bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Joshua 3
Joshua 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 4 →
1
Yosua akaamka asubuhi na mapema, wakaondoka kule Sitimu, wakaja Yordani, yeye na wana wote wa Isiraeli, wakalala huko kabla ya kuvuka.
2
Siku tatu zilipopita, wenye amri wakazunguka makambini,
3
wakawaagiza watu kwamba: Mtakapoliona Sanduku la Agano la Bwana Mungu wenu, watambikaji Walawi wakilichukua, nanyi mtaondoka mahali penu, mlifuate.
4
Mtaangalia tu, hapo katikati yenu nalo hilo Sanduku pawe mahali penye urefu wa mikono elfu mbili, msilikaribie zaidi, mpate kuijua njia yenu ya kuishika, kwani hamtavuka katika njia ya siku zote.
5
Kisha Yosua akawaambia watu: Jieueni! Kwani kesho Bwana atafanya vioja kwenu.
6
Kisha Yosua akawaambia watambikaji kwamba: Lichukueni Sanduku la Agano, mwatangulie watu! Ndipo, walipolichukua Sanduku la Agano, wakawatangulia watu.
7
Ndipo, Bwana alipomwambia Yosua: Siku hii ya leo nitaanza kukukuza machoni pa Waisiraeli wote, kwa kuwa watajua, ya kama nitakuwa na wewe, kama nilivyokuwa na Mose.
8
Nawe uwaagize watambikaji wanaolichukua Sanduku la Agano kwamba: Mtakapofika ukingoni penye maji ya Yordani mtasimama.
9
Yosua akawaambia wana wa Isiraeli: Fikeni karibu, myasikie maneno ya Bwana Mungu wenu!
10
Kisha Yosua akawaambia: Hapo ndipo, mtakapojua, ya kuwa Mungu Mwenye usima yuko katikati yenu, atakapowafukuza kabisa mbele yenu Wakanaani na Wahiti na Wahiwi na Waperizi na Wagirgasi na Waamori na Wayebusi.
11
Nanyi mtaliona sanduku la Agano la Bwana wa nchi zote, likiwatangulia kuuvuka Yordani.
12
Kwa hiyo jichagulieni watu kumi na wawili katika mashina ya Waisiraeli, katika kila shina moja mtu mmoja!
13
Itakuwa hapo, nyayo za miguu ya watambikaji wanaolichukua Sanduku la Agano la Bwana wa nchi zote zitakapoyagusa maji ya Yordani, ndipo, maji ya Yordai yatakapojitenga, hayo maji yanayoshuka nayo yanayotoka juu, haya yasimame kuwa kama boma moja tu.
14
Watu walipoondoka mahemani kwao, wauvuke Yordani, watambikaji wakalichukua Sanduku la Agano kuwatangulia watu;
15
basi, wachukuzi wa hilo Sanduku walipofika Yordani, nayo miguu yao watambikaji waliolichukua hilo Sanduku ilipojichovya ukingoni katika maji, kwani siku zote za mavuno Yordani hujaa maji mpaka juu ukingoni pande zote mbili,
16
ndipo, maji yaliyotoka upande wa juu yaliposimama, yakafurika juu kuwa kama boma moja tu, yakafika mbali sana mpaka mji wa Adamu ulioko upande wa Sartani; nayo maji yaliyoshuka kuingia katika bahari ya nyikani, ile Bahari ya Chumvi, yakapwa yote pia; kwa hiyo watu wakapata kuvuka na kuuelekea mji wa Yeriko.
17
Nao watambikaji waliolichukua Sanduku la Agano la Bwana wakasimama katikati ya mto wa Yordani na kuishikiza miguu pakavu penyewe, nao Waisiraeli wote wakapitia pakavu; vikawa hivyo, hata watu wote wakaisha kuuvuka Yordani.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24