bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 49
Jeremiah 49
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 48
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 50 →
1
Yatakayowapata wana wa Amoni. Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Je? Hakuna wana kwao Waisiraeli? Hakuna awezaye kulichukua fungu lake? Mbona Malkamu ameichukua nchi ya Gadi nao watu wa ukoo wake wanakaa katika miji yao?
2
Ndivyo, asemavyo Bwana: Wataona, siku zikija, nitakapovumisha makelele ya vita huko Rabati ulio mji wa wana wa Amoni, nao utakuwa machungu ya mabomoko, nayo miji ya wana wao itateketezwa kwa moto; ndipo, Waisiraeli watakapoyachukua mafungu yao kwao walioyachukua. Ndivyo, Bwana anavyosema:
3
Pigeni vilio, ninyi wa Hesiboni, ya kuwa Ai umebomolewa! Pigeni makelele, ninyi wanawali wa Raba! Jifungeni magunia! Ombolezeni na kwenda huko na huko penye nyua! Kwani Malkamu atakwenda kutekwa na kuhamishwa pamoja na watambikaji wake na wakuu wake.
4
Mnayasifiaje mabonde zaidi, mlio na bonde lichuruzikalo maji, ninyi wanawali wakatavu? Mnaviegemea vilimbiko vyenu kwamba: Yuko nani atakayenijia?
5
Ndivyo, asemavyo Bwana Mungu Mwenye vikosi: Mtaniona, nikiwaletea mastusho toka pande zote pia, nanyi mtafukuzwa, kila mtu akimbie pasipo kutazama nyuma, tena hatakuwako atakayewakusanya hao watoro.
6
Hayo yatakapokwisha, nitayafungua mafungo ya wana wa Amoni.
7
Yatakayowapata Waedomu. Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Je? Huko Temani hakuna tena werevu wa kweli? Wajuzi wamepotelewa na akili, werevu wao wa kweli ukatoweka?
8
Kimbieni, mtoroke! Chimbeni mashimo ya kukaa ndani yao, ninyi mkaao Dedani! Kwani nitawaletea angamio la Esau siku ya kuwapatiliza.
9
Kama wachuma zabibu wanakujia, hawasazi za kuokoteza; kama wezi wanakujia na usiku, hupokonya, mpaka wakitoshewa.
10
Kwani mimi nimemvumbua Esau, nikayafunua maficho yake, asiweze kujificha tena. Kizazi chake kumeharibiwa pamoja na ndugu zake, nao waliokaa nao hawako kabisa.
11
Waacheni watoto wenu waliofiwa na wazazi! Mimi nitawatunza; nao wajane wenu na waniegemee!
12
Kwani hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Tazama, wasiopaswa kukinywa kinywaji changu hawakuwa na budi kukinywa, nawe wewe usilipishwe? Nawe utalipishwa, kwani utakinywa!
13
Ndivyo, asemavyo Bwana: Nimejiapia mwenyewe kwamba: Bosira sharti ustukiwe kwa kutiwa soni, ukae peke yake kwa kuapizwa, nayo miji yake yote itakuwa mabomoko kale na kale.
14
Nimesikia mbiu kwake Bwana, mjumbe ametumwa kwenda kwa mataifa kwamba: Jikusanyeni, mwujie! Ondokeni kwenda vitani!
15
Kwani mtaniona, nikiwafanya kuwa wadogo katika mataifa, mbezwe na watu!
16
Kuogopesha kwenu ni majivuno tu ya mioyo yenu yaliyowadanganya, kwa kuwa mnakaa nyufani kwenye miamba, mkagandamana na milima mirefu. Lakini ijapo mvijenge vituo vyenu juu kabisa kama tai, huko nako nitawashusha; ndivyo, asemavyo Bwana.
17
Nchi ya Edomu itakuwa mapori matupu, kila atakayepapita atastuka na kuyazomea mapigo yake yote.
18
Bwana anasema: Kama Sodomu na Gomora ilivyoangamizwa pamoja na vijiji vyao, hivyo napo hapo hapatakaa mtu, wala hapatalala mgeni wa kimtu.
19
Kama simba anavyopanda akitoka machakani kwenye Yordani, ajie maboma yenye nguvu, ndivyo, nitakavyowakimbiza kwao kwa mara moja, naye aliyechaguliwa nitamweka kuwa mkuu wao, kwani yuko nani afananaye na mimi? Au yuko nani atakayeniwekea siku? Yuko mchungaji gani atakayesimama usoni pangu?
20
Kwa hiyo lisikieni shauri la Bwana, alilowakatia Waedomu, nayo mawazo yake, aliyowawazia wakaao Temani: kweli watakaowakokotakokota ndio wadogo wa makundi, kweli nchi yao yenyewe itawastukia.
21
Kwa mtutumo wa kuanguka kwao nchi itatetemeka, nazo sauti za vilio vyao zitasikilika hata kwenye Bahari Nyekundu.
22
Tazameni, anaurukia Bosira kama kozi na kuukunjulia mabawa yake. Kwa hiyo mioyo ya wapiga vita wa Edomu itakuwa siku ile kama moyo wa mwanamke anayetaka kuzaa.
23
Yatakayoupata Damasko. Hamati na Arpadi wamepatwa na soni, kwani wamesikia mbiu mbaya, wakayeyuka na kuhangaika kama bahari isiyoweza kutulia.
24
Wadamasko wamelegea, wakageuka, wakimbie, mtetemeko ukawashika, masongano na machungu yakawapata kama mwanamke anayetaka kuzaa.
25
Kumbe umeachwa wote mji huo uliokuwa mji, walimoshangilia kwa kufurahi!
26
Kwa hiyo wavulana wake wataanguka barabarani mwake, nao wapiga vita wote watanyamazishwa siku ile; ndivyo, asemavyo Bwana Mwenye vikosi.
27
Kisha nitawakisha moto bomani mwa Damasko, uyale majumba ya Beni-hadadi.
28
Yatakayoipata nchi ya Kedari nazo nchi za kifalme za Hasori, Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, alizozipiga. Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Inukeni, mpande kwenda Kedari, mwaangamize wana wa nchi iliyoko maawioni kwa jua!
29
Na wayachukue mahema yao na makundi yao, wajitwalie mazulia yao na vyombo vyao vyote na ngamia wao, nao watawalilia kwamba: Matisho po pote!
30
Kimbieni na kupiga mbio sana! Chimbeni mashimo ya kukaa ndani yao, ninyi mkaao Hasori! ndivyo, asemavyo Bwana; kwani Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, amewakatia shauri na kuwawazia mawazo.
31
Ndivyo, asemavyo Bwana: Inukeni, mpande kwenda kwa taifa lililojituliza na kukaa pasipo mahangaiko! Hawama milango wala makomeo, hujikalia peke yao tu.
32
Ngamia wao watakuwa mateka yenu, nao kondoo na mbuzi wao wengi mno watakuwa mapato yenu. Wao wenyewe wanyoao denge nitawatawanya kwenda pande zote, upepo utokako, nikiwaletea maangamizo, yawatokee po pote; ndivyo, asemavyo Bwana.
33
Ndipo, Hasori utakapokuwa kao la mbwa wa mwitu kwa kukaa peke yao tu kale na kale. Hapatakaa mtu, wala hapatalala mgeni wa kimtu.
34
Hili ndilo neno la Bwana lililomjia mfumbuaji Yeremia kuwaambia Waelamu, Sedekia, mfalme wa Yuda, alipoanzia kuwa mfalme.
35
Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Mtaniona, nikizivunja pindi zao Waelamu, nguvu zao nyingi zilimo.
36
Nitawaletea Waelamu pepo nne zitokazo pande nne za mbinguni, niwatawanye kwenye hizo pepo, pasiwe taifa lisilojiwa na watoro wa nchi ya Elamu.
37
Nitawastusha Waelamu, wawaogope adui zao nao wazitafutao roho zao; kisha nitawaletea mabaya, makali yangu yenye moto yatakapowawakia, mpaka niwamalize.
38
Ndipo, nitakapokiweka kiti changu cha kifalme huko Elamu, nimwangamize mfalme na wakuu, watoweke huko; ndivyo, asemavyo Bwana.
39
Lakini siku zitakapotimia, nitayafungua mafungo ya Waelamu; ndivyo, asemavyo Bwana.
← Chapter 48
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 50 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52