bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Job 19
Job 19
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 20 →
1
Roho yangu mtaisikitisha mpaka lini
2
kwa kujisemea maneno tu ya kuniumiza?
3
Sasa ni mara kumi, mkinitukana; lakini kwa kunihangaisha hivyo hamwoni soni?
4
Itakapotokea kuwa kweli, ya kama nimekosa, mimi ndiye, litakayemkalia hilo kosa langu.
5
Kama mnajikuza kweli na kunibeua, kama mimi ni mtu apaswaye na kutwezwa, haya! Niumbueni!
6
Jueni, ya kuwa ndiye Mungu aliyenipotoa kwa kunitegea pande zote tanzi lake.
7
Tazameni! Nikiulilia ukorofi sijibiwi, wala hakuna aniamuliaye, nikilalamika.
8
Njia yangu ameifunga kwa kitalu, nisipitie hapo, napo penye mikondo yangu amepapatia giza.
9
Yaliyokuwa utukufu wangu amenivua, nacho kilemba amekiondoa kichwani pangu.
10
Kwa sababu amenibomolea pande zote, sina budi kujiendea, nacho kingojeo changu ameking'oa, kama ni mti tu.
11
Akanitolea makali yake, yaniwakie moto, akaniwazia kuwa kama mmoja wao wapingani wake.
12
Vikosi vyake vikaja, vikutanie pamoja, vikajitengenezea njia ya kufika kwangu, vikayapiga makambi yao, yanizunguke hemani mwangu.
13
Ndugu zangu akawaweka mbali, wasije kwangu, nao wenzangu wa kujuana nao wakanigeukia kuwa kama wageni.
14
Walio wa ukoo wangu nao wakapotea, nao rafiki zangu wema wakanisahau.
15
Waliokaa pamoja na watumishi wa kike nyumbani mwangu wao ndio wanaoniwazia kuwa mgeni, machoni pao nikageuka kuwa mtu asiye wa kwao.
16
Nikimwita mtumishi wangu, haitikii, sharti nimwambie maneno mengi ya kumbembeleza.
17
Pumzi zangu zinamchukia mke wangu, mnuko wangu mbaya unawachukia, niliowazaa mwenyewe.
18
Nao walio vijana bado hunibezabeza, nikiinuka, husema maneno ya kunifyoza.
19
Wote waliokuwa wenzangu wa njama wanachukizwa na mimi, nao waliogeuka kuwa wapingani wangu ndio, niliowapenda.
20
Ngozi na nyama za mwili wangu zinagandamana na mifupa, kilichopona kwangu ni ufizi tu.
21
Nihurumieni, nihurumieni, ninyi wenzangu! Kwani mkono wa Mungu umenipiga.
22
Mbona mnanikimbiza kama Mungu, msishibe kuzinyafuanyafua nyama za mwili wangu?
23
Laiti maneno yangu yangeandikwa kwa kupigwa chapa kitabuni!
24
Laiti yangechorwa namo mwambani kwa kalamu ya chuma, kisha kutiwe risasi, yawepo kale na kale!
25
Mimi ninayoyajua ndiyo haya: Mkombozi wangu yupo, ni mwenye uzima, naye huko mwisho ndiye atakayeinuka uvumbini.
26
Mwili wangu wenye ngozi utakapokwisha kuharibika, huu mwili wangu wenye nyama utakapokuwa haupo, hapo ndipo, nitakapopata kumwona Mungu;
27
mimi mwenyewe nitamwona kuwa wangu, macho yangu ndiyo yatakayomwona, siyo ya mgeni tu; mafigo yangu yanazimia ndani yangu kwa kuyatunukia hayo.
28
Mkisema: Haya! Na tumkimbize! kwani mizizi ya mambo haya imeonekana kwangu:
29
uogopeni upanga rohoni mwenu! Kwani kutoa makali yenye moto hutupatia hukumu za upanga; zitakapotokea, ndipo, mtakapojua: mapatilizo yako! Sofari wa Nama akajibu akisema:
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 20 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42