bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 48
Jeremiah 48
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 47
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 49 →
1
Yatakayowapata Wamoabu. Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema: Nebo yameupata, kwani umebomolewa! Kiriatemu umepatwa na soni kwa kutekwa, kweli boma lake lililokuwa mlimani limepatwa na soni kwa kustuka.
2
Hakuna tena utukufu wa Moabu; mle Hesiboni wanawawazia mabaya kwamba: Twende, tuwang'oe, wasiwe kabila! Nawe Madimeni, utanyamazishwa, panga zitakufuata nyuma.
3
Toka Horonemu kunasikilika makelele, maangamizo na mavunjiko ni makubwa.
4
Wamoabu wamevunjika, vilio vinasikilika hata Soari.
5
Kwani njia ya kupandia Luhiti wanaipanda na kulia, hata katika njia ya kutelemkia toka Horonemu kunasikilika yowe zao wasongekao kwa ajili ya mavunjiko kwamba:
6
Kimbieni! Ziponyeni roho zenu! Mwe kama mti wa nyikani usio na majani!
7
Kwa kuwa unayaegemea matendo yako na vilimbiko vyako, wewe nawe utatekwa, naye Kemosi hana budi kwenda kuhamishwa pamoja na watambikaji wake na wakuu wake.
8
Mwangamizaji ataujia kila mji, hakuna mji utakaopona, penye bonde pataangamia, napo penye mbuga pataharibika, kama Bwana alivyosema.
9
Wapeni Wamoabu mabawa, watoke na kuruka! Kwani miji yao itakuwa mapori, msikae mtu.
10
Ameapizwa afanyaye kazi ya Bwana na kulegea! Ameapizwa auzuiaye upanga, usiue!
11
Wamoabu walikaa pasipo kuhangaishwa tangu ujana wao, wakatulia penye mvinyo zao zenye shimbi, hawazitoi chomboni na kumimina katika kingine, wala hawajakwenda kuhamishwa; kwa hiyo yapendezayo vinywa vyao kuyala ni yaleyale, nayo yapendezayo pua zao kuyanusa hayakugeuka.
12
Ndivyo, asemavyo Bwana: Kwa hiyo wataona, siku zikija, nitakapotuma kwao mafundi wa mvinyo, watavipindua vyombo vyao na kuzimwaga mvinyo zilizomo, kisha wataivunja hiyo mitungi yao.
13
Ndipo, Wamoabu watakapoona soni kwa ajili ya Kemosi, kama walio wa mlango wa Isiraeli walivyoona soni kwa ajili ya Beteli mlimokuwa na egemeo lao.
14
Mwasemaje: Sisi tu wenye nguvu, tu mafundi wa kupiga vita?
15
Wamoabu wataangamia, miji yao itapandiwa, nao vijana wao waliochaguliwa watakuwa hawana budi kutelemka, wauawe; ndivyo, asemavyo Mfalme, Jina lake ni Bwana Mwenye vikosi.
16
Angamio lao Wamoabu liko karibu, mabaya yao yanakuja upesi sana.
17
Nyote mkaao na kuwazunguka waombolezeeni pamoja nao wote walijuao jina lao! Semeni: Kumbe fimbo yenye nguvu imevunjika! Nayo ilikuwa bakora yenye utukufu!
18
Ondokeni penye utukufu, mkae mchangani penye ugumu, ninyi wanawali mkaao Diboni! Kwani mwenye kuwaangamiza Wamoabu anapanda kufika kwako, ayabomoe maboma yako!
19
Ninyi mkaao Aroeri, simameni njiani na kupeleleza mkiwauliza watoro walioepuka, mkisema: Kumetendeka nini?
20
Wamoabu wamepatwa na soni kwa kuvunjika; lieni na kupaza sauti: Yatangazeni kwenye Arnoni, ya kuwa Wamoabu wameangamia!
21
Mapatilizo yameijia nchi yenye mbuga huko Holoni na Yasa na Mefati,
22
na Diboni na Nebo na Beti-Dibulatemu,
23
na Kiriatemu na Beti-Gamuli na Beti-Meoni,
24
na Kirioti na Bosira na miji yote ya nchi ya Moabu iliyoko mbali, nayo iliyoko karibu.
25
Pembe ya Moabu imekatwa, nao mkono wake umevunjwa; ndivyo, asemavyo Bwana.
26
Walevyeni! Kwani wamejikuza kuliko Bwana; na waanguke kifudifudi katika matapiko yao, wachekwe nao hao!
27
Au Waisiraeli hawakuchekwa kwenu? Je? Walionwa kwenye wezi, mkiwatingishia vichwa kila mlipowataja?
28
Ninyi mkaao Moabu, tokeni mijini, mkae magengeni, mwe kama hua wanaojenga matundu yao juu penye miamba iliyokatika.
29
Tumesikia, ya kuwa Wamoabu walijivuna sanasana, wakajikuza kwa kujivuna kwao, kwa kiburi chao wakawaza makuu mioyoni mwao.
30
Ndivyo, asemavyo Bwana: Mimi nimeyajua makorofi yao, ya kuwa hayana maana, nayo maneno yao makuu, ya kuwa hawakuyafanya.
31
Kwa hiyo ninawalilia Wamoabu, ninawapigia Wamoabu wote makelele; wengine wanawapigia kite watu wa Kiri-Heresi.
32
Kuliko Yazeri ninawalilia ninyi mizabibu ya Sibuma, matawi yenu yaliendelea kufika baharini, yalifika kweli kwenye bahari ya Yazeri; siku za kiangazi walipochuma zabibu zenu, mara mwangamizaji akaja.
33
Ndipo, shangwe za furaha zilipotoweka Karmeli na katika nchi ya Moabu. Nayo mvinyo iliyokuwa kamulioni nikaikomesha, hawakamui tena kwa kupiga shangwe; shangwe zao sizo shangwe tena.
34
Toka Hesiboni wanapiga makelele, hata Elale na Yasa wanapaza sauti zao, tena toka Soari hata Horonemu na Eglati-Selisia hulia, ya kuwa nayo maji ya Nimurimu yatakuwa yamekauka.
35
Ndivyo, asemavyo Bwana: Nitawakomesha Wamoabu, wasipande vilimani kuivukizia miungu yao.
36
Kwa hiyo moyo wangu unawapigia Wamoabu kite na kuvuma kama zomari, nao watu wa Kiri-Heresi moyo wangu unawapigia kite na kuvuma kama zomari, kwa kuwa mapato waliyojipatia yamepotea.
37
Kwani vichwa vyote vitakuwa vyenye vipara, nazo ndevu zote zitakuwa zimenyolewa, nayo mikono yote itakuwa yenye chale, navyo viuno vyote vitakuwa na magunia.
38
Po pote vipaani katika nchi ya Moabu napo barabarani po pote patakuwa na maombolezo, kwani nitawavunja Wamoabu, kama ni chombo kisichopendeza; ndivyo, asemavyo Bwana.
39
Kumbe wamevunjika! Pigeni vilio! Kumbe Wamoabu wamezigeuza kosi zao kwa soni! Tangu hapo Wamoabu watakuwa kicheko na kitisho kwao wote wakaao na kuwazunguka.
40
Kwani hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Tazameni, anawarukia Wamoabu kama kozi na kuwakunjulia mabawa yake.
41
Kirioti umetekwa, nayo miji yenye maboma imechukuliwa; kwa hiyo mioyo ya wapiga vita wa Moabu itakuwa siku ile kama moyo wa mwanamke anayetaka kuzaa.
42
Wamoabu wataangamizwa, wasiwe taifa tena, kwa kuwa wamejikuza kuliko Mungu.
43
Mastuko na miina na matanzi yatawapata ninyi mkaao Moabu; ndivyo, asemavyo Bwana.
44
Ayakimbiaye mastuko ataanguka mwinani; atokaye mwinani atakamatwa na tanzi; haya yatakuwa hapo, nitakapowatimilizia hao Wamoabu mwaka wa mapatilizo yao; ndivyo, asemavyo Bwana.
45
Watoro wakisimama kivulini kwenye Hesiboni kwa kuishiwa nguvu, moto utatoka Hesiboni namo Sihoni kati, moto uwakao sana utatoka, utavila vipanja vya Wamoabu nazo tosi zao wapigao vita.
46
Yatawapata, ninyi Wamoabu! Ukoo wake Kemosi utaangamia! Kwani wanao wa kiume watachukuliwa kwenda utumwani, nao wanao wa kike watakwenda kuwa vijakazi.
47
Kisha nitayafungua mafungo ya Moabu, siku zitakapotimia; ndivyo, asemavyo Bwana. Mpaka hapa ni hukumu za Moabu.
← Chapter 47
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 49 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52