bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 42
Jeremiah 42
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 41
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 43 →
1
Wakuu wote wa vikosi na Yohana, mwana wa Karea, na Yezania, mwana wa Hosaya, nao watu wote wa ukoo huu, wadogo kwa wakubwa, wakamjia
2
mfumbuaji Yeremia, wakamwambia: Malalamiko yetu na yakuangukie, utuombee kwa Bwana Mungu wako sisi sote tuliosazwa huku! Kwani tumesalia wachache tu kwa wale wengi, kama macho yako yanavyotuona sisi.
3
Bwana Mungu wako atuonyeshe njia, tutakayoishika, na jambo, tutakalolifanya.
4
Mfumbuaji Yeremia akawaambia: Nimesikia; sasa hivi nitawaombea kwa Bwana Mungu wenu kwa ajili ya njia yenu; kila neno, Bwana atakalowajibu, nitawaambia, sitawanyima neno kamwe.
5
Nao wakamwambia Yeremia: Bwana na awe kwetu shahidi mkweli na mtegemevu kwamba: Kila neno, Bwana Mungu wako atakalokutuma, litakavyotuambia, ndivyo, tutakavyofanya.
6
Kama ni jema au kama ni baya, sauti ya Bwana Mungu wetu tutaisikia, kwa kuwa tunakutuma kwake, kusudi tuone mema tukiisikia sauti ya Bwana Mungu wetu.
7
Siku kumi zilipopita, neno la Bwana likamjia Yeremia,
8
akamwita Yohana, mwana wa Karea, nao wakuu wote wa vikosi waliokuwa naye, nao watu wote wa ukoo huu, wadogo kwa wakubwa,
9
akawaambia: Hivi ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyosema, kwa kuwa mmenituma kwake, kumpelekea malalamiko yenu, yamwangukie,
10
akasema: Mtakapokaa tu katika nchi hii, nitawajenga, nisiwabomoe tena, nitawapanda, nisiwang'oe tena, kwani nitageuza moyo, nisiyafanye yale mabaya, niliyowawazia.
11
Msimwogope mfalme wa Babeli, mnayemwogopa ninyi! Ndivyo, asemavyo Bwana: Msimwogope, kwani mimi niko pamoja nanyi, niwaokoe na kuwaponya mikononi mwake!
12
Nami nitawapatia huruma, awahurumie na kuwarudisha katika nchi yenu.
13
Lakini ninyi mkisema: Hatutakaa katika nchi hii, msiisikie sauti ya Bwana Mungu wenu;
14
mkisema: Hivi sivyo, sharti tuende Misri, maana hatutaona huko vita, wala sauti za mabaragumu hazitasikilika huko, wala hatutaona njaa kwa kukosa chakula, kwa hiyo tunataka kukaa huko;
15
basi, sasa lisikieni neno la Bwana, ninyi mlio masao ya Yuda: Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema: Kama mnazielekeza nyuso zenu kwenda Misri, mkaja kukaa ugenini huko,
16
ndipo, panga, ninyi mnazoziogopa, zitakapowafikia katika nchi ya Misri, nayo njaa inayowatisha itawafuata huko Misri na kugandamana nanyi, kwa hiyo ndiko, mtakakofia.
17
Itakuwa hivyo: Watu wote waliozielekeza nyuso zao kwenda Misri, wakae ugenini huko, watauawa huko kwa panga na kwa njaa na kwa magonjwa mabaya; hawataona pa kuponea wala pa kuyakimbilia mabaya, mimi nitakayowaletea.
18
Kwani hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema: Kama makali yangu yenye moto yalivyomwagiwa wakaao Yerusalemu, ndivyo, mtakavyomwagiwa makali yangu nanyi, mtakapokwenda Misri. Nanyi mtaapizwa kwa kustukiwa, mtazomelewa na kutukanwa, lakini mahali hapa hamtapaona tena.
19
Bwana anawaambia ninyi mlio masao ya Yuda: Msiende Misri! Yajueni kabisa, ya kuwa nimewashuhudia leo!
20
Msiposikia mtazipoteza roho zenu, kwani ninyi wenyewe mmenituma kwa Bwana Mungu wenu kwamba: Tuombee sisi kwa Bwana Mungu wetu! Nayo yote, Bwana Mungu wetu atakayotuambia, tutayafanya vivyo hivyo, kama atakavyotujulisha.
21
Nikawajulisha leo, lakini hamwisikii sauti ya Bwana Mungu wenu na kuyafanya yote, aliyonituma kuwaambia.
22
Kwa hiyo jueni sasa: Panga na njaa na magonjwa mabaya ndiyo yatakayowaua mahali hapo panapowapendeza kupaendea na kukaa ugenini kuko huko.
← Chapter 41
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 43 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52