wote wa ukoo huu kwamba:
2
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Akaaye humu mjini atakufa kwa panga na kwa njaa na kwa magonjwa mabaya; lakini atakayewatokea Wakasidi atapona, roho yake itakuwa pato lake.
3
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Mji huu utatiwa kweli mikononi mwao vikosi vya mfalme wa Babeli, atauteka.
4
Wakuu wakamwambia mfalme: Mtu huyu sharti auawe! Kwani anailegeza mikono ya wapiga vita waliosalia humu mjini, nayo mikono yao wote walio wa ukoo huu, akiwaambia maneno kama hayo; kwani mtu huyu hatafuti, jinsi watu watakavyokaa salama, ila jinsi watakavyoona mabaya.
5
Mfalme Sedekia akawaambia: Tazameni! Yumo mikononi mwenu. Kwani hakuna mfalme awashindaye ninyi jambo lo lote.
6
Wakamchukua Yeremia, wakamtupa katika kisima cha Malkia, mwana wa mfalme, kilichokuwa hapo uani penye kifungo, wakamshusha Yeremia mle kwa kamba. Mle kisimani hamkuwa na maji, ila ni matopetope tu, Yeremia akaanza kuzama matopeni.
7
Mnubi Ebedimeleki aliyekuwa mtumishi nyumbani mwa mfalme akasikia, ya kuwa wamemtumbukiza Yeremia mle kisimani. Siku moja, mfalme alipokaa penye lango la Benyamini,
8
Ebedimeleki akatoka nyumbani mwa mfalme, akaja kusema na mfalme kwamba:
9
Bwana wangu mfalme, yote, watu waliyomfanyizia mfumbuaji Yeremia, ni mabaya, wakimtupa kisimani, afie mle ndani kwa njaa, kwani hamna mkate tena humu mjini.
10
Ndipo, mfalme alipomwagiza yule Mnubi Ebedimeleki kwamba: Chukua hapa kwa mkono wako watu thelathini, umwopoe mfumbuaji Yeremia mle kisimani, angaliko hajafa bado!
11
Ebedimeleki akawachukua wale watu kwa mkono wake, akaingia nyumbani mwa mfalme chumba cha chini cha kuwekea malimbiko, akachukua mle vitambaa vya nguo zilizopasuka na vitambaa vya nguo chakavu, akavishusha kwa kamba kisimani kwake Yeremia.
12
Yule Mnubi Ebedimeleki akamwambia Yeremia: Hivi vitambaa vya nguo zipasukazo na vya nguo chakavu vitie makwapani chini ya kamba! Yeremia akayafanya hivyo.
13
Kisha wakamvuta Yeremia kwa hizo kamba, wakamwopoa kisimani, Yeremia akakaa tena uani penye kifungo.
14
Mfalme Sedekia akatuma kumchukua mfumbuaji Yeremia, aje kwake penye lango la tatu la kuiingilia Nyumba ya Bwana, mfalme akamwambia Yeremia: Mimi ninataka kukuuliza neno, lakini usinifiche lo lote!
15
Yeremia akamwambia Sedekia: Je? Nikikujulisha yote, hutaniua? Tena nikikupa shauri, hutanisikia.
16
Ndipo, mfalme alipomwapia Yeremia penye njama kwamba: Hivyo, Bwana alivyo Mwenye uzima, aliyetuumbia hii roho yetu, sitakuua, wala sitakutia mikononi mwao watu hawa wanaoitafuta roho yako.
17
Ndipo, Yeremia alipomwambia Sedekia: Hivi ndivyo, Bwana Mungu Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema: Kama utawatokea wakuu wa mfalme wa Babeli, roho yako itapona, nao mji huu hautateketezwa kwa moto; hivyo utapona wewe na mlango wako.
18
Lakini usipowatokea wakuu wa mfalme wa Babeli, mji huu utatiwa mikononi mwao Wakasidi, wauteketeze kwa moto, wewe nawe hutapona mikononi mwao.
19
Mfalme Sedekia akamwambia Yeremia: Mimi ninawaogopa Wayuda waliorudi upande wa Wakasidi, wasinitie mikononi mwao, nao wakanizomea.
20
Yeremia akamjibu: Hawatakutoa. Isikie tu sauti ya Bwana, niliyokuambia mimi! Ndivyo, utakavyoona mema, nayo roho yako itapona.
21
Lakini wewe ukikataa kuwatokea, basi, neno, Bwana alilonionyesha, ni hili:
22
Utaona, wanawake wote waliosalia nyumbani mwa mfalme wa Yuda wakitolewa na kupelekwa kwa wakuu wa mfalme wa Babeli; nao watakwenda wakisema: Wamekupoteza, wakakushinda wale, uliotengemana nao! Lakini hapo, miguu yako iliposhikwa na matope, wamerudi nyuma!
23
Wakeo wote na wanao wa kiume wote watawatoa na kuwapeleka kwa Wakasidi, wewe nawe hutapona mikononi mwao, kwani utakamatwa kwa mikono ya mfalme wa Babeli, nao mji huu utateketea kwa moto.
24
Ndipo, Sedekia alipomwambia Yeremia: Mtu ye yote asiyajue haya maneno, wewe usife!
25
Kama wakuu wanasikia, ya kuwa nimesema na wewe, wakija kwako kukuambia: Tusimulie, uliyomwambia mfalme, usitufiche! Hatutakuua, tusimulie nayo, mfalme aliyokuambia!
26
ndipo, utakapowaambia: Mimi nimekuwa nikimlalamikia mfalme na kumwangukia, asinirudishe nyumbani mwa Yonatani, nisifie mle!
27
Wakuu wakaja kwake Yeremia, wakamwuliza, akawaambia hayo maneno yote, kama mfalme alivyomwagiza, wakamwacha na kunyamaza, kwani lile shauri halikujulikana.
28
Kisha Yeremia akakaa uani penye kifungo mpaka siku ile, Yerusalemu ulipotekwa.
← Chapter 37
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 39 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52