bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Joshua 1
Joshua 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 2 →
1
Mose, mtumishi wa Bwana, alipokwisha kufa, ndipo, Bwana alipomwambia Yosua, mwana wa Nuni, mtumishi wake Mose, kwamba:
2
Mtumishi wangu Mose amekwisha kufa; sasa ondoka, uuvuke huu Yordani, wewe na watu wote wa ukoo huu, mwiingie nchi hiyo, mimi nitakayowapa wana wa Isiraeli.
3
Kila mahali, nyayo za miguu yenu zitakapopakanyaga, nitawapa ninyi, kama nilivyomwambia Mose.
4
Kutoka nyikani na huko Libanoni mpaka kwenye lile jito kubwa, lile jito la Furati, nchi yote nzima ya Wahiti, tena mpaka kwenye Bahari Kubwa iliyoko upande wa machweoni kwa jua; huko ndiko, mpaka wenu utakakokuwa.
5
Siku zote, utakazokuwapo, hatakuwako mtu atakayesimama mbele yako. Kama nilivyokuwa na Mose, vivyo hivyo nitakuwa na wewe, sitakuepuka, wala sitakuacha.
6
Jipe moyo, upate nguvu! Kwani wewe utawapeleka watu hawa, waichukue nchi hiyo, niliyowaapia baba zenu kuwapa.
7
Ni hii tu: Jipe moyo, upate nguvu sana za kuyaangalia na kuyafanya Maonyo yote, mtumishi wangu Mose aliyokuagiza! Usiyaache kupitia kuumeni wala kushotoni, upate kujua njia ya kweli po pote, utakapokwenda.
8
Kitabu cha Maonyo haya kisiondoke kinywani mwako, ila uyawaze moyoni mchana na usiku, upate kuyaangalia na kuyafanya yote yaliyoandikiwa humo, kwani ndivyo, utakavyofanikiwa katika njia zako kwa kuzijua zitakazokuwa za kweli.
9
Sukukuagiza kujipa moyo, upate nguvu? Usiogope, wala usiingiwe na vituko! Kwani Bwana Mungu wako yuko pamoja na wewe po pote, utakapokwenda.
10
Yosua akawaagiza wenye amri ya watu kwamba:
11
Piteni makambini po pote, mwaagize watu kwamba: Jitengenezeeni pamba za njiani! Kwani baada ya siku tatu mtauvuka huu Yordani kwenda kuichukua hiyo nchi, Bwana Mungu wenu atakayowapa ninyi, mwichukue, iwe yenu.
12
Nao Warubeni na Wagadi na nusu ya watu wa shina la Manese Yosua akaanza kuwaambia kwamba:
13
Likumbukeni lile neno, Mose, mtumishi wa Bwana, alilowaagiza kwamba: Bwana Mungu enu atawapatia kutulia na kuwapa ninyi nchi hii.
14
Wake na watoto na nyama wenu wa kufuga watakaa katika nchi hii, Mose aliyowapa ninyi ng'ambo hii ya Yordani; lakini ninyi nyote mlio mafundi wa vita wenye nguvu mtashika mata, mvuke na kuwatangulia ndugu zenu, mwasaidie.
15
Tena hapo, Bwana atakapowapatia nao ndugu zenu kutulia kama ninyi, nao waichukue hiyo nchi, Bwana Mungu wenu watakavyowapa, iwe yao, ndipo, mtakaporudi katika nchi iliyo yenu wenyewe, mwichukue, iwe yenu kweli, ni hii, Mose, mtumishi wa Bwana, aliyowapa ninyi ng'ambo hii ya Yordani upande wa maawioni kwa jua.
16
Wakamjibu Yosua kwamba: Yote, uliyotuagiza, tutayafanya, napo po pote, utakapotutuma, tutakwenda.
17
Kama tulivyomsikia Mose katika mambo yote, hivyo tutakusikia hata wewe. Tunataka tu, Bwana Mungu wako awe na wewe, kama alivyokuwa na Mose.
18
Kila mtu atakayekupingia, ukisema neno, asiyasikie maneno yako yote, utakayotuagiza, atauawa. Jipe moyo, upate nguvu!
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24