bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Job 27
Job 27
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 26
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 28 →
1
Hivyo, Mungu alivyo Mwenye uzima, ijapo akatae kuniamulia,
2
hivyo, Mwenyezi alivyoitia roho yangu machungu haya,
3
siku zote, nitakapokuwa ninakokota roho bado, pumzi ya Mungu itakapokuwa ingalimo puani mwangu:
4
midomo yangu haitasema neno lipotokalo, wala ulimi wangu hautaongopa.
5
Ninyi sitawaitikia kale na kale mpaka nitakapozimia, sitakoma kuvieleza kwamba: Sikukosa.
6
Neno hili ninalishika sana, sitaliacha kwamba: Mimi ni mwongofu, moyo wangu haunisutii moja tu miongoni mwao siku zangu.
7
Mchukivu wangu na yampate yanayompata asiyemcha Mungu, naye aniinukiaye na yampate yaleyale yanayompata mpotovu.
8
Kwani mwovu akijipatia mapato kwa kukorofisha watu, Mungu atakapoitaka roho yake kwake, yuko na kingojeo gani?
9
Mungu atavisikia vilio vyake, masongano yatakapompata?
10
Au atamfurahia Mwenyezi, amlilie Mungu kila, anapotaka?
11
Nitawafundisha ninyi matendo yake mkono wa Mungu, Mwenyezi anayoyafanya, sitawaficha!
12
Ninyi nyote yatazameni mliyoyaona! mbona mwajisemea tena maneno yaliyo bure kabisa?
13
Hili ni fungu lake asiyemcha Mungu lililoko kwake Mungu, tena ni urithi, watakaoupata kwake Mwenyezi, wao wakorofi.
14
Wanawe watakapokua watauawa na upanga, nao wajukuu wake hawatashiba vyakula.
15
Watakaosalia kwake watazikwa kwa kuuawa na kipindupindu, nao wajane wao hawatawaombolezea.
16
Ijapo, alimbike fedha kuwa nyingi kama mavumbi, ijapo, ajiwekee mavazi kuwa mengi kama mchanga,
17
ijapo, ayaweke hivyo, atakayeyavaa ni mwongofu, nazo fedha watajigawanyia wao watakatao.
18
Akijenga nyumba yake, huwa kama buibui, au kama dungu, wanalomjengea mlinzi.
19
Anakwenda kulala mwenye mali, lakini ni mara ya mwisho, akifumbua macho, hakuna mali tena.
20
Mastusho yanamfikia kama maji mengi, upepo wa chamchela unampokonya usiku.
21
Upepo utokao maawioni kwa jua unamchukua, ajiendee, ukimwondoa kwa nguvu hapo pake, alipokuwa.
22
Unampiga mishale yake pasipo kumhurumia, hata atake hili mojo tu: kukimbia, atoke mkononi mwake.
23
Watu wanampigia makofi na kumzomea, akitoka hapo pake, alipokuwa.
← Chapter 26
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 28 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42