bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Joshua 6
Joshua 6
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 7 →
1
Wayeriko walikuwa wamefunga malango, nayo yakakaa hivyo, yalivyofungwa wa ajili ya wana wa Isiraeli, hakuwako aliyetoka wala aliyeingia.
2
Bwana akamwambia Yosua: Tazama, huu mji wa Yeriko pamoja na mfalme wake na mafundi wa vita walio wenye nguvu nimeutia mkononi mwako.
3
Uzungukeni mji huu, ninyi wapiga vita wote, mwuzunguke wote pia mara moja! Fanyeni hivyo siku sita!
4
Tena watambikaji saba na washike mabaragumu saba yenye milio mikubwa, walitangulie Sanduku la Agano! Siku ya saba sharti mwuzunguke mji huu mara saba, watambikaji wakiyapiga mabaragumu yao.
5
Tena pembe ya kondo yenye mlio mrefu itakapopigwa, watu watakapozisikia sauti za mabaragumu, watu wote pia na wazomee mazomeo makubwa, ndipo, kuta za boma la mji zitakapoanguka chini, watu wenu wapate kupanda na kuingia mjini kila mtu hapo, anaposimama.
6
Ndipo, Yosua, mwana wa Nuni, alipowaita watambikaji, akawaambia: Lichukueni Sanduku la Agano! Tena watambikaji saba na wachukue mabaragumu saba yenye milio mikubwa, walitangulie Sanduku la Bwana.
7
Nao watu akawaambia: Nendeni kuuzunguka mji huu wote! Nao wenye mata na walitangulie Sanduku la Bwana!
8
Yosua alipowaagiza watu hivyo, watambikaji saba wakachukua mabaragumu saba yenye milio mikubwa kwenda mbele ya Bwana, nao wakaenda wakiyapiga hayo mabaragumu, nalo Sanduku la Agano la Bwana likawafuata.
9
Nao wenye mata walikwenda mbele ya watambikaji waliopiga mabaragumu, nao wafuasi wa nyuma walikwenda nyuma ya Sanduku hilo, wote walikuwa wanakwenda, mabaragumu yakilia.
10
Lakini wale watu Yosua alikuwa amewaagiza kwamba: Msizomee! Wala sauti zenu zisisikilike! Wala neno lo lote lisitoke vinywani mwenu mpaka ile siku, nitakayowaambia: Zomeeni! Hapo ndipo, mtakapozomea.
11
Basi, wakalizungusha Sanduku la Bwana na kuuzunguka mji huo wote mzima mara moja, kisha wakaingia makambini, wakalala humo makambini.
12
Kesho yake Yosua akaamka na mapema, nao watambikaji wakalichukua Sanduki la Bwana.
13
Nao wale watambikaji saba wakayachukua yale mabaragumu yenye milio mikubwa kwenda mbele ya Bwana; basi, walikuwa wanakwenda na kuyapiga hayo mabaragumu, nao wenye mata walikwenda mbele yao, nao wafuasi wa nyuma walikwenda nyuma ya Sanduku la Bwana; wote walikuwa wanakwenda, mabaragumu yakilia.
14
Walipokwisha kuuzuguka huo mji mara moja siku ya pili, wakarudi makambini. Nidvyo, walivyofanya siku sita.
15
Siku ya saba wakaamka asubuhi, mapambazuko yalipoanza, wakauzunguka huo mji mara saba vivyo hivyo, kama walivyofanya siku zote; lakini siku hiyo wakauzunguka huo mji mara saba.
16
Ilipofika mara ya saba, watambikaji wale walipoyapiga mabaragumu, ndipo, Yosua alipowaambia watu: Zomeeni! Kwani Bwana amewapa mji huu.
17
Lakini mji uwe wenye mwiko wa kuwapo, yote yaliyomo yawe mali za Bwana. Rahabu tu, yule mwanamke mgoni na apone pamoja nao wote waliomo nyumbani mwake, kwa kuwa aliwaficha wajumbe, niliowatuma.
18
Jiangalieni sana kwa ajili yao yaliyo yenye mwiko, msiyatie kwanza mwiko, kisha mkachukua mengine yaliyo yenye mwiko. Kwani hivyo mtayapatia makambi ya Waisiraeli viapizo kwa kuyaponza
19
Fedha zote na dhahabu na vyombo vya shaba na vya chuma ni mali za Bwana, sharti viingie katika kilimbiko cha Bwana.
20
Ndipo, watu walipozomea, nayo mabaragumu yakapigwa; watu walipozisikia sauti za mabaragumu, nao wakazidi kuzomea mazomeo makubwa, ndipo, kuta za boma zilipoanguka chini, watu wakapanda kuuingia mji kila mtu hapo, aliposimama; ndivyo, walivyouteka huo mji.
21
Wote waliokuwamo mjini wakawatia mwiko wa kuwapo, wakawaua kwa ukali wa panga, waume kwa wake, watoto kwa wazee, hata ng'ombe na kondoo na punda.
22
Wale watu wawili walioipeleleza nchi hiyo Yosua akawaambia: Ingieni nyumbani mwake yule mwanamke mgoni, mmtoe mle nyumbani yule mwanamke nao wote waliomo mwake, kama mlivyomwapia.
23
Ndipo, wale wapelelezi vijana walipoingia mwake, wakamtoa Rahabu na baba yake na mama yake na ndugu zake nao wote waliokuwa kwake, nao wote wa ukoo wake wakawatoa, wakawaweka mahali palipokuwa nje ya makambi ya Waisiraeli.
24
Kisha huo mji wakauteketeza kwa moto pamoja navyo vyote vilivyokuwamo, lakini fedha na dhahabu na vyombo vya shaba na vya chuma wakavitia katika kilimbiko cha Nyumbani mwa Bwana.
25
Lakini yule mwanamke mgoni Rahabu na mlango wa baba yake nao wote waliokuwa wake Yosua akawaacha, asiwaue, naye akakaa katikati ya Waisiraeli mpaka siku hii ya leo, kwa kuwa aliwaficha wajumbe, Yosua aliowatuma kupeleleza Yeriko.
26
Kisha Yosua akawaapisha watu hao kwamba: Mtu na awe ameapizwa machoni pa Bwana atakayeinuka, aujenge tena mji huu wa Yeriko! Atakapoweka misingi yake, mwanawe we kwanza atakufa, tena atakapoyatia malango yake, mwanawe mdogo atakufa!
27
Bwana akawa naye Yosua, nao uvumi wake ukasikilika katika nchi yote nzima.
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 7 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24