bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Job 12
Job 12
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 13 →
1
Kweli, ninyi tu ndio walio watu,
2
werevu wa kweli utakufa nao, mtakapokufa ninyi.
3
Mimi nami ninazo akili kama ninyi, sikupungukiwa na akili, ninyi mnishinde, yuko nani asiyeyajua mambo kama hayo?
4
Mtu wa kuchekwa na wenziwe ni mimi, mimi niliyemwita Mungu, akaniitikia; kweli mwongofu asiyekosa kabisa ni mtu wa kuchekwa.
5
Atesekaye hubezwa moyoni mwake naye akaaye na kutulia, yuko tayari kuwasukuma wajikwaao miguu.
6
Mahema yao wapokonyi hutengemana, nao wamkasirishao Mungu hukaa na kutulia, ndio, Mungu anaowatia mengi mikononi mwao.
7
Haya! Uliza nyama, wakufundishe, nao ndege wa angani, wakueleze!
8
Au sema na nchi yenyewe, nayo itakufundisha! Hata samaki wa baharini watakusimulia mambo.
9
Yuko nani asiyeyajua haya yote, ya kuwa mkono wa Mungu ndio ulioyatengeneza haya?
10
Mkononi mwake zimo roho zao hao nyama wote, zimo nazo pumzi zao wote wenye miili ya kimtu.
11
Sikio silo linaloyajaribu yanayosemwa, kama ufizi unavyovionja vyakula vyake?
12
Werevu wa kweli uko kwao walio wazee, siku zikiwa nyingi, mtu hupata utambuzi.
13
Werevu wa kweli na uwezo uko kwake Mungu, tena wongozi na utambuzi.
14
Tazama: Akibomoa, hapajengwi tena; akimfunga mtu, hafunguliwi tena.
15
Tazama: Akiyazuia maji, hukauka; tena akiyaachia huifudikiza nchi.
16
Yeye ni mwenye nguvu na uwezo wa kufanya mambo, wake yeye ni apoteaye naye apotezaye.
17
Wenye kukata mashauri huwapeleka kuwa mateka, nao waamuzi huwapumbaza.
18
Mafungo ya wafalme huyafungua, tena huwafunga wenyewe kwa kamba viunoni pao.
19
Nao watambikaji huwapeleka kuwa mateka, nao wenye nguvu huwaangamiza.
20
Waliotegemewa kuwa mafundi wa kusema huwasemesha kibubu, nazo akili zao wazee huzipumbazisha.
21
Huwamwagia mabezo walio wakuu, nao wenye nguvu huwalegeza mikanda.
22
Huvumbua yaliyofichwa ndani ya nchi na kuyatoa gizani, nacho kivuli kiuacho hukitokeza mwangani.
23
Hukweza mataifa, kisha huyaangamiza, hueneza mataifa mahali, kisha huyaacha, yatekwe.
24
Wakuu wa makabila ya huku nchini huwatia kichaa, kisha huwapoteza nyikani pasipo na njia,
25
wapapasepapase gizani pasipo na mwanga, huwaacha, wapepesuke kama mlevi.
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 13 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42