bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Job 33
Job 33
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 32
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 34 →
1
Kwa hiyo Iyobu, yasikilize nitakayoyasema! Maneno yangu yote yategee masikio yako!
2
Tazama! Nitakifumbua kinywa changu, ulimi wangu useme kinywani mwangu.
3
Maneno yangu yananyoka kama moyo wangu; midomo yangu itayasema ninayoyajua, yaliyo ya kweli.
4
Roho ya Mungu aliyeniumba na pumzi ya Mwenyezi zinanipa kuwapo.
5
Kama utaweza na unijibu! Jiweke tayari kusimama usoni pangu!
6
Tazama! Mimi na wewe kwake Mungu tu sawa, mimi nami nilifinyangwa kwa udongo.
7
Tazama! Sikutishi, usinistukie, nayo nitakayokutwika yasikulemeze.
8
Kweli ulisema masikioni pangu, nikaisikia sauti yao hayo maneno:
9
Ninatakata, sikufanya kiovu, mimi ni safi, sikukora manza.
10
Tazama! Yako mambo, Mungu aliyonionea: ananiwazia kuwa miongoni mwao wachukivu wake.
11
Anaitia miguu yangu mikatale, anapaangalia pote, nipitapo.
12
Tazama! Ninakujibu: kwa hiyo huongoki, kwani Mungu ni mkuu kuliko mtu.
13
Mbona unamgombeza kwa kusema: Hayo yote hajibu neno liwalo lote?
14
Lakini Mungu akisema mara moja au mara mbili, mtu haangalii; au sivyo?
15
Watu wakiona ndoto kwa kulala usiku wenye usingizi mwingi, hapo, wanapokuwa wanalala vitandani pao,
16
ndipo, anapoyazibua masikio ya watu, ayatie muhuri hayo, aliyowafunza na kuwaonya,
17
amkataze mtu kuyafanya tena, aliyoyafanya, ayakinge majivuno, yasimpate mtu;
18
aizuie nayo roho yake, isitumbukie shimoni, nao mwili wake wenye uzima, usipite penye mishale iuayo.
19
Kwa hiyo mtu anachapwa na kuumizwa kitandani pake, mifupa yake ikishindana na mateso pasipo kukoma.
20
Huchafukwa na moyo anapokula, ijapo kiwe chakula hicho, anachokitamani rohoni.
21
Nyama za mwili wake zinakauka, zisionekane, mifupa yake iliyokuwa haionekani ikatokea waziwazi.
22
Roho yake ikafika karibu kuingia shimoni, nao moyo wake ukawafikia wauuao.
23
Hapo malaika akamtokea, ampatanishe na Mungu, mmoja wao walioko kama elfu; akimwonyesha mtu njia ya kunyoka tena,
24
ndipo, atakapomhurumia na kumwambia: Mwokoe huyu, asishuke shimoni! Kwani makombozi yake nimeyapata.
25
Ndipo, nyama za mwili wake zitakapochipuka kuliko zile za utoto, azirudie kuwa kama siku hizo za ujana wake.
26
Atakapomwomba Mungu, atapendezwa naye, atamwonyesha uso wake, aushangilie; ndivyo, anavyompatia mtu kuwa mwongofu tena.
27
Naye ataimba, watu wamsikie, akiungama kwamba: Nalikosa kwa kuyapotoa yanyokayo, lakini hakuna malipo, niliyotozwa!
28
Akaikomboa roho yangu, isitumbukie shimoni, moyo wangu uufurahie huu mwanga!
29
Tazama! Hayo yote ndiyo, Mungu anayoyafanya mara mbili, hata mara tatu,
30
airudishe roho ya mtu, isitumbukie shimoni, mwanga wenye uzima umwangazikie.
31
Tega masikio, Iyobu, unisikilize! Nyamaza tu, mimi niseme!
32
Kama unaona la kusema, nijibu! Sema! Kwani nitapendezwa kukuona kuwa mwenye wongofu.
33
Kama wewe huna la kusema, nisikilize! Nyamaza tu, nikufunze werevu ulio wa kweli! Elihu akajibu tena akisema:
← Chapter 32
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 34 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42