bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 6
Jeremiah 6
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 7 →
1
Jihimizeni kukimbia, ninyi wana wa Benyamini, mtoke Yerusalemu! Namo Tekoa pigeni baragumu! Nako kwenye Beti-Keremu twekeni bendera, kwani toka kaskazini yanakuja mabaya yanayotisha na mavunjiko yaliyo makuu.
2
Binti Sioni aliye mzuri aliyejizoeza mororo nitamwangamiza.
3
Watakuja kwake wachungaji na makundi yao, watapiga mahema kwake na kumzinga, walishe kila mmoja fungu lake wakisema: Jitakaseni, mpigane nao!
4
Inukeni, tupapandie, jua lingaliko juu! A, tumechelewa sisi! Jua linataka kuchwa, vivuli vya jioni vinajivuta.
5
Inukeni! Tupande na usiku, tuyaharibu majumba yake!
6
Kwani ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Kateni miti, kisha mwifukie kuwa boma la kuuzinga Yerusalemu! Maana ndio mji utakaopatilizwa kwa ajili ya ukorofi uliomo mwake.
7
Kama kisima kinavyoyatoa maji yake, ndivyo, unavyoyatoa mabaya yake. Makorofi na mapotovu husikilika mwake, macho yangu huona siku zote maumivu na mapigo.
8
Onyeka, Yerusalemu, roho yangu isije kujitenga nawe, nisikugeuze kuwa nchi yenye mapori matupu yasiyokaa watu!
9
Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Masao yako, Isiraeli, yataokotezwa kama yake mzabibu; ukunjue tena mkono wako kama mchuma zabibu, akiyatazama matawi!
10
Nimwambie nani na kumshuhudia, wapate kusikia? Tazama! Hawakutahiriwa penye masikio, hawawezi kusikia. Neno lake Bwana likawa kicheko kwao, hawapendezwi nalo.
11
Nami nimejaa makali ya Bwana yenye moto, nimechoka kuyazuia. Basi, na yapige watoto wanaocheza njiani nao vijana, wakikusanyika pamoja, kwani wote, waume na wake, wazee na wakongwe, watashikwa nayo.
12
Nyumba zao zitaachiliwa wengine, hata mashamba na wanawake vilevile, kwani nitawakunjulia mkono wangu wao wakaao katika nchi hii; ndivyo, asemavyo Bwana.
13
Kwani wao wote, walivyo wadogo mpaka wakiwa wakubwa, hutamani mali tu; hata wafumbuaji na watambikaji wote pia hufanya yenye uwongo.
14
Madonda yao walio wazaliwa wa ukoo wangu huyaponya juujuu wakisema: Tengemaneni! Tengemaneni! lakini hakuna utengemano.
15
Watapatwa na soni, kwani hufanya yatapishayo; lakini hawaoni soni, wala hawajui kuiva nyuso. Kwa hiyo wataanguka pamoja na wenzao watakaoanguka siku hiyo, nitakapowapatiliza; ndipo, watakapojikwaa. Ndivyo, Bwana anavyosema.
16
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Simameni njiani, mwone! Ulizeni mapito ya kale, kama njia njema ni ipi? Hiyo ishikeni, mzipatie roho zenu kituo! Wakasema: Hatutaishika.
17
Nitawawekea walinzi, mwiangalie sauti ya baragumu! Wakasema: Hatutaiangalia.
18
Kwa hiyo sikieni, ninyi wamizimu! Ninyi mliokutanika, yatambueni yatakayokuwa kwao!
19
Nayo nchi, sikia! Na mnione, nikiwaletea mabaya watu wa ukoo huu, ndiyo yaliyozaliwa na mawazo yao, kwani maneno yangu hawakuyasikiliza, nayo Maonyo yangu wameyakataa.
20
Uvumba utokao Saba unanifaliaje? Nayo manukato yatokayo nchi ya mbali ni ya nini? Ng'ombe zenu za tambiko hazinipendezi, wala vipaji vyenu vya tambiko havinifurahishi.
21
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Nitazameni, jinsi ninavyoweka mawe ya kukwazia njiani kwao walio ukoo huu, nao watajikwaa wote pia, baba na watoto, wenyeji na wenzao wataangamia.
22
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Tazameni! Watu watakuja toka nchi ya kaskazini, taifa kubwa litainuka kwenye mapeo ya nchi.
23
Hushika pindi na mikuki, ni wakorofi pasipo huruma, makelele yao ni kama kuvuma kwa bahari, nao hupanda farasi; wamejivika kama watu waendao vitani, wapigane na wewe, binti Sioni.
24
Tulipokisikia kivumo chao, mikono yetu ikalegea, tukasongeka, uchungu ukatushika kama wa mzazi.
25
Msitoke kwenda shambani, wala njiani msiende! Kwani panga za adui ziko, zinawastusha po pote.
26
Mlio wazaliwa wa ukoo wangu, jivikeni magunia, mpate kugaagaa mavumbini! Ombolezeni kama waliofiwa na mwana wa pekee! Vilio na viwe vyenye uchungu sana! Kwani mara mwangamizi atatujia.
27
Nimekuweka kwao walio ukoo wangu, uwajaribu, kwani ni wagumu, uwatambue ukizijaribu njia zao.
28
Wao wote ndio wabishi wenyewe waendao wakisingizia, ni wagumu kama shaba na vyuma, wao wote ndio wapotezaji wabaya.
29
Mifuo ikifukutwa, mle motoni hutoka shaba tu. Imekuwa kazi bure kuyeyusha mara kwa mara, kwani mabaya yaliyomo hayakutengeka.
30
Sharti waitwe fedha zitupwazo, kwani Bwana amewatupa.
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 7 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52