bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 44
Jeremiah 44
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 43
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 45 →
1
Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kuwaambia Wayuda wote waliokaa katika nchi ya Misri, ndio waliokaa Migidoli na Tahapanesi na Nofu na katika nchi ya Patirosi, la kwamba:
2
Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema: Ninyi mmeyaona hayo mabaya yote, niliyouletea Yerusalemu nayo miji yote ya Yuda, mkaiona, ya kuwa leo ni mavunjiko tu, hamna akaaye humo
3
kwa ajili ya mabaya yao, waliyoyafanya ya kunikasirisha, walipokwenda kuvukizia na kutumikia miungu mingine, wasiyoijua wenyewe, wala ninyi wala baba zenu.
4
Nami nilituma kwenu watumishi wangu wote waliokuwa wafumbuaji pasipo kuchoka kila kulipokucha kuwaambia: Msilifanye neno hilo la kutapisha, ninalochukizwa nalo!
5
Lakini hawakusikia, wala hawakuyatega masikio yao, warudi na kuyaacha mabaya yao, wasivukizie miungu mingine.
6
Ndipo, makali yangu yenye moto yalipomwagika, moto ukawaka katika miji ya Yuda na katika barabara za Yerusalemu, hiyo miji ikawa mavunjiko na mahame, kama inavyojulikana leo.
7
Sasa hivi ndivyo, Bwana Mungu Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema: Mbona mnazifanyizia roho zenu mabaya makuu, mwang'oe kwenu waume na wake, vijana na wachanga, watoweke katikati ya Wayuda, kwenu lisisalie hata sao?
8
Mbona mnanikasirisha kwa matendo ya mikono yenu, mkivukizia miungu mingine huku katika nchi ya Misri, mlikokuja kukaa ugenini tu? Mbona mnataka kujing'oa wenyewe, kusudi mwe wa kuapizwa na wa kutukanwa na mataifa yote ya huku nchini?
9
Je? Mmeyasahau mabaya ya baba zenu na mabaya ya wafalme wa Yuda na mabaya ya wake zao na mabaya yenu na mabaya ya wake zenu, waliyoyafanya katika nchi ya Yuda namo barabarani mwa Yerusalemu?
10
Mpaka siku hii ya leo hawajanyenyekea, wala hawakuogopa, kwani hawaendelei kwa Maonyo wala kwa maongozi yangu, niliyowapa ninyi na baba zenu, yawe machoni penu.
11
Kweli hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema: Mtaniona, nikiwaelekezea uso wangu, niwafanyizie mabaya na kuwang'oa Wayuda wote pia.
12
Nitawachukua masao ya Wayuda waliozielekeza nyuso zao kuja katika nchi ya Misri kukaa ugenini huku. Watamalizika wote katika nchi ya Misri, wakiuawa kwa panga na kwa njaa; kwa hiyo watamalizika wadogo kwa wakubwa wakifa kwa panga na kwa njaa; nao wataapizwa kwa kustukiwa, watazomelewa na kutukanwa,
13
nikiwapatiliza wakaao katika nchi ya Misri, kama nilivyowapatiliza Wayerusalemu kwa panga na kwa njaa na kwa magonjwa mabaya.
14
Hawatapata pa kuponea wala pa kukimbilia wale walio masao ya Wayuda waliokuja katika nchi ya Misri kukaa ugenini huku, wapate kurudi halafu katika nchi ya Yuda, roho zao zinayoitunukia, warudi huko na kukaa; kwani hawatarudi, isipokuwa watoro tu.
15
Wakamjibu Yeremia waume wote waliojua, ya kuwa wake zao huvukizia miungu mingine, nao wake wote waliosimama hapo mkutano mkubwa, nao wote wa ukoo huu waliokaa Patirosi katika nchi ya Misri, wakasema:
16
Neno hili, ulilotuambia katika Jina la Bwana, kwetu sisi hakuna atakayekusikia.
17
Kwani tutayafanya kabisa maneno yote yaliyotoka vinywani mwetu, tumvukizie mfalme wa kike wa mbinguni na kummwagia vinywaji vya tambiko, kama tulivyofanya sisi na baba zetu na wafalme wetu na wakuu wetu katika miji ya Yuda namo barabarani mwa Yerusalemu, tukashiba vyakula, tukafanikiwa, lakini mabaya hatukuyaona.
18
Toka hapo, tulipoacha kumvukizia mfalme wa kike wa mbinguni na kummwagia vinywaji vya tambiko, ndipo, tulipokosa yote, tukamalizika kwa panga na kwa njaa.
19
Tena tukimvukizia mfalme wa kike wa mbinguni na kummwagia vinywaji vya tambiko, je? Waume wetu hawako, tukimtengenezea mikate yenye mifano yake na kummwagia vinywaji vya tambiko?
20
Yeremia akawaambia watu wote wa ukoo huu, waume kwa wake na watu wote pia waliomjibu neno hilo, akasema:
21
Kweli mmevukiza mavukizo katika miji ya Yuda namo barabarani mwa Yerusalemu ninyi na baba zenu, wafalme wenu na wakuu wenu nao watu wote waliokuwako katika nchi. Lakini hayo ndiyo, Bwana aliyoyakumbuka, akayaweka moyoni mwake.
22
Kwa hiyo Bwana hakuweza kuvumilia tena kwa ajili ya ubaya wa matendo yenu na kwa ajili ya matapisho, mliyoyafanya; ndipo, nchi ilipogeuka kuwa mavunjiko na mapori tu, ikaapizwa, pasiwepo aikaaye, kama ilivyo siku hizi.
23
Kwa kuwa mmevukiza na kumkosea Bwana, mkakataa kuisikia sauti yake na kuendelea kwa Maonyo yake na kwa maongozi yake na kwa mashuhuda yake, kwa sababu hii yamewafikia haya mabaya, mnayoyaona siku hizi.
24
Yeremia akawaambia waume wote wa ukoo huu nao wake wote: Lisikieni neno la Bwana, ninyi Wayuda wote mlioko katika nchi ya Misri!
25
Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema kwamba: Ninyi na wake zenu mliyoyasema kwa vinywa vyenu, myamalize kwa mikono yenu, yale ya kwamba: Tutayafanya kabisa maagano yetu, tuliyoyaapiana ya kumvukizia mfalme wa kike wa mbinguni na kummwagia vinywaji vya tambiko, basi, vitimizeni viapo vyenu! Vifanyizeni kabisa hivyo viapo vyenu!
26
Lakini lisikieni neno la Bwana, ninyi Wayuda wote mkaao katika nchi ya Misri! Bwana anasema: Tazameni, nimeapa katika Jina langu kubwa kwamba: Jina langu lisitajwe tena katika nchi yote ya Misri vinywani mwa watu wa Kiyuda wo wote wakisema: Hivyo, Bwana Mungu alivyo Mwenye uzima!
27
Mtaniona, nikiwa macho kuyaangalia mabaya, nitakayowafanyizia, siyo mema! Ndipo, watakapomalizika watu wote wa Kiyuda walioko katika nchi ya Misri kwa panga na kwa njaa, mpaka watakapokuwa wamekwisha.
28
Nao watakaopona panga watatoka katika nchi ya Misri, warudi katika nchi ya Yuda, lakini watakuwa wachache sana, mkiwahesabu. Ndipo, masao yote ya Yuda waliokuja Misri kukaa ugenini huku watakapojua, kama ni neno lipi litakalosimama, langu au lao.
29
Ndivyo, asemavyo Bwana: Hiki kitakuwa kielekezo chenu cha kwamba: Mimi nitawapatiliza mahali hapa, kusudi mjue, ya kuwa maneno yangu hutimilika kweli na kuwapatia mabaya.
30
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Mtaniona, nikimtia Farao Hofura, mfalme wa Misri, mikononi mwa adui zake namo mikononi mwao wanaoitafuta roho yake, kama nilivyomtia Sedekia, mfalme wa Yuda, mkononi mwa adui yake Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, aliyeitafuta roho yake.
← Chapter 43
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 45 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52