bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Job 30
Job 30
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 29
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 31 →
1
Sasa wananicheka walio wenye siku chache kuliko mimi, ambao baba zao nilikataa kuwaweka mahali, mbwa wa makundi yangu ya kondoo walipokuwa nao.
2
Nazo nguvu za mikono yao zingenifalia nini? Kwani uwezo wao wenye nguvu ulikuwa umeangamia.
3
Kwa kuwa ukosefu na njaa zilikuwa ziliwagofua, huguguna nayo mazao ya nyika iliyo kama jangwa jeusi, iliyo tupu kabisa pasipo cho chote cha kulisha watu.
4
Kwa hiyo huchuma vijanijani vyenye chumvi panapo na vichakachaka, nayo mizizi ya mifagio ni chakula chao.
5
Hufukuzwa penye watu wengine, wakiwazomea kama wezi.
6
Hawana budi kukaa katika makorongo yaogopeshayo, hata mashimoni ndani ya nchi, hata miambani.
7
Hulia kwa njaa vichakani wakilala chini ya upupu.
8
Ndio wenye upumbavu wenyewe wasiojua hata majina yao, nako kwao walifukuzwa na kupigwa.
9
Sasa nimegeuka kuwa mtu wao hao wa kumzomea, nikapata kuwa kwao kama fumbo.
10
Kwa kutapishwa na mimi huwa mbali, wasinifikie karibu, lakini hawajikatazi kunitemea mate usoni pangu.
11
Vilivyowazuia wakavifungua, wanitese, usoni pangu wakavitupa mbali hivyo vifungo vyao.
12
Hawa watu waovu hujisimamisha kuumeni kwangu, waisukume miguu yangu, iondoke kwao, nazo njia zao zilizowaangamiza hunitwika mimi.
13
Njia yangu wakaichimbua, isipitike, wao wakosao msaidiaji husaidia kunitumbukiza mwangamizoni.
14
Kama ni kutokea katika ufa mpana, hunijia mimi, makelele yao huzidi sana kwa kusukumana.
15
Mastusho kama hayo yakanigeukia, kama ni kwa nguvu za upepo yakautangua ukuu wangu upesi, nayo yawezayo kuniokoa yakatoweka kama wingu.
16
Kwa hiyo roho yangu imeyeyuka sasa ndani yangu, siku za kuteseka zikanipata.
17
Usiku unaichoma mifupa yangu huko ndani, mpaka ioze, nayo maumivu yangu yanayoniguguna hayapumziki.
18
Hizo nguvu nyingi zikaligeuza vazi langu, zikanikaza kama ukosi wa kanzu yangu.
19
Zikanibwaga matopeni, nikafanana nayo mavumbini na majivu.
20
Nikikulilia, wewe, hunijibu; hata nikisimama, unanitazama tu.
21
Umegeuka kuwa mpingani wangu asiyenihurumia, kwa huo uwezo wa mkono wako ukanifukuza.
22
Ukaniinua na kuniweka juu ya upepo, unipeleke, ukaniyeyusha kwa hizo nguvu za chamchela.
23
Nakujua, utakakonipeleka, ndiko kufani, uniingize nyumbani mwenye mkutano wao wote waliokuwa uzimani.
24
Je? Mtu akitumbukia shimoni hanyoshi mkono? Au mtu akizama hapigi yowe kwa sababu hiyo?
25
Aliyepatwa na siku ngumu sikulia naye? Roho yangu haikumsikitikia naye mkiwa?
26
Nilipotazamia mema, mabaya yakaja; nilipongojea mwanga, giza ikaja.
27
Matumbo yakachafuka, yakakataa kunyamaza, siku za mateso ziliponifikia mimi nami.
28
Nikajiendea na msiba wangu pasipo kuona jua, nikaondoka penye mkutano, nipate kulia.
29
Nimegeuka kuwa ndugu yao mbwa wa mwitu, na mwenzao mumbi wapigao kite.
30
Ngozi yangu inachubuka kwa kuwa nyeusi, itoke mwilini mwangu, nayo mifupa yangu imeungua kwa joto la mwili.
31
Hivyo zeze langu limegeuka kuwa la kuombolezea, nalo zomari langu hupiga sauti za vilio tu.
← Chapter 29
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 31 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42