bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 46
Jeremiah 46
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 45
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 47 →
1
Hili ndilo neno la Bwana lililomjia mfumbuaji Yeremia kwa ajili ya wamizimu.
2
Yatakayowapata Wamisri. Kwa ajili ya vikosi vya Farao Neko, mfalme wa Misri, vilivyokuwa Karkemisi penye mto wa Furati, vilipopigwa na Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, katika mwaka wa nne wa Yoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, anasema:
3
Tengenezeni ngao ndogo na kubwa, mwende vitani!
4
Watandikeni farasi, wapandeni, ninyi wapanda farasi! Jipangeni, wenye kofia za chuma vichwani! Inoeni mikuki, kisha zivaeni shati za chuma!
5
Mbona ninawaona hawa, wakirudi nyuma kwa kustuka? Mbona wanguvu wao wamepondeka, wakakimbia sana pasipo kugeuka? Matisho po pote! ndivyo, asemavyo Bwana.
6
Lakini naye mwenye miguu miepesi hatakimbia, wala mwenye nguvu hatapona. Upande wa kaskazini kando ya mto wa Furati wamejikwaa, wakaanguka.
7
Alikuwa nani aliyepanda kama mto wa Nili, maji yake yakajirusha kama ya mito mikubwa?
8
Mmisri alipanda kama mto wa Nili, maji yakajirusha kama ya mito mikubwa, akasema: Nitapanda kuifunikiza nchi, niangamize mji nao wakaao humo!
9
Pandeni, ninyi farasi! Pigeni mbio kama wenye wazimu, ninyi magari! Wapiga vita na watokee, wale Wanubi na Waputi washikao ngao na Waludi washikao pindi, wajuao kuzivuta!
10
Siku hii ni yake Bwana Mungu Mwenye vikosi, ni siku ya lipizi ya kuwalipiza wapingani wake, panga zitakula, zishibe, mpaka zilewe kwa damu zao, kwani wao ndio kama ng'ombe za kumtambikia Bwana Mungu Mwenye vikosi katika nchi ya upande wa kaskazini kwenye mto wa Furati.
11
Pandeni Gileadi kuchukua mafuta ya kwaju, ninyi wanawali mliozaliwa Misri! Ni bure, ukitumia dawa nyingi, hakuna itakayokuponya.
12
Mataifa yameyasikia yakutiayo soni, vilio vyako vimeijaza nchi. Kwani mpiga vita amejikwaa kwa mpiga vita mwenziwe, wakaanguka wote wawili pamoja.
13
Hili ndilo neno, Bwana alilomwambia mfumbuaji Yeremia, Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, alipokuja kuipiga nchi ya Misri:
14
Pigeni mbiu huko Misri na kuitangaza Migidoli! Tena itangazeni Nofu na Tahapanesi kwamba: Jipangeni na kujitengeneza! Kwani panga zimewala waliokuzunguka.
15
Mbona watukufu wako wamelazwa chini? Hawakusimama, kwani Bwana aliwakumba;
16
akakwaza wengi, wakaangukiana mtu na mwenziwe wakiambiana: Inuka, turudi kwetu kwa wenzetu wa ukoo katika nchi, tulikozaliwa, tuzikimbie panga za wanguvu!
17
Ndiko, walikomwita Farao, mfalme wa Misri: Angamio, ameikosa siku yake ya kupona!
18
Ndivyo, asemavyo Mfalme, Jina lake Bwana Mwenye vikosi: Hivyo, nilivyo Mwenye uzima, atakuja afananaye na Tabori ulio mkuu wa kuipita milima mingine au na Karmeli huko pwani.
19
Jifanyizieni vyombo vya kwenda navyo mkitekwa, ninyi wanawali mkaao Misri! Kwani Nofu utakuwa mahame tu kwa kuteketea, msikae mtu.
20
Misri ni mori mzuri mno, lakini mbung'o anakuja upesi toka kaskazini.
21
Nao warugaruga wao waliokuwa kwao kama ndama wenye manono, hao nao wamegeuka, wakakimbia wote pamoja, hawakusimama, kwani siku ya kuangamia kwao iliwafikia, ndio wakati wa kupatilizwa kwao.
22
Mashindo yao yakawa kama ya nyoka akikimbia, kwani wale wanakuja na vikosi vyao, wanawajia wakishika mashoka kama wakata kuni.
23
Ndivyo, asemavyo Bwana: Wataikata misitu yao isiyochunguzika, kwani ni wengi kuliko nzige, hawahesabiki.
24
Wanawali wa Misri, wamepatwa na soni kwa kutiwa mikononi mwa watu waliotoka kaskazini.
25
Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anasema: Mtaniona, ninavyompatiliza Amoni wa No naye Farao na nchi yake ya Misri hata miungu yake na wafalme wake; nitampatiliza Farao kweli nao wote wamwegemeao.
26
Nitawatia mikononi mwao wanaozitafuta roho zao, namo mikononi mwa Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, namo mikononi mwa watumishi wake. Lakini hayo yatakapokwisha, nchi itakaa watu kama siku za kale; ndivyo, asemavyo Bwana.
27
Wewe mtumishi wangu Yakobo, usiogope! Nawe Isiraeli, usistuke! Kwani utaniona, nikikuokoa na kukutoa huko mbali, nao walio kizazi chako nitawatoa katika ile nchi, walikopelekwa kwa kutekwa. Yakobo atarudi, akae na kutulia pasipo kuhangaika, kwani hakuna atakayemstusha.
28
Ndivyo, asemavyo Bwana: Wewe ntumishi wangu Yakobo, usiogope! Kwani mimi niko pamoja na wewe, kwani nitayamaliza mataifa yote, ambayo nimekutupa kwao, lakini wewe sitakumaliza, nitakuchapa tu, kama yakupasavyo, nisikuache pasipo patilizo lo lote.
← Chapter 45
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 47 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52