bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Joshua 12
Joshua 12
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 13 →
1
Hawa ndio wafalme wa nchi hii, wana wa Israeli waliowapiga, walipoichukua nchi yao, iwe yao wenyewe ng'ambo ya huko ya Yordani upande wa maawioni kwa jua toka mto wa Arnoni mpaka milimani kwa Hermoni, nayo nyika hiyo yote iliyoko upande wa maawioni kwa jua:
2
Sihoni, mfalme wa Waamori, aliyekaa Hesiboni na kutawala toka Aroeri ulioko kwenye mto wa Arnoni kuanzia mle mtoni katikati kufikia nusu ya Gileadi mpaka mto wa Yaboko, mpaka wa wana wa Amoni uliko.
3
Aliitawala nayo nyika kufikia upande wa maawioni kwa jua wa bahari ya Kineroti mpaka upande wa maawioni kwa jua wa bahari ya nyikani, ndiyo Bahari ya Chumvi, ukifuata njia ya kwenda Beti-Yesimoti, tena kusini chini ya matelemko ya Pisiga.
4
Tena mipaka ya Ogi, mfalme wa Basani, aliyekuwa wa masao ya wale Majitu; naye alikuwa anakaa Astaroti na Edirei;
5
aliitawala milima ya Hermoni na Salka na Basani yote mpaka kwenye mipaka ya Wagesuri na ya Wamakati na nusu ya Gileadi mpaka kwenye mipaka ya Sihoni, mfalme wa Hesiboni.
6
Mose, mtumishi wa Bwana, na wana wa Isiraeli waliwapiga, nazo nchi zao Mose, mtumishi wa Bwana, akazigawia wao wa Rubeni na wa Gadi nao walio nusu ya shina la Manase, ziwe nchi zao.
7
Nao hawa ndio wafalme, Yosua na wana wa Isiraeli waliowapiga ng'ambo ya huku ya Yordani inayoelekea baharini toka Baali-Gadi ulioko katika bonde la Libanoni mpaka kwenye ile milima mitupu inayoendelea hata Seiri; nchi hiyo Yosua akaigawia mashina ya Waisiraeli, iwe yao wenyewe, kama walivyogawanyika,
8
wakae milimani na katika nchi ya tambarare na nyikani, hata kwenye matelemko na mbuga, nako kusini kwao Wahiti na Waamori na Wakanaani na Waperizi na Wahiwi na Wayebusi:
9
Mfalme wa Yeriko mmoja, mfalme wa Ai ulioko upande wa Beteli mmoja,
10
mfalme wa Yerusalemu mmoja, mfalme wa Heburoni mmoja,
11
mfalme wa Yarmuti mmoja, mfalme wa Lakisi mmoja,
12
mfalme wa Egloni mmoja, mfalme wa Gezeri mmoja,
13
mfalme wa Debiri mmoja, mfalme wa Gederi mmoja,
14
mfalme wa Horma mmoja, mfalme wa Aradi mmoja,
15
mfalme wa Libuna mmoja, mfalme wa Adulamu mmoja,
16
mfalme wa Makeda mmoja, mfalme wa Beteli mmoja,
17
mfalme wa Tapua mmoja, mfalme wa Heferi mmoja,
18
mfalme wa Afeki mmoja, mfalme wa Saroni mmoja,
19
mfalme wa Madoni mmoja, mfalme wa Hasori mmoja,
20
mfalme wa Simuroni-Meroni mmoja, mfalme wa Akisafu mmoja,
21
mfalme wa Taanaki mmoja, mfalme wa Megido mmoja,
22
mfalme wa Kedesi mmoja, mfalme wa Yokinamu wa Karmeli mmoja,
23
mfalme wa Dori milimani kwa Dori mmoja, mfalme wa makabila ya Gilgali mmoja,
24
mfalme wa Tirsa mmoja, wafalme hawa wote ni 31.
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 13 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24