bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Joshua 21
Joshua 21
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 22 →
1
Kisha wakuu wa milango ya Walawi wakamjia mtambikaji Elazari na Yosua, mwana wa Nuni, na wakuu wa milango ya mashina ya wana wa Isiraeli,
2
wakawaambia huko Silo katika nchi ya Kanaani kwamba: Bwana aliagiza kinywani mwa Mose kutupa sisi miji ya kukaa pamoja na malisho yao ya nyama wetu wa kufuga.
3
Kwa hiyo wana wa Isiraeli wakawatolea Walawi kwa kuagizwa na Bwana katika mafungu yao miji hii pamoja na malisho yao:
4
Koo za Wakehati zilipopigiwa kura, wana wa mtambikaji Haroni waliokuwa katika hawa Walawi walipata miji 13 kwa shina la Yuda na kwa shina la Simeoni na kwa shina la Benyamini.
5
Nao wana wa Kehati waliosalia walipopigiwa kura walipata miji 10 kwa koo za shina la Efuraimu na kwa shina la Dani na kwa nusu ya shina la Manase.
6
Nao wana wa Gersoni walipopigiwa kura walipata miji 13 kwa koo za shina la Isakari na kwa shina la Aseri na kwa shina la Nafutali na kwa nusu ya shina la Manase kule Basani.
7
Nao wana wa Merari walipata miji 12 ya kuzigawanyia koo zao kwa shina la Rubeni na kwa shina la Gadi na kwa shina la Zebuluni.
8
Miji hii ndiyo, wana wa Isiraeli waliyowapa Walawi pamoja na malisho yao kwa kuwapigia kura, kama Bwana alivyoviagiza kinywani mwa Mose.
9
Kwa shina la wana wa Yuda na kwa shina la wana wa Simeoni waliwapa Walawi miji hii, waliyoita kwa majina yao.
10
Wana wa Haroni walipigiwa kura ya kwanza ya koo za Kehati katika wana wa Lawi.
11
Wakawapa Kiriati wa Arba aliyekuwa baba yake Anaki, ndio Heburoni ulioko milimani kwa Yuda pamoja na malisho yake yaliyouzunguka.
12
Lakini mashamba yake pamoja na mitaa yake walikuwa wamempa Kalebu, mwana wa Yefune, yawe mali zake za kuzishika.
13
Lakini wana wa mtambikaji Haroni waliwapa huo mji wa Heburoni, uliokuwa wa kukimbilia wauaji, pamoja na malisho yake, tena Libuna pamoja na malisho yake,
14
na Yatiri pamoja na malisho yake na Estemoa pamoja na malisho yake,
15
na Holoni pamoja na malisho yake na Debiri pamoja na malisho yake,
16
na Aini pamoja na malisho yake na Yuta pamoja na malisho yake, Beti-Semesi pamoja na malisho yake, ndio miji 9 kwa mashina haya mawili.
17
Tena kwa shina la Benyamini: Gibeoni pamoja na malisho yake na Geba pamoja na malisho yake,
18
na Anatoti pamoja na malisho yake na Almoni pamoja na malisho yake, ndio miji 4.
19
Miji yote ya wana wa Haroni waliokuwa watambikaji ilikuwa miji 13 pamoja na malisho yao.
20
Nazo koo za wana wa Kehati waliokuwa Walawi, ndio wana wa Kehati waliosalia, walipopigiwa kura yao walipata miji kwa shina la Efuraimu.
21
Wakawapa Sikemu uliokuwa wa kukimbilia wauaji pamoja na malisho yake milimani kwa Efuraimu na Gezeri pamoja na malisho yake,
22
na Kibusaimu pamoja na malisho yake na Beti-Horoni pamoja na malisho yake, ndio miji 4.
23
Tena kwa shina la Dani: Elteke pamoja na malisho yake na Gibetoni pamoja na malisho yake,
24
na Ayaloni pamoja na malisho yake na Gati-Rimoni pamoja na malisho yake, ndio miji 4.
25
Tena kwa nusu ya shina la Manase: Taanaki pamoja na malisho yake na Gati-Rimoni pamoja na malisho yake, ndio miji 2.
26
Miji yote ilikuwa 10 pamoja na malisho yao ya kuzigawanyia koo za wana wa Kehati waliosalia.
27
Nao wana wa Gersoni waliokuwa miongoni mwa koo za Walawi walipata kwa nusu ya shina la Manase mji wa Golani huko Basani uliokuwa wa kukimbilia wauaji pamoja na malisho yake na Bestera pamoja na malisho yake, ndio miji 2.
28
Tena kwa shina la Isakari Kisioni pamoja na malisho yake na Daberati pamoja na malisho yake,
29
Yarmuti pamoja na malisho yake na Eni-Ganimu pamoja na malisho yake, ndio miji 4.
30
Tena kwa shina la Aseri: Misali pamoja na malisho yake na Abudoni pamoja na malisho yake,
31
Helkati pamoja na malisho yake na Rehobu pamoja na malisho yake, ndio miji 4.
32
Tena kwa shina la Nafutali: mji wa Kedesi uliokuwa wa kukimbilia wauaji kule Galili pamoja na malisho yake na Hamoti-Dori pamoja na malisho yake na Kartani pamoja na malisho yake, ndio miji 3.
33
Miji yote, Wagersoni waliyozipatia koo zao, ilikuwa miji 13 pamoja na malisho yao.
34
Nazo koo za wana wa Merari, ndio Walawi waliosalia, walipata kwa shina la Zebuluni: Yokinamu pamoja na malisho yake, Karta pamoja na malisho yake,
35
Dimuna pamoja na malisho yake, Nahalali pamoja na malisho yake, ndio miji 4.
36
Tena kwa shina la Rubeni: Beseri pamoja na malisho yake na Yasa pamoja na malisho yake.
37
Kedemoti pamoja na malisho yake na Mefati pamoja na malisho yake, ndio miji 4.
38
Tena kwa shina la Gadi: mji wa Rama wa Gileadi, uliokuwa wa kukimbilia wauaji, pamoja na malisho yake na Mahanaimu pamoja na malisho yake,
39
Hesiboni pamoja na malisho yake, Yazeri pamoja na malisho yake, yote ndio miji 4.
40
Miji yote, wana wa Merari waliosalia miongoni mwa koo za Walawi waliyozipatia koo zao kwa kupigiwa kura, ilikuwa miji 12.
41
Miji yote ya Walawi iliyokuwa katikati ya nchi zao wana wa Isiraeli ilikuwa miji 48 pamoja na malisho yao yaliyoizunguka;
42
miji hii ilikuwa mji kwa mji pamoja na malisho; ndivyo, miji hiyo yote ilivyokuwa.
43
Ndivyo, Bwana alivyowapa Waisiraeli nchi hii yote, aliyoapa kuwapa baba zao, wakaichukua, wakakaa humo.
44
Naye Bwana akawapatia utulivu pande zote pia, kama alivyowaapia baba zao, mtu asiweze kusimama mbele yao miongoni mwa adui zao wote, kwani adui zao wote Bwana aliwatia mikononi mwao.
45
Yale mema yote, Bwana aliyowaagia wao wa mlango wa Isiraeli, halikuwapotelea hata moja, yalikuwa yametimia yote pia.
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 22 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24