bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Job 21
Job 21
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 22 →
1
Sikieni na kulisikiliza neno langu!
2
Hili litakuwa la kuituliza mioyo yenu.
3
Niacheni, nipate kusema mimi nami! Nitakapokwisha kuyasema yangu, na msimange tena.
4
Je? Yuko mtu, ninayemsuta? Mbona sishindwi na kuvumilia?
5
Nigeukieni mimi, mpate kustuka na kuiweka mikono vinywani mwenu!
6
Kweli nami nikiyakumbuka nashikwa na woga, mwili wangu nao unakufa ganzi.
7
Mbona wasiomcha Mungu huwapo? Mbona huwa wazee, nguvu zao zikiendelea kuongezeka?
8
Vizazi vyao huviona kwao kwa macho yao kuwa vyenye nguvu, nao wajukuu wao wako machoni pao.
9
Nyumba zao hukaa salama pasipo kustushwa, nayo fimbo ya Mungu haiwapigi.
10
Ng'ombe wao waume huzaza vema pasipo kukosa, ng'ombe wao wake huzaa vizuri pasipo kuharibu mimba.
11
Huwatembeza watoto wao walio wengi kama kundi la kondoo, nao vijana wao huchezacheza na kupaza sauti
12
wakiimbia patu na mazeze na kuifurahia milio ya mazomari.
13
Siku zao huzitumia za kula mema, kisha hushuka kuzimuni kwa mara moja.
14
Nao humwambia Mungu: Ondoka kwetu! hatupendezwi kuzijua njia zako.
15
Mwenyezi ni nani, tumtumikie? Inatufaliaje kumtokea na kumwomba?
16
Lakini tazameni: mema yao hawayashiki mikononi mwao, kwa hiyo mashauri yao wasiomcha Mungu na yanikalie mbali!
17
Taa zao wasiomcha Mungu zikizima, ni mara ngapi? Si kila mara, unapowajia mwangamizo wao? Ni mara ngapi, Mungu akiwapatia matanzi kwa kuwakasirikia,
18
wawe kama bua kavu penye upepo au kama makapi, yakipokonywa na upepo wa chamchela?
19
Mwasema: Mungu huwawekea watoto wao maovu yao; lakini angewalipisha wenyewe, wapate kumjua,
20
macho yao wenyewe yangeuona mwangamizo wao, wakinyweshwa makali yake Mwenyezi yaliyo yenye moto.
21
Kwani mlango wao unawezaje kuwapendeza huko nyuma yao, miezi yao ikiisha kukatwa kwa kuitimiza hesabu yao?
22
Je? Wanataka kumfundisha Mungu, apate kuwajua? Naye ndiye awahukumuye nao walioko huko juu.
23
Huwa hivi: mmoja anakufa mwenye nguvu zake zote, naye alikuwa anatengemana na kutulia kabisa,
24
vyombo vyake vya kukamulia vikijaa maziwa, kiini cha mifupa yake nacho kikiwa chenye mafuta.
25
Mwingine anakufa mwenye uchungu rohoni mwake, kwa kuwa hakuna chema cho chote, alichokila.
26
Kisha hulala pamoja humo uvumbini, vidudu vikiwafunika wote wawili.
27
Tazameni! Ninayajua mawazo yenu nayo mashauri yenu ya kunikorofisha.
28
Mwasema: Nyumba ya mkuu aliyetesa watu iko wapi? Mahema, wasiomcha Mungu waliomokaa, yako wapi nayo?
29
Je? Wapitao njiani hamkuwauliza hayo? Hamzitambui habari zao za mambo, waliyoyaona wao?
30
Kwamba: Siku ya msiba mbaya hupona, siku, makali yanapotokea, huepuka.
31
Yuko nani anayeziumbua njia zake usoni pake? Tena yuko nani anayemlipisha aliyoyafanya yeye?
32
Naye husindikizwa mpaka mazikoni, tena kaburini kwake wanangoja zamu.
33
Udongo wa bondeni anauona kuwa mtamu, watu wote wanamfuata nyuma yake, nao waliomtangulia hawahesabiki.
34
Nanyi mnaniambiaje matulizo ya moyo yaliyo ya bure? Kwani yanayosalia ya majibu yenu, ni ukatavu tu. Elifazi wa Temani akajibu akisema:
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 22 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42