bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Job 20
Job 20
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 21 →
1
Kwa sababu hii mawazo yangu yananishurutisha, nikujibu,
2
maana ninachafuka sana moyoni mwangu.
3
Ninasikia maneno ya kunikanya, nayo ya kunitukana, lakini kwa utambuzi wangu ninajibiwa mengine rohoni mwangu.
4
Je? Hayo huyajui tangu kale, tangu hapo, watu walipokaa katika nchi?
5
Ya kuwa shangwe zao wasiomcha Mungu hukoma upesi? Ya kuwa furaha ya mwovu hukaa kitambo kidogo tu?
6
Ijapo ayakuze majivuno yake, yafike mbinguni, kichwa chake kiyaguse nayo mawingu,
7
hupotelea kale na kale kama mavi yake, waliomwona waulize: yuko wapi?
8
Hupita kwa kuruka kama ndoto, watu wasimwone tena, hufukuzwa kama ono baya la usiku.
9
Jicho lililomchungulia halitomwona tena, wala mahali pake, alipokuwa, hapatamtazama tena.
10
Wanawe watabembeleza walio wanyonge, mikono yao itazirudisha mali, alizozinyang'anya.
11
Ijapo, mifupa yake izidi kuwa nazo nguvu za ujana, lakini haina budi kulala pamoja naye uvumbini.
12
Kama anauona ubaya kuwa mtamu kinywani mwake, aufiche, upate kukaa chini ya ulimi wake,
13
autunze vizuri, asitake kuuachilia, ujiendee, ila auzuie, usiondoke penye ufizi wake:
14
kisha hicho chakula chake kitageuzwa tumboni mwake kuwa uchungu wa pili mle ndani yake;
15
hizo mali nyingi, alizozimeza, hana budi kuzitapika, Mungu akizitoa kwa nguvu tumboni mwake.
16
Kwa hivyo, alivyonyonya sumu iliyo ya pili, mwisho ulimi wa moma utamwua,
17
asijifurahishe tena kwa kuvitazama vile vijito wala ile mito inayokwenda na kujaa asali na mafuta.
18
Aliyoyasumbukia hana budi kuyarudisha, hawezi kuyameza, ijapo mapato yake yawe mengi mno, hayafurahii.
19
Kwani alipokwisha kuwaponda wanyonge, aliwaacha papo hapo, akanyang'anya nyumba, asizozijenga.
20
Lakini hakujua kutulia ndani yake yeye; kwa hiyo hatapona pamoja nayo, aliyoyatunukia.
21
Kwa ulafi wake hakikuwako kitu, asichokichukua; kwa sababu hii hivyo vyema vyake havikai kabisa.
22
Hapo atakapofurikiwa, ndipo, atakaposongeka, mikono yao walioteswa naye ikimjia yote.
23
Ndipo, Mungu atakapolijaza tumbo lake akituma kwake makali yake yawakayo moto, ayanyeshe juu yake yampatie chakula cha kushiba.
24
Itakapokuwa, ayakimbie mata ya chuma, uta wa shaba utampiga, achomwe;
25
akitaka kuutoa mshale, utakuwa umetokea mgongoni pake, chembe yake imetukayo itakuwa imeichoma nayo nyongo; basi, mastusho yatamjia vivyo hivyo.
26
Mambo yote ya giza yako tayari kwake kuviangamiza vilimbiko, nao moto uwakao pasipo kupulizwa utamla mwenyewe, nayo yaliyosalia hemani mwake utayamaliza.
27
Mbingu zitazifunua manza, alizozikora, nayo nchi itainuka kumshinda shaurini.
28
Nyumba yake iliyompatia yatatekwa, yatakuwa kama maji yakaukayo, siku ya ukali wake Mungu itakapotimia.
29
Hilo ndilo fungu, mtu asiyemcha Mungu atakalolipata kwake Mungu, ndio urithi, atakaogawiwa naye Mungu. Iyobu akajibu akisema:
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 21 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42