bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 52
Jeremiah 52
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 51
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
1
Sekedia alikuwa mwenye miaka 21 alipopata ufalme, akawa mfalme mle Yerusalemu miaka 11; jina la mama yake ni Hamutali, binti Yeremia, wa Libuna.
2
Akayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana kama yote, Yoyakimu aliyoyafanya.
3
Kwa kuwa Bwana aliwakasirikia Wayerusalemu na Wayuda, akawatupa, waondoke usoni pake, ikawa hivyo: Sedekia akakataa kumtii mfalme wa Babeli.
4
Ikawa katika mwaka wa 9 wa ufalme wake mwezi wa kumi siku ya kumi ya mwezi, ndipo, Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, alipoujia Yerusalemu yeye na vikosi vyake vyote, wakapiga makambi huko, wakaujengea boma la kuuzungusha.
5
Mji ukaja kusongwa hivyo na kuzingwa mpaka mwaka wa 11 wa mfalme Sedekia.
6
Katika mwezi wa nne siku ya tisa njaa ikazidi mle mjini, watu wa nchi hii hawakuwa na vyakula.
7
Ndipo, mji ulipobomolewa, nao wapiga vita wote wakatoroka na kutoka mjini na usiku kwa njia ya lango lililokuwa kati ya kuta mbili penye bustani ya mfalme; Wakasidi walipokuwa wamelala usingizi na kuuzunguka mji, wale wakashika njia ya nyikani.
8
Kisha vikosi vya Wakasidi vikamfuata mfalme na kupiga mbio, vikampata Sedekia katika nyika ya Yeriko, navyo vikosi vyake vyote vilikuwa vimetawanyika na kumwacha.
9
Wakamkamata mfalme, wakampeleka kwa mfalme wa Babeli huko Ribula katika nchi ya Hamati, akasema naye na kumhukumu.
10
Mfalme wa Babeli akawaua wana wa Sedekia machoni pake, nao wakuu wote wa Wayuda akawaua huko Ribula.
11
Kisha akayapofua macho yake Sedekia, akamfunga kwa minyororo; kisha mfalme wa Babeli akampeleka Babeli, akamtia kifungoni mpaka siku ya kufa kwake.
12
Katika mwezi wa tano siku ya kumi ya mwezi, - ulikuwa mwaka wa 19 wa mfalme Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, - ndipo, Nebuzaradani, mkuu wao waliomlinda mfalme, aliyesimama usoni pa mfalme wa Babeli, alipoingia Yerusalemu.
13
Akaiteketeza Nyumba ya Bwana na nyumba ya mfalme, nazo nyumba zote za Yerusalemu, nazo nyumba kubwa zote akaziteketeza kwa moto.
14
Kisha vikosi vyote vya Wakasidi waliokuwa na mkuu wao waliomlinda mfalme vikazibomoa kuta za boma lililouzunguka Yerusalemu.
15
Kisha Nebuzaradani, mkuu wao waliomlinda mfalme, akawateka na kuwahamisha wanyonge wa ukoo huo nayo masao ya watu waliosalia mjini nao waliokuwa wamemwangukia mfalme wa Babeli na kurudi upande wake nao mafundi waliosalia.
16
Lakini kwa wanyonge wa nchi Nebuzaradani, mkuu wao waliomlinda mfalme, wengine akawasaza, waiangalie mizabibu, wengine walime tu.
17
Lakini zile nguzo mbili za shaba zilizokuwa penye Nyumba ya Bwana na vile vilingo vya kuwekea mitungi ya maji na bahari ya shaba iliyokuwa penye Nyumba ya Bwana Wakasidi wakazivunja, nazo zile shaba zao zote wakazipeleka Babeli.
18
Hata masufuria na majembe na makato ya kusafishia mishumaa na vyano na kata navyo vyombo vyote pia vya shaba vilivyotumiwa Nyumbani mwa Bwana wakavichukua.
19
Nazo sahani na mikungu na mabakuli na vyano na taa na vijiko na vivukizio vilivyokuwa vya dhahabu tupu navyo vilivyokuwa vya fedha tupu mkuu wao waliomlinda mfalme akavichukua.
20
Zile nguzo mbili na ile bahari moja na zile ng'ombe kumi na mbili zilizokuwa chini yake na vile vilingo vya kuwekea mitungi ya maji, ambavyo mfalme Salomo alivitengenezea Nyumba ya Bwana, shaba zao hivyo vyombo vyote hazikuwezekana kupimwa kwa mizani.
21
Zile nguzo urefu wake nguzo moja ulikuwa mikono kumi na nane, nayo kamba ya mikono kumi na miwili ikaizunguka, unene wa shaba ulikuwa nyanda nne, ndani palikuwa penye uvurungu.
22
Juu yake palikuwa na kilemba cha shaba, urefu wa kwenda juu wa hiki kilemba kimoja ulikuwa mikono mitano; hiki kilemba kilikuwa kimezungukwa na misuko kama ya mkeka iliyokuwa yenye komamanga, yote pia ni ya shaba; nayo nguzo ya pili ilikuwa vivyo hivyo, nayo ilikuwa yenye komamanga.
23
Komamanga zilikuwa tisini na sita zilizoning'inia; komamanga zote penye msuko wa nguzo moja zilikuwa mia.
24
Mkuu wao waliomlinda mfalme akamchukua mtambikaji mkuu Seraya na mtambikaji wa pili Sefania nao walinda kizingiti watatu.
25
Namo mjini akachukua mtumishi mmoja wa nyumbani mwa mfalme aliyewekwa kuwa mkuu wa kuwasimamia wapiga vita na watu saba waliokuwa na kazi machoni pa mfalme waliopatikana mjini na mwandishi wa mkuu wa vikosi aliyewaandika watu wa nchi waliotakiwa uaskari na watu sitini wa shambani waliopatikana mle mjini.
26
Hao akawachukua Nebuzaradani, mkuu wao waliomlinda mfalme, akawapeleka Ribula kwa mfalme wa Babeli.
27
Naye mfalme wa Babeli akawapiga na kuwaua huko Ribula katika nchi ya Hamati. Kisha akawahamisha Wayuda, waitoke nchi yao.
28
Watu wa ukoo huu, Nebukadinesari aliowahamisha katika mwaka wa saba, ndio hawa: Wayuda 3023.
29
Katika mwaka wa kumi na nane wa ufalme wa Nebukadinesari waliohamishwa Yerusalemu ni 832.
30
Katika mwaka wa ishirini na tatu wa ufalme wa Nebukadinesari, Nebuzaradani, mkuu wao waliomlinda mfalme, akahamisha Wayuda 745; wote pamoja walikuwa 4600.
31
Ikawa katika mwaka wa 37 wa kuhamishwa kwake Yoyakini, mfalme wa Wayuda, katika mwezi wa kumi na mbili siku ya ishirini na tano, ndipo, Ewili-Merodaki, mfalme wa Babeli, alipomwonea uchungu Yoyakini, mfalme wa Wayuda; ikawa katika mwaka huohuo, alipoupata ufalme, akamtoa kifungoni,
32
akasema naye maneno mema, akampa kiti chake cha kifalme juu ya viti vya kifalme vya wafalme wengine waliokuwa naye huko Babeli.
33
Ndipo, alipoyavua mavazi yake ya kifungoni, akala chakula usoni pa mfalme pasipo kukoma siku zote, alizokuwapo.
34
Nazo mali za kujitunza kila siku akapewa na mfalme wa Babeli siku zote, alizokuwapo, akapata siku kwa siku yaliyompasa mpaka siku ya kufa kwake.
← Chapter 51
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52