bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Job 29
Job 29
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 28
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 30 →
1
Laiti ningekuwa, kama nilivyokuwa katika miezi iliyopita,
2
Mungu alipoziangalia siku zangu!
3
Hapo taa yake ilimulika juu ya kichwa changu, kwa mwanga wake nikaenda hata gizani.
4
Siku zile nilikuwa mwenye nguvu za kiume, Mungu naye akakaa hemani mwangu kuwa mwenzangu wa mashauri.
5
Hapo Mwenyezi alikuwa pamoja na mimi, nao watoto wangu wakanizunguka.
6
Hapo miguu yangu ilioshwa kwa maziwa, nao mwamba uliochuruzika vijito vya mafuta ulikuwa kwangu.
7
Nilipotokea langoni kwenye mji, nikiweke kiti changu uwanjani,
8
vijana waliponiona wakaondoka kwenda pengine, nao wazee wakainuka, wasimame;
9
Wakuu wakayakomesha maneno yao na kuviweka viganja vinywani mwao.
10
Sauti za mabwana wakubwa nazo zikanyamaza, ndimi zao zikagandamana na fizi zao.
11
Sikio la mtu liliponisikia, akanishangilia, jicho la mtu liliponiona, akanishuhudia.
12
Kwani nilimponya mnyonge, aliponililia, hata waliofiwa na wazazi, walipokosa msaidiaji.
13
Mbaraka yake aliyeufikia mwangamizo ikanijia, nayo mioyo ya wajane nikaichangamsha.
14
Nilivaa wongofu, uniwie nguo, nayo maamuzi yangu yakawa kama kanzu na kilemba.
15
Kipofu nilikuwa macho yake, kiwete nilikuwa miguu yake.
16
Maskini mimi nilikuwa baba yao, nalo shauri la mtu, nisiyemjua, nikalichunguza vema.
17
Lakini mpotovu nilimvunja meno, namo mlemle katika meno yake nikayapokonya aliyoyanyang'anya.
18
Kwa hiyo nilisema: Katika kiota changu ndimo, nitakamozimia, siku zangu zitakapokuwa nyingi kama za mtende.
19
Mizizi yangu itatandama juu penye maji, nao umande utayanyea matawi yangu usiku kucha.
20
Utukufu, nilio nao, utakuwa mpya kila siku, nao upindi wangu utajipatia nguvu mpya mkononi mwangu.
21
Mimi watu walinisikiliza na kungoja, nimalize; nilipowapa shauri langu, wakaninyamazia.
22
Hakuwako mwingine aliyesema, nilipokwisha kusema, maneno yangu yakawa kama matone yaliyowadondokea.
23
Kama wanavyongoja mvua, ndivyo, walivyoningoja, vinywa vyao vikaasama kama vyao wanaotwetea mvua ya vuli.
24
Walipotaka kukata tamaa, nikawachekea, hawakuweza kuuinamisha chini uso wangu, ulipoangaza.
25
Nilipojielekeza kwenda kwao nilikaa nao kama kichwa chao, au kama mfalme katika vikosi vyake kwa kuwa kama mtu anayewatuliza mioyo waliosikitika.
← Chapter 28
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 30 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42