bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Job 34
Job 34
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 33
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 35 →
1
Mlio werevu wa kweli, yasikieni ninayoyasema!
2
Nitegeeni masikio yenu, mlio wajuzi!
3
Kwani sikio huyajaribu yanayosemwa, ufizi nao huyaonja yanayoliwa.
4
Yaliyo sawa ndiyo, tujichagulie, sote pamoja tuyajue yaliyo mema!
5
Kwani Iyobu amesema: Mimi sikukosa, lakini Mungu ananinyima shauri lililo sawa.
6
Ingawa sikukosa, napewa uwongo, kidonda, mshale wake ulichonipiga, hakiponi, tena hakuna kiovu, nilichokifanya.
7
Mtu aliye kama Iyobu yuko wapi? Masimango ya kwake yakichuruzika kama maji ya kunywa,
8
akifanya bia nao wafanyao maovu, akitembea na watu wasiomcha Mungu?
9
Kwani amesema: Hakuna mafaa, mtu anayojipatia kwa kupendezana naye Mungu.
10
Kwa hiyo nisikilizeni, ninyi waume mlio wenye akili! Mungu asiwaziwe kamwe ya kwamba: Hufanya maovu, wala Mwenyezi ya kwamba: Hufanya mapotovu!
11
Ila humlipisha mtu matendo yake, aone yaupasayo mwenendo wake.
12
Hii ni kweli, Mungu hafanyi maovu, wala Mwenyezi hayapotoi mashauri yaliyo sawa.
13
Kuiangalia nchi hii alimwagiza nani? Au yuko nani aliyeuweka huu ulimwengu wote?
14
Kama angeuelekeza moyo wake kuyaangalia yamfaliayo mwenyewe, au kama angeirudisha kwake roho na pumzi yake,
15
wote wenye miili yenye nyama wangezimia kwa mara moja, nao watu wangerudi kuwa mavumbi tena.
16
Kama uko na utambuzi, yasikilize haya! Itegee sauti ya maneno yangu masikio yako!
17
Je? Achukizwaye na mashauri yaliyo sawa anaweza kutawala? Au mkuu aongokaye utamwazia kuwa mwovu?
18
Utamwambia mfalme: Hufai kitu? au wakuu: M waovu?
19
Naye Mungu hazipendelei nyuso za wakuu, wala hawatazami wenye nguvu kuliko wanyonge, kwani wote ni viumbe vya mikono yake.
20
Punde si punde, mara watu hufa, usiku wa manane hupepesuka, kisha huenda zao, nao wenye nguvu huondolewa pasipo kushikwa mikono.
21
Kwani macho yake huziangalia njia za watu, nyayo zao zinapokanyaga, hupaona pote.
22
Hapapatikani penye giza kabisa wala kivuli chenye weusi, wapate kujificha mlemle wafanyao maovu.
23
Kwani Mungu hamwangalii mtu mara kwa mara akimtaka, aje kwake kukatwa shauri.
24
Huvunja wenye nguvu pasipo kuwachunguzachunguza, akaweka wengine mahali pao.
25
Kwani anazijua kazi zao, zilivyo kweli, akawakumba usiku, wapondwe.
26
Kwa kuwa ni waovu, huwapiga mahali palipo na watu wanaovitazama.
27
Ni kwa sababu waliacha kumfuata, nazo njia zake zote hawakuziangalia, wazishike.
28
Huko ni kuwatwika vilio vyao wakorofikao, navyo vilio vya wanyonge, alivyovisikia.
29
Akiwanyamazisha hivyo, yuko nani atakayemwambia: Unafanya nini? Akiuficha uso wake, yuko nani awezaye kumwona? Njia yake ya kuwaendea wote ni hiyo moja, wao walio mataifa mazima naye mtu aliye peke yake.
30
Huku ni kwamba: Mtu mpotovu asiwe mfalme, asigeuke kuwa tanzi la kutegea watu.
31
Je? Mungu anaambiwa: Nalipishwa, lakini sikukosa?
32
Kama yako, nisiyoyaona, nifundishe wewe! Kama nilifanya mapotovu, sitayafanya tena?
33
Je? Kama inavyokupendeza wewe, ndivyo alipishe? Unavikataaje? Ni wewe upaswaye kuchagua malipo, siye yeye? Haya! Yaseme unayoyajua!
34
Watu wenye akili wataniambia pamoja na waume walio werevu wa kweli wanaonisikia:
35
Iyobu aliyoyasema siyo ya ujuzi, kweli maneno yake siyo ya mtu mwenye akili.
36
Basi, kwa hiyo Iyobu na ajaribiwe kale na kale, kwani kama watu waovu wanavyojibu, ndivyo, anavyojibu naye.
37
Kwani makosa yake anayaongeza na kufanya maovu, akitupigia makofi machoni petu, tena akimgombeza Mungu kwa kusema kwake. Elihu akajibu tena akisema:
← Chapter 33
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 35 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42