bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 9
Jeremiah 9
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 10 →
1
Nataka sana, kichwa changu kingegeuka kuwa maji, nayo macho yangu yangegeuka kuwa kisima cha machozi, nipate kuwalilia mchana na usiku wazaliwa wa ukoo wangu waliouawa!
2
Nataka sana, ningepata nyikani fikio la wasafiri, ningewaacha wao walio ukoo wangu na kutoka kwao, kwani wao wote ndio wagoni, ni chama cha wadanganyi.
3
Huzikaza ndimi zao kuwa pindi za kupiga maneno ya uwongo; wamepata nguvu katika nchi, lakini si kwa welekevu, kwani wakitoka pabaya huingia pabaya pengine, lakini mimi hawanijui; ndivyo, asemavyo Bwana.
4
Jilindeni kila mtu kwa ajili ya mwenziwe! Hata ndugu na ndugu msiegemeane! Kwani kila ndugu humponza ndugu yake, hata kila rafiki hufuata masingizio.
5
Kila mmoja humwongopea mwenziwe, lakini neno la kweli hawalisemi, wakazifunza ndimi zao kusema uwongo, hupotoa, mpaka wachoke.
6
Unakaa kwenye madanganyifu katikati, nami kwa udanganyifu wamekataa kunijua; ndivyo, asemavyo Bwana.
7
Kwa hiyo Bwana Mwenye vikosi anasema hivi: Kweli wataniona, nikiwayeyusha na kuwajaribu. Kwani nifanye mengine gani nikiwatazama wazaliwa wa ukoo wangu?
8
Ndimi zao ni mishale ya kuchoma na kuua, husema madanganyifu: kwa vinywa vyao husema matengemano na wenzao, lakini mioyoni huviziana.
9
Mambo kama hayo nisiyapatilize kwao? watu walio hivyo Roho yangu isiwalipize? ndivyo, asemavyo Bwana.
10
Milima nitaililia na kuiombolezea, nazo mbuga za nyikani nitazitungia wimbo wa kilio, kwani ziko peke yao, hakuna mtu apitaye hapo, hapasikiliki tena sauti za ng'ombe, hata ndege wa angani pamoja na nyama wa porini wamekimbia kwenda zao.
11
Hata Yerusalemu nitaugeuza kuwa machungu ya mawe tu, panapokaa mbwa wa mwitu, nayo miji ya Yuda nitaigeuza kuwa peke yao, isikae watu.
12
Yuko nani aliye mwerevu wa kweli, ayatambue haya? Yuko nani, ambaye kinywa cha Bwana kilisema naye, ayatangaze, kama ni kwa sababu gani, nchi hii ikiangamia, iwe peke yake, pasipite mtu?
13
Bwana akasema: Kwa sababu wameyaacha Maonyo yangu, niliyowapa, wayaangalie, wakakataa kuisikia sauti yangu, hawakuifuata.
14
Ila wameufuata ushupavu wa mioyo yao, wakayafuata Mabaali, kama baba zao walivyowafundisha.
15
Kwa hiyo Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anasema hivi: Wataniona kweli, nikiwalisha majani machungu na kuwanywesha maji yenye sumu.
16
Nitawatawanya kwenye wamizimu, wasiowajua hawa wala baba zao, tena nitatuma panga nyuma yao, mpaka niwamalize.
17
Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Yatambueni! Waiteni wanawake waombolezaji, waje! Tumeni nako kwao wanawake walio werevu wa kweli, waje!
18
Waje upesi kutuombolezea, macho yetu yachuruzike machozi, nazo kope zetu zitiririke maji!
19
Sauti za maombolezo zinasikilika upande wa Sioni kwamba: Tumetekwa namna gani na kutwezwa kabisa? Hatuna budi kuiacha nchi yetu, kwani makao yetu wameyabwaga chini.
20
Sasa ninyi wanawake, lisikieni neno la Bwana, masikio yenu yalipokee neno la kinywa chake! Wafundisheni wana wenu wa kike kuomboleza, kila mwanamke mmoja amfundishe mwenziwe kulilia kufa kwamba:
21
Kifo kimepanda madirishani mwetu, kimeingia majumbani mwetu, kiwapokonye watoto barabarani mwa mji, nao wavulana viwanjani!
22
Sema: Ndivyo, asemavyo Bwana: Mizoga ya watu itaanguka shambani kuwa kama vinyesi au kama miganda inavyoanguka chini nyuma ya mvunaji, lakini hakuna mwenye kuiokota.
23
*Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Mwerevu wa kweli asijivunie werevu wake! Wala mwenye nguvu asijivunie nguvu zake! Wala mwenye mali asijivunie mali zake!
24
Ila mwenye kujivuna na ajivunie kuwa mtambuzi wa kunijua mimi, ya kuwa mimi Bwana ndiye afanyaye upole na maamuzi yaongokayo katika nchi hii! Kwani hayo ndiyo yanipendezayo; ndivyo, asemavyo Bwana.*
25
Ndivyo, asemavyo Bwana: Tazameni! Siku zinakuja, nitakapowapatiliza wote waliotahiriwa kwa kuwa tena kama watu wasiotahiriwa,
26
akina Wamisri na Wayuda na Waedomu nao wana wa Amoni na Wamoabu nao wote wakatao nywele za panjani wakaao nyikani; kwani wamizimu wote ni watu wasiotahiriwa miilini, lakini wote walio wa mlango wa Isiraeli ni wenye mioyo isiyotahiriwa.
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 10 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52