bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Job 24
Job 24
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 25 →
1
Mbona hazikuwekwa na Mwenyezi siku zake za mapatilizo? Mbona hawazioni hizo siku zake wao wamjuao?
2
Wasogezao mipaka wako huku, nao wanyang'anyao makundi ya kondoo, wayachunge kuwa yao.
3
Punda wao waliofiwa na wazazi huwachukua, nao ng'ombe wa wajane huwakamata kuwa rehani.
4
Huwakumba maskini, waondoke njiani, wanyonge wa huku chini wote pia hawana budi kujificha.
5
Watazameni, kama hawafanani nao vihongwe vya nyikani: hutoka na mapema kufanya kazi zao za kujipatia chakula, wanakojipatia chakula cha watoto, ndiko porini.
6
Mashambani kwa watu huchuma ya kujilisha, nayo mizabibu yao wasiomcha Mungu huiokoteza.
7
Hulala usiku wenye uchi pasipo nguo za kujifunika, hawana mablanketi ya kujizuilia baridi ya kipupwe.
8
Hulowa kwa kunyewa na mvua za milimani, kwa kukosa kimbilio hujibana mwambani.
9
Tena wako wapokonyao kifuani kwa mama waliofiwa na baba, nao wanyonge huwavua mavazi kuwa rehani;
10
kisha huwaacha, wajiendee wenye uchi pasipo nguo yo yote; nao wenye njaa huchukuzwa viganda vya ngano.
11
Uani pa mabwana zao hutengeneza mafuta, ijapo wenyewe wawe wenye kiu, huwakamulia wao zabibu.
12
Wenye kufa wakipiga kite, husikilika toka mjini, nazo roho zao waliouawa kwa nguvu hulilia malipizo, lakini wakipumbazwa vibaya hivyo, Mungu haviangalii.
13
Wenye kuchukizwa na mwanga ndio wenzao wale, hukataa kuzitambua njia zake hivyo, zilivyo, penye mikondo yake hawakai.
14
Mwuaji huinuka, kukipambazuka, aje kumwua mnyonge naye mkiwa, mambo ya usiku hufanana nayo yake mwizi.
15
Macho ya mzinzi hungoja kuchwa kwa kwamba: Pasipatikane jicho litakaloniona; kwa hiyo huuficha uso wake.
16
Penye giza hujipenyeza nyumbani mwa watu, kwa kukataa kuona mwanga hujifungia mchana.
17
Mapema yao hao wote pamoja ndio giza kuu, kwani huvijua mastusho yake hilo giza kuu.
18
Yeye kwa kuwa kama aendaye juu ya maji laiti angepita upesi, fungu lake la huku chini liapizwe, njia ya kwenda mizabibuni asiishike tena!
19
Kama kiangazi kinavyotowesha maji ya theluji kwa ukali wa jua, vivyo hivyo kuzimu na kuwatoweshe wakosaji walio hivyo.
20
Nalo tumbo la mama na limsahau, wadudu wakiufurahia utamu wa mwili wake; kwa kuwa mpotovu na avunjwe kama mti, asikumbukwe tena.
21
Kwa maana aliwanyang'anya vyao wanawake wasiozaa, nao wajane hakuwafanyizia chema cho chote.
22
Kwa uwezo wake Mungu huwakalisha sana walio wenye nguvu, hata aliyekwisha kukata tamaa ainuke tena na kupata uzima.
23
Humpa kukaa na kutulia kwa kupata egemeo, nayo macho yake huzielekea njia zao.
24
Wakiisha kujipatia utukufu mara hawako tena, hutoweka kwa kupokonywa kama wote wengine; nao hukatwa kama masuke yaliyoko juu mabuani.
25
Au sivyo vilivyo? Yuko nani awezaye kuniumbua kuwa mwongo na kuyatokeza maneno yangu kuwa ya bure? Bildadi wa Sua akajibu akisema:
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 25 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42