bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Joshua 23
Joshua 23
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 24 →
1
Siku zilipopita nyingi tangu hapo, Bwana alipowapatia wana wa Isiraeli kutulia, wasipigane na adui zao wote waliowazunguka, Yosua akawa mzee kwa kuwa mwenye siku nyingi.
2
Kwa hiyo Yosua akawaita Waisiraeli wote, wazee wao na wakuu wao na waamuzi wao na wenye amri wa kwao, kisha akawaambia: Mimi sasa ni mzee mwenye siku nyingi.
3
Ninyi mmeyaona yote, Bwana Mungu wenu aliyowafanyizia hao wamizimu wote machoni penu, Bwana Mungu wenu akiwapigia vita.
4
Tazameni: Nimewagawia nazo nchi zao hao wamizimu waliosalia na kuyapigia mashina yenu kura, wazipate kuwa zao toka mto wa Yordani pamoja nazo za wale wamizimu, niliokwisha kuwatowesha mpaka kwenye Bahari Kubwa, jua linakoingia.
5
Bwana Mungu mwenyewe atawakumba, waondoke machoni penu, atawafukuza, msiwaone tena, mpate kuzichuua nchi zao, kama Bwana Mungu wenu alivyowaambia.
6
Kwa hiyo jishupazeni sana, myaangalie na kuyafanya yote yaliyoandikwa katika kitabu cha Maonyo ya Mose, msiyaache na kugeuka kuumeni wala kushotoni!
7
Msiingie kwao hao wamizimu waliosalia kwenu, wala majina ya miungu yao msiyalilie, wala msiyakumbushe, wala msiyataje mkiapa, wala msiitumikie na kuiangukia!
8
Ila gandamaneni na Bwana Mungu wenu, kama mlivyofanya mpaka siku hii ya leo!
9
Naye Bwana amefukuza machoni penu mataifa makubwa yenye watu wenye nguvu, hata mmoja asiweze kusimama mbele yenu mpaka siku hii ya leo.
10
Mtu mmoja wa kwenu hufukuza elfu wa kwao, kwani Bwana Mungu wenu ndiye anayewapigia vita, kama alivyowaambia.
11
Kwa hiyo jiangalieni sana kwa ajili ya roho zenu, mmpende Bwana Mungu wenu!
12
Kwani mtakaporudi nyuma na kuandamana na masao ya hao wamizimu waliosalia kwenu, mwoane nao mkiingia kwao nao wakiingia kwenu,
13
ndipo mjue kabisa, ya kuwa Bwana Mungu wenu hataendelea kuwafukuza wamizimu hao, msiwaone tena, ila watakuwa mitego na matanzi ya kuwanasa na viboko vya kuwapiga mbavuni na miiba ya kuyachoma macho yenu, mpaka mwangamie katika nchi hii nzuri, Bwana Mungu wenu aliyowapa.
14
Tazameni, mimi sasa ninajiendea na kuishika njia yao wote walioko huku nchini. Nanyi tambueni kwa mioyo yenu yote na kwa roho zenu zote, ya kuwa yale mema yote, Bwana Mungu wenu aliyowaagia, yamewatimilia yote pia, halikuwapotelea hata moja lao!
15
Lakini kama yale mema yote, Bwana Mungu wenu aliyowaagia, yalivyowatimilia, vivyo hivyo Bwana atawatimizia nayo yale mabaya yote, mpaka awatoweshe katika nchi hii nzuri, Bwana Mungu wenu aliyowapa.
16
Hayo yatafanyika, msipolishika Agano, Bwana Mungu wenu alilowaagiza, mtakapokwenda kutumikia miungu mingine na kuiangukia, basi, hapo ndipo, makali ya Bwana yatakapowawakia, mwangamie upesi na kutoweka katika nchi hii nzuri, aliyowapa ninyi.
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 24 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24