bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Joshua 14
Joshua 14
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 15 →
1
Hizi ndizo nchi, wana wa Isiraeli walizozipata katika nchi ya Kanaani kuwa mafungu yao; nao waliowagawanyia haya mafungu ni mtambikaji Elazari na Yosua, mwana wa Nuni, pamoja na wakuu wa baba za mashina ya wana wa Isiraeli.
2
Waliyapata mafungu yao kwa kuyapigia kura, kama Bwana alivyoviagiza kinywani mwa Mose kwa ajili ya hayo mashina tisa na nusu ya Manase.
3
Kwani yale mashina mawili na nusu ya lile shina moja Mose aliwapa mafugu yao ng'ambo ya huko ya Yordani, lakini Walawi hakuwapa fungu katikati yao.
4
Kwani wana wa Yosefu walikuwa mashina mawili: Manase na Efuraimu, lakini Walawi hawakuwapa fungu katika nchi yao, walipata miji tu ya kukaa pamoja na malisho yao ya kulisha nyama wao wa kufuga na mahali pa kuwekea mapato yao.
5
Kama Bwana alivyomwagiza Mose, ndivyo, wana wa Isiraeli walivyovifanya walipojigawanyia nchi hiyo.
6
Hapo, wana wa Yuda walipofika kwake Yosua kule Gilgali, Mkenizi Kalebu, mwana wa Yefune, akamwambia: Wewe unalijua lile neno, Mungu alilolisema kule Kadesi-Barnea kwa ajili yangu na kwa ajili yako.
7
Mimi nilikuwa mwenye miaka 40, Mose, mtumishi wa Bwana, aliponituma kule Kadesi-Barnea kwenda kuipeleleza nchi hii, nami nikamletea habari za mambo ya huku, kama nilivyoyaona moyoni mwangu.
8
Lakini ndugu zangu waliopanda pamoja nami wakaiyeyusha mioyo ya watu hawa, lakini mimi nilijishupaza kabisa kumfuata Bwana Mungu wangu.
9
Siku hiyo Mose akaapa kwamba: Nchi hiyo, miguu yako iliyoikanyaga, itakuwa fungu lako, iwe yako na ya wanao kale na kale, kwa kuwa umejishupaza kabisa kumfuata Bwana Mungu wangu.
10
Sasa tazama, Bwana amenikalisha uzimani, kama alivyosema, tangu hapo, alipomwambia Mose lile neno, miaka hii 45, Waisiraeli waliyoitembea nyikani, sasa leo hivi unaniona kuwa mwenye miaka 85.
11
Na leo ningaliko mwenye nguvu kama siku hiyo, Mose aliponituma; nguvu zangu kama zilivyokuwa hapo, ndivyo, hizo nguvu zangu zilivyo na leo za kupiga vita, nipate kwenda na kurudi.
12
Sasa nipe milima hiyo, Bwana aliyoitaja siku hiyo. Kwani mwenyewe ulisikia siku hiyo, ya kuwa wako Waanaki, ya kuwa iko nayo miji mikubwa yenye maboma. Labda Bwana atakuwa pamoja na mimi, nipate kuwafukuza, kama Bwana alivyosema.
13
Ndipo, Yosua alipombariki Kalebu, mwana wa Yefune, akampa Heburoni, uwe fungu lake.
14
Kwa hiyo Heburoni ukawa wake Mkenizi Kalebu, mwana wa Yefune, uwe fungu lake mpaka siku hii ya leo, kwa kuwa alijishupaza kabisa kumfuata Bwana Mungu wa Isiraeli.
15
Kale jina lake Heburoni lilikuwa mji wa Arba aliyekuwa mkubwa kuwapita Waanaki wote. Siku zile nchi hii ikapata kutengemana, kwa kuwa vita vilikoma.
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 15 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24