bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Joshua 16
Joshua 16
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 17 →
1
Wana wa Yosefu kura ikawapatia nchi toka Yordani karibu ya Yeriko, nao mpaka wa maawioni kwa jua ulikuwa yale maji ya Yeriko, ulichukua nayo nyika inayopanda kutoka Yeriko mpaka mlimani kwa Beteli.
2
Mpaka ulipotoka Beteli ulifika Luzi, tena uliendelea, ufike mpakani kwa Waarki hata Ataroti.
3
Toka huko ulitelemka upande wa baharini kuufikia mpaka wa Wayafuleti hata mpaka wa Beti-Horoni wa chini mpaka Gezeri; mwisho ulitokea baharini.
4
Wana wa Yosefu, Manase na Efuraimu, wakazipata nchi hizi, ziwe mafungu yao.
5
Nchi, wana wa Efuraimu walizozipata za kuzigawanyia koo zao, mipaka yao ni hii: mpaka wa fungu lao wa maawioni kwa jua ulianzia Ataroti-Adari, ulifika Beti-Horoni wa juu.
6
Toka huko mpaka ulikwenda kufika baharini. Upande wa kaskazini mpaka ulianzia Mikimetati, ulizunguka kwenda upande wa maawioni kwa jua, ufike Tanati-Silo, kisha ulipitia Yonoha upande wake wa maawioni kwa jua.
7
Toka Yanoha ulitelemka kufika Ataroti na Nara, kisha uligusa Yeriko na kutokea Yordani.
8
Tena kutoka Tapua mpaka ulikwenda upande wa baharini, ufike kwenye mto wa Kana, kisha ulitokea baharini. Nchi hizi zilikuwa fungu la shina la wana wa Efuraimu la kuzigawanyia koo zao.
9
Tena wana wa Efuraimu walikuwa na miji waliyowekewa katikati ya fungu la wana wa Manase, nayo miji hiyo ilikuwa pamoja na mitaa yao.
10
Lakini hawakuwafukuza Wakanaani waliokaa Gezeri; kwa hiyo Wakanaani wakakaa katikati ya Waefuraimu mpaka siku hii ya leo, lakini hawakuwa na budi kuwafanyizia kazi za kitumwa
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 17 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24