bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Job 14
Job 14
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 15 →
1
*Mtu aliyezaliwa na mwanamke huwapo siku chache, nayo anayoyashiba ni mahangaiko tu.
2
Huchanua kama ua, kisha hupukutika, hupita upesi kama kivuli, hakai.
3
Ingawa awe hivyo, unayafumbua macho, kusudi yamlinde; lakini mimi unanipeleka shaurini, tusemeane huko.
4
Miongoni mwao waliotoka kwa mwenye uchafu yuko atakataye? Hata mmoja tu hayuko.
5
Mtu amekwisha kukatiwa siku zake, miezi yake imekwisha kuhesabiwa na wewe mwenyewe, umeiweka mipaka yake, asiipite.*
6
Ikiwa hivyo, acha kumtazama, apate kupumzika, aifurahie hiyo siku yake kama mkibarua!
7
Kwani kiko kingojeo kinachoupasa huo mti nao: kama unakatwa, huchipuka tena, nayo hayo machipukizi yake hayakomi.
8
Mizizi yake ikioza nchini ndani, nalo shina lake likifa mchangani,
9
kwa unyevu wa maji tu utachipuka tena, upate matawi sawasawa kama mche mpya.
10
Lakini mtu akifa hutoweka, mwana wa Adamu akiisha kuzimia huenda wapi?
11
Maji ya bahari hupwa, nayo ya mtoni hupotea kabisa, pawe pakavu.
12
Vivyo hivyo naye mtu akija kulala hainuki tena; mpaka mbingu zitakapotoweka, hawaamki, wala hawataamshwa usingizini mwao.
13
Laiti ungenificha kuzimuni, ukanilindia huko, mpaka yatulie makiali yako! Muda ulionikatia utakapokwisha pita, ungenikumbuka hapo!
14
Mtu atarudi uzimani tena akiisha kufa? Kama ndivyo, ningengoja siku zangu zote za kushindana na mateso, mpaka nitakapopokelewa na mwenzangu mwingine.
15
Hapo ningekuitikia, utakaponiita kwa kukitunukia kiumbe cha mikono yako.
16
Sasa ukizihesabu nyayo zangu po pote, zilipokanyaga, makosa yangu nayo huyaangalii?
17
Hapo maovu yangu yangefungiwa mfukoni na kutiwa muhuri, nazo manza zangu, nilizozikora, ungezifuta.
18
Lakini sivyo; mlima ukianguka hutoweka, nao mwamba huondoka mahali pake, ulipokuwapo.
19
Maji husaga mawe, yawe madogo, nayo mafuriko ya maji huuchukua mchanga wa nchi, hivyo nacho kingojeo cha mtu unakiangamiza.
20
Unamshinda siku zote pia, ajiendee, unaugeuza uso wake ukimtuma kujiendea.
21
Wanawe kama wanapata macheo, havijui; au kama wananyenyekezwa, hayatambui mambo yao.
22
Huyasikia tu maumivu ya mwili wake yeye, nayo roho yake husikitika kwa ajili yake yeye. Elifazi wa Temani akajibu akisema:
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 15 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42