bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Job 13
Job 13
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 14 →
1
Tazameni! Jicho langu limeyaona hayo yote pia, sikio langu limeyasikia na kuyatambua.
2
Mnayoyajua ninyi, nimeyajua ami, sikupungukiwa na akili, ninyi mnishinde.
3
Kweli mimi na niseme naye Mwenyezi, napenda sana kujikania kwake Mungu.
4
Kweli ninyi hutunga maneno yaliyo ya uwongo, nyote m waganga wasiofaa.
5
Kama mngenyamaza kimya kabisa, mngejitokeza kuwa wenye werevu ulio wa kweli.
6
Sikieni, jinsi ninavyojikania! Yategeni masikio, midomo yangu ikiyasema mashindano yangu!
7
Je? Mtamtetea Mungu kwa kusema yaliyo mapotovu? Au mtamtetea kwa kusema yaliyo madanganyifu?
8
Je? Mtampendelea Mungu kwa kumgombea magomvi yake?
9
Je? Akiwachunguza ninyi, ingekuwa vema? Au mtaweza kumdanganyadanganya, kama watu wanavyodanganyana?
10
Atawakemea kwa nguvu, mkipendelea watu na kufichaficha.
11
Je? Utukufu wake hautawatia woga? Kitisho chake nacho hakitawaangukia ninyi?
12
Makumbusho yenu ni mafumbo ya kijivu, nazo ngome zenu ni ngome za udongo.
13
Ninyamazieni mimi, nipate kusema nami! Yatakayonijia na yanijie!
14
Ingefaaje, nikiuma nyama za mwili wangu kwa meno yangu? Au nikiiweka roho yangu mikononi mwangu?
15
Mtaona, akiniua; hakuna kingine, nikingojeacho; ninataka tu kumwelezea njia zangu usoni pake.
16
Hili tu litasaidia kuniokoa, kwani mwovu hatokei usoni pake.
17
Lisikilizeni vema neno langu, nayo maelezo yangu na yaingie masikioni mwenu!
18
Tazameni! Nimelitengeneza shauri langu, najua, ya kuwa nitajitokeza kuwa asiyekosa.
19
Yuko nani atakayebishana na mimi hapa? Kama yuko, ningenyamaza tu, nipate kuzimia.
20
Haya mawili ninayataka, unifanyie, nisije kujificha usoni pako:
21
uondoe mkono wako, usinilemee! Tena kizuie kitisho chako, kisinistushe!
22
Kisha hapo, utakaponiita, mimi nitakuitikia! Au mimi niseme, nawe unijibu!
23
Maovu yangu na makosa yangu, niliyoyafanya, ni mangapi? Nijulishe mapotovu yangu nayo makosa yangu!
24
Mbona unauficha uso wako, ukaniwazia kuwa miongoni mwao wapingani wako?
25
Utatetemesha jani lipeperushwalo? Au utakimbiza kibua kilicho kikavu?
26
Kwani unaniandikia machungu kama haya, tena unanilipisha manza, nilizozikora nilipokuwa nikingali mwana.
27
Nayo miguu yangu unaitia mikatale, ukapaangalia pote, nipitiapo, napo, nyayo za miguu yangu zinapokanyaga, unachora alama zako.
28
Nami ninanyauka kama mwenye kibovu, nafanana na nguo iliyoliwa na nondo.
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 14 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42