bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Joshua 2
Joshua 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 3 →
1
Yosua mwana wa Nuni, akatuma na kufichaficha toka Sitimu watu wawili kwenda kupeleleza, akiwaambia: Nendeni, mwitazame nchi hii nao mji wa Yeriko! Wakaenda, wakafikia nyumbani mwa mwanamke mgoni, jina lake Rahabu, wakalala huko.
2
Mfalme wa Yeriko alipoambiwa: Tazama, wako watu waliotoka kwa wana wa Isiraeli, wamekuja usiku huu kuipeleleza nchi hii,
3
mfalme wa Yeriko akatuma kwa Rahabu kumwambia: Watoe wale watu waliokuja kwako na kuingia nyumbani mwako, kwani wamekuja kuipeleleza nchi hii yote.
4
Lakini yule mwanamke akawachukua wale watu wawili, akawaficha, kisha akasema: Kweli wale watu walifika kwangu, lakini sikujua, walikotoka.
5
Tena hapo, malango yalipofungwa jioni, wale watu wakatoka, nami sikujua, wale watu walikokwenda. Wafuateni upesi kwa kupiga mbio, na mwakamate.
6
Lakini alikuwa amewapandisha darini na kuwaficha katika makonge yaliyotandikwa naye huko darini.
7
Nao wale watu wakawafuata upesi wakishika njia ya kwenda Yordani mpaka huko vivukoni. Hao waliowafuata upesi walipokwisha kutoka, wakalifunga lango la mji.
8
Wale walipokuwa hawajalala bado, yule mwanamke akapanda darini na kufika huko, walikokuwa,
9
akawaambia wale watu: Ninajua, ya kuwa Bwana amewapa nchi hii, asi tukaingiwa na mastuko kwa kuwaogopa ninyi, nao wenyeji wote wa nchi hii mioyo yao imeyeyuka kwa ajili yanu ninyi;
10
kwani tumesikia, jinsi Bwana alivyokausha mbele yenu maji ya Bahari Nyekundu, mlipotoka Misri, tena mliyowatendea wale wafalme wawili wa Waamori, Sihoni na Ogi, waliokuwako ng'ambo ya huko ya Yordani, mliowaangamiza kabisa kwa kuwatia mwiko wa kuwapo.
11
Tulipoyasikia, mioyo yetu ikayeyuka, hakuna mtu asiyekatika roho kwa ajili yenu, kwani Bwana Mungu wenu ni Mungu huko mbinguni juu, hata huku chini katika nchi.
12
Sasa niapieni na kumtaja Bwana kwamba: Kama mimi nilivyowatendea mema, ndivyo, nanyi mtakavyoutendea mema mlango wa baba yangu, mnipe kielekezo cha welekevu wenu,
13
mkiacha kuwaua akina baba na mama na ndugu zangu wa kiume na wa kike nao wote wa kwao, mkiziponya roho zetu, tusife.
14
Wale watu wakawaambia: Tutazitoa roho zetu, ziwakomboe ninyi kufani, msipoyaeleza haya mambo yetu. Hapo, Bwana atakapotupa nchi hii, tutakufanyizia mambo mema yenye welekevu.
15
Kisha akawashusha kwa kamba dirishani, kwani nyumba yake ilikuwa imejengwa juu ya boma la mji; hapo juu ya boma ndipo, alipokaa.
16
Akawaambia: Nendeni milimani kujificha huko siku tatu, wanaowafuata wasiwapate! Wao wanaowafuata watakaporudi, basi, mtakwenda zenu.
17
Wale watu wakamwambia: Kwa ajili ya hicho kiapo, ulichotuapisha, hatutakora manza,
18
ila itakuwa hivyo: sisi tutakapoingia katika nchi hii, sharti ulifunge kamba hili la nyuzi nyekundu hapa dirishani, ulipotushusha, kisha baba yako na mama yako na ndugu zako nao wote walio wa mlango wa baba yako uwakusanye kwako humu nyumbani.
19
Na viwe hivyo: kila atakayetoka milangoni: pa nyumbani mwako kwenda nje, damu yake itamjia kichwani pake, lakini sisi tutakuwa hatumo; lakini kila atakayekuwa kwako humu nyumbani, damu yake itatujia sisi vichwani petu, kama mkono wa mtu utampiga.
20
Tena mtakapoyaeleza hayo mambo yetu, sisi tutakuwa hatufungwi tena na hicho kiapo, ulichotuapisha.
21
Akawaambia: Kama mlivyosema, basi, na viwe hivyo. Kisha akawaondokesha, wakaenda zao, naye akalifunga lile kamba jekundu dirishani.
22
Walipokwenda, wakaenda milimani, wakakaa huko siku tatu, mpaka wao waliowafuata wakirudi; nao hao waliowafuata waliwatafuta njiani po pote, lakini hawakuwaona.
23
Kisha wale watu wawili wakarudi wakishuka milimani na kuvuka mtoni; walipofika kwake Yosua, mwana wa Nuni, wakamsimulia yote yaliyowapata.
24
Wakamwambia Yosua: Kweli Bwana ameitia hiyo nchi yote mikononi mwetu, nao wenyeji wote wa nchi hiyo wameyeyuka mioyo kwa ajili yetu.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24