bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Job 9
Job 9
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 10 →
1
Iyobu akajibu akisema: Najua, hii ni kweli; ndivyo, vilivyo kweli:
2
Sisi watu hakuna aliye mwongofu mbele yake Mungu.
3
Kama anataka kuulizana na mtu, akimwuliza maneno elfu, moja tu hawezi kumjibu.
4
Moyo wake ni wenye werevu wa kweli, naye ni mwenye nguvu nyingi, yuko nani aliyejishupaza kushindana naye, akapona?
5
Aondoa milima na kuiweka pengine, isivijue, makali yake yakiwaka, anaifudikiza.
6
Anaitetemesha nchi, itoweke mahali pake, nayo mashikizo yake yatikisike sana.
7
Akiliagiza jua, halichi, nazo nyota anazifunga na kuzitia muhuri.
8
Yeye peke yake ndiye anayezitanda mbingu, anatembea na kuyakanyaga mawimbi ya bahari.
9
Yeye ndiye aliyezitengeneza nyota, kama za Gari nazo za Choma, nikuchome, hata za Kilimia, nazo zile za mifanofano iliyoko upande wa kusini.
10
Hufanya mambo makuu yasiyochunguzika, navyo vioja vyake havihesabiki.
11
Tazama! Akinikaribia na kujiendea tena, simwoni, wala simtambui, akipita.
12
Tazama! Yuko nani awezaye kumrudisha nyuma, akipokonya? Yuko nani awezaye kumwuliza: Unafanya nini?
13
Kwa kuwa Mungu haachi kukasirika, nao wanaosaidiana na nondo wa baharini hawana budi kumwangukia.
14
Sembuse mimi nitawezaje kumjibu lo lote? Mbele yake nitawezaje kuchagua maneno yafaayo?
15
Ingawa niwe sikukosa, nisingemjibu, ila kwa kuwa ni mwamuzi wangu, ningemlalamikia tu.
16
Kama ningemwita, akaniitikia, nisingemtegemea kwamba: Ataisikia sauti yangu.
17
Kwa kunijia na nguvu za chamchela yeye ameniponda, akanitia vidonda vingi zaidi pasipo kosa langu lo lote.
18
Tena haniachi kabisa, nipate kutoa pumzi tu, kwani machungu ndiyo, anayonishibisha.
19
Kama ninatazamia nguvu, nimekwisha kumwona, anavyoshupaa; kama ninatazamia kupiga shauri, yuko nani atakayenishuhudia?
20
Ingawa niwe mwenye wongofu, kinywa changu kingeniponza; kingenitokeza kuwa mpotovu, ingawa niwe sikukosa.
21
Mimi ni mtu asiyekosa. Kuzimia kwa roho yangu nakuwazia kuwa si kitu, huku kuwapo kwangu kunanichukiza.
22
Yote ni mamoja; kwa hiyo nasema: Wasiokosa nao wasiomcha yeye huwaangamiza wote.
23
Akiwapatia watu mapigo ya kuwaua kwa mara moja, huwasimanga nao wasiokora manza, wakiyeyuka.
24
Nchi hii imetiwa mikononi mwao wasiomcha Mungu, naye huzifunika nyuso zao waamuzi wake; kama siye yeye mwenyewe mwingine yuko wapi?
25
Nazo siku zangu hupita upesi sana kuliko mpiga mbio, ijapo, hazikuona mema hujikimbilia.
26
Zimepita upesi kama mitumbwi ya matete, zinafanana na tai, akiangukia chakula.
27
Ikiwa, niseme: Na nivisahau hivi vinavyoniliza, na niache kununa usoni, nichangamke,
28
maumivu yangu yote hunistusha, kwani najua: hutanitokeza kabisa kuwa mtu asiyekosa.
29
Basi, kwa kuwa mimi nitatokezwa kuwa mtu asiyemcha Mungu, nijichokeshe bure tena, nipate nini?
30
Ingawa ningejitawaza kwa maji ya theluji, au ningeinawa mikono yangu kwa sabuni,
31
hapo napo ungenichovya shimoni mwenye machafu, nguo zangu mwenyewe zinitapishe.
32
Kwani Mungu si mtu kama mimi, nimjibu, tukaja kukutana shaurini kuamuliwa.
33
Kwetu sisi, yeye na mimi, hakuna awezaye kutuamua, akitushika sote wawili kwa mkono wake.
34
Na aiondoe fimbo yake, isinipige, vitisho vyake visinistushe!
35
Ndipo, nitakaposema pasipo kumwogopa, kwani hivyo sivyo, mimi nionavyo moyoni mwangu.
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 10 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42