bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Joshua 18
Joshua 18
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 19 →
1
Mkutano wote wa wana wa Isiraeli ukakusanyika huko Silo, wakapanga huko lile Hema la Mkutano, kwani nchi hii ilikuwa imekwisha kushindwa nao.
2
Lakini kwao wana wa Isiraeli walikuwako mashina saba wasiopata bado mafungu yao ya nchi.
3
Ndipo, Yosua alipowaambia wana wa Isiraeli: Mpaka lini ninyi mtailegeza mikono yenu, msiende kuichukua nchi hii, Bwana Mungu wa baba zenu aliyowapa?
4
Haya! Jichagulieni kila shina watu watatu, niwatume, waondoke kwenda katika nchi hiyo, waiandike hiyo itakayokuwa fungu lao! Kisha watakaporudi kwangu,
5
waigawanye, itoke mafungu saba, Wayuda wakiushika mpaka wao upande wa kusini nao wa mlango wa Yosefu wakiushika wao mpaka upande wa kaskazini.
6
Ninyi mtakapokwisha kuiandika nchi, itoke mafungu saba, mniletee hapa huo mwandiko! Ndipo, nitakapowapigia kura hapa machoni pa Bwana Mungu wetu.
7
Kwani Walawi hawatapata fungu katikati yenu, kwani utambikaji wa Bwana ndio fungu lao; nao Wagadi na Warubeni na nusu ya Wamanase wamekwisha kuyachukua mafungu yao ng'ambo ya huko ya Yordani upande wa maawioni kwa jua, aliyowapa Mose, mtumishi wa Bwana.
8
Ndipo, watu wale walipoondoka kwenda zao, nao waliokwenda kuiandika nchi Yosua akawaagiza kwamba: Nendeni kuzunguka katika nchi hiyo na kuiandika! Kisha rudini kwangu! Ndipo, nitakapowapigia kura machoni pa Bwana hapa Silo.
9
Wale watu wakaenda, wakapita po pote katika hizo nchi, wakaziandika katika kitabu, mji kwa mji, zipate kutokea kuwa mafungu saba, kisha wakarudi makambini kwa Yosua huko Silo.
10
Ndipo, Yosua alipowapigia kura huko Silo machoni pa Bwana; ndivyo, Yosua alivyowagawanyia wale wana wa Isiraeli hizo nchi, wayapate mafungu yao.
11
Ikatokea kura ya shina la wana wa Benyamini ya kuzigawanyia koo zao, nayo nchi, kura iliyowapatia, ilikuwa katikati ya wana wa Yuda na wana wa Yosefu.
12
Mpaka wao wa upande wa kaskazini ulitoka mtoni kwa Yordani, kisha mpaka ulipanda kandokando ya Yeriko upande wake wa kaskazini, tena uliendelea kupanda milimani upande wa baharini, utokee katika nyika ya Beti-Aweni.
13
Toka huko mpaka uliendelea kufika Luzi, kando ya Luzi kuelekea kusini, nao Luzi ndio Beteli; kisha mpaka ulishukia Ataroti-Adari katika ule mlima ulioko upande wa kusini wa Beti-Horoni wa chini.
14
Kisha mpaka uliendelea na kugeuka upande wake wa baharini, uelekee kusini toka mlima huo unaoelekea Beti-Horoni upande wa kusini, utokee Kiriati-Baali, ndio Kiriati-Yearimu ulio mji wa wana wa Yuda. Huu ndio upande wake wa kuelekea baharini.
15
Nao upande wake wa kuelekea kusini ulianza pembeni kwa Kiriati-Yearimu; mpaka ulipotoka huko uliendelea upande wa baharini kufika kwenye chemchemi ya maji ya Nefutoa.
16
Toka huko mpaka ulitelemka kufika pembeni kwa mlima ule unaoelekea bondeni kwa mwana wa Hinomu ulioko upande wa kaskazini wa Bonde la Majitu, ulishuka Bondeni kwa Hinomu kando kwao Wayebusi upande wao wa kusini, tena uliendelea kushuka Eni-Rogeli.
17
Toka huko mpaka uliendelea na kugeukia kaskazini na kutoka Eni-Semesi, ulitokea Geliloti unaoelekea hapo pa kukwelea Adumimu, kisha ulishuka kwenye mwamba wa Bohani, mwana wa Rubeni.
18
Toka huko mpaka uliendelea na kupita upande wa kaskazini kando ya kilima kinachoelekea Araba, kisha ulitelemkia hapo Araba;
19
kisha mpaka uliendelea na kupita kando ya Beti-Hogla upande wa kaskazini, upate kutokea pembeni kwa Bahari ya Chumvi upande wake wa kaskazini kwenye mwisho wa kusini wa Yordani. Huu ndio mpaka wa kusini.
20
Lakini Yordani ulikuwa mpaka wake wa upande wa maawioni kwa jua. Hili lilikuwa fungu lao wana wa Benyamini la kuzigawanyia koo zao, mipaka yake ilivyolizunguka.
21
Miji ya shina la wana wa Benyamini ya kuzigawanyia koo zao ilikuwa: Yeriko na Beti-Hogla na Emeki-Kesisi,
22
na Beti-Araba na Semaraimu na Beteli,
23
na Awimu na Para na Ofura,
24
na Kefari-Amoni na Ofuni na Geba; ndio miji 12 pamoja na mitaa yao.
25
Gibeoni na Rama na Beroti,
26
na Misipe na Kefira na Mosa,
27
na Rekemu na Iripeli na Tarala,
28
na Sela, na Elefu na Yebusi, ndio Yerusalemu, Gibeati, Kiriati, ndio miji 14 pamoja na mitaa yao. Hili lilikuwa fungu lao wana wa Benyamini la kuzigawanyia koo zao.
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 19 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24