bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 8
Jeremiah 8
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 9 →
1
Ndivyo, asemavyo Bwana: Siku zile wataifukua makaburini mwao mifupa ya wafalme wa Yuda na mifupa ya wakuu wao na mifupa ya watambikaji na mifupa ya wafumbuaji na mifupa yao waliokaa Yerusalemu.
2
Kisha wataitandaza penye jua na penye mwezi napo penye kikosi chote cha mbinguni, maana wamepapenda, wakapatunukia, wakapafuata, wakapatafuta, wakapaangukia; haitaokotwa, wala haitazikwa tena, itakuwa mbolea tu juu ya nchi.
3
Nayo masazo yote yatakayosazwa ya mlango huu mbaya yatapendezwa zaidi na kufa kuliko kuwapo mahali po pote, nilipowatupia hayo masazo; ndivyo, asemavyo Bwana Mwenye vikosi.
4
*Uwaambie: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Je? Wako waangukao wasioinuka tena? Au yuko ageukaye asiyerudi tena?
5
Mbona ukoo huu wa Yerusalemu umegeuka pasipo kurudi kale na kale? Wameyashika madanganyifu, wakakataa kurudi.
6
Nikaangalia na kusikiliza, hawasemi yaliyo sawa, wala hakuna mtu aujutiaye ubaya wake kwamba: Je? Nimefanya nini? Kila mmoja hugeuka kwa kujikimbilia kwao kama farasi akimbiaye vitani.
7
Naye korongo wa angani huzijua siku zake, hata hua na kinega na mbayuwayu huzishika siku zao za kuja, lakini walio ukoo wangu hawayajui yampasayo Bwana.
8
Mnasemaje: Sisi tu werevu wa kweli, nayo Maonyo yake Bwana tunayo? Ndio, lakini tazameni! Kalamu zao waandishi zenye uwongo zimeyageuza kuwa uwongo!
9
Walio werevu wa kweli wamepatwa na soni, wanazizimuka kwa kuumbuliwa; Neno lake Bwana wamelitupa, sasa wako na werevu gani tena ulio wa kweli?*
10
Kwa hiyo nitawapa wengine wake zao, nayo mashamba yao nitawapa wale watakaowatwaa, kwani wao wote, walivyo wadogo mpaka wakiwa wakubwa, hutamani mali tu, hata wafumbuaji na watambikaji wote pia hufanya yenye uwongo.
11
Madonda yao walio wazaliwa wa ukoo wangu huyaponya juujuu wakisema: Tengemaneni! Tengemaneni! Lakini hakuna utengemano.
12
Watapatwa na soni, kwani hufanya yatapishayo; lakini hawaoni soni, wala hawajui kuiva nyuso. Kwa hiyo wataanguka pamoja na wenzao watakaoanguka siku hiyo, nitakapowapatiliza; ndipo, watakapojikwaa; ndivyo, Bwana anavyosema.
13
Ndivyo, asemavyo Bwana: Ninapotaka kuchuma kwao, mizabibu, haina zabibu, wala mikuyu haina kuyu, nayo majani yao inakuwa inanyauka; kwa hiyo nitatoa watu, wawaondoe.
14
Mbona sisi tunajikalia? Na tukusanyike, tuingie katika miji yenye maboma, tukaangamie humo! Kwani Bwana Mungu wetu atatuangamiza na kutunywesha maji yenye sumu, kwa kuwa tumemkosea Bwana.
15
Mbona tunangojea utengemano? Lakini hakuna chema! Mbona tunangojea siku za kupona? Lakini tunayoyaona ni mastuko.
16
Upande wa Dani kunasikilika, farasi wao wanavyofoka, kwa uvumi wa makelele yao walio wenye nguvu nchi hii yote inatetemeka; watakuja, wataila nchi nayo yote yaliyomo, miji pamoja nao wakaaamo.
17
Angalieni! Nitatuma kwenu nyoka za pili wasiowezekana kwa uganga wo wote, wawaume ninyi; ndivyo, asemavyo Bwana.
18
Napata wapi utulivu wa roho katika masikitiko? Moyo wangu umeugua humu ndani.
19
Nikiangalia ninasikia sauti za vilio vyao walio wazaliwa wa ukoo wangu, zikitoka katika nchi ya mbali kwamba: Je? Bwana hayumo naye? Sioni wala mfalme wake hayumo naye? Kwa sababu gani wamenisikitisha na vinyago vyao na mambo mageni yasiyo maana?
20
Mavuno yamepita, kiangazi kimekwisha, lakini sisi hatukuokolewa.
21
Kwa mavunjiko yao walio wazaliwa wa ukoo wangu nami nimevunjika, nikaomboleza, ushangao ukanishika kwa nguvu.
22
Je? Haiko miti yenye dawa huko Gileadi? Wala hakuna mponya huko? Mbona wazaliwa wa ukoo wangu hawakupata kuponywa?
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 9 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52