bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Judges 13
Judges 13
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 14 →
1
Wana wa Isiraeli walipoendelea kuyafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana, Bwana akawatia mikononi mwa Wafilisti miaka 40.
2
Hapo palikuwa na mtu mmoja wa Sora wa ukoo wao Wadani, jina lake Manoa, mkewe huyu mtu alikuwa mgumba, hakuzaa.
3
Huyu mwanamke akatokewa na malaika wa Bwana, akamwambia: Tazama, wewe u mgumba, hujazaa; lakini utapata mimba, uzae mtoto mwanamume.
4
Sasa jiangalie, usinywe mvinyo wala kileo cho chote, wala usile chakula cho chote chenye mwiko.
5
Kwani utajiona kuwa nwenye mimba, kisha utazaa mtoto mwanamume; nacho kinyoleo kisifike kichwani pake, kwani kijana huyo atakuwa ametengwa kuwa wake Mungu tangu hapo, atakapozaliwa. Naye ndiye atakayeanza kuwaokoa Waisiraeli mikononi mwa Wafilisti.
6
Ndipo, yule mwanamke alipokwenda kumwambia mumewe kwamba: Mtu wa Mungu amekuja kwangu, nayo sura yake ilionekana kabisa kuwa kama sura ya malaika wa Mungu, naye alikuwa wa kutisha sana, kwa hiyo sikumwuliza, anakotoka, naye hakuniambia jina lake.
7
Akaniambia: Utajiona kuwa mweye mimba, kisha utazaa mtoto mwanamume. Toka sasa usinywe mvinyo wala kileo cho chote, wala usile chakula cho chote chenye mwiko, kwani kijana huyo atakuwa ametengwa kuwa wake Mungu tangu hapo, atakapozaliwa hata siku ya kufa kwake.
8
Ndipo, Manoa alipomlalamikia Bwana kwamba: E Bwana, yule mtu wa Mungu, uliyemtuma, na aje tena kwetu, atufundishe vema, tutakayomfanyizia huyo kijana atakayezaliwa.
9
Mungu akaisikia sauti ya Manoa, yule malaika wa Mungu akaja mara ya pili kwa yule mwanamke, alipokuwa anakaa shambani, lakini mumewe Manoa alikuwa hayuko kwake.
10
Ndipo, yule mwanamke alipopiga mbio na kukimbia sana, akampasha mumewe hiyo habari akimwambia: Tazama, amenitokea yule mtu aliyekuja kwangu siku hiyo.
11
Ndipo, Manoa alipoondoka, akamfuata mkewe, akafika kwa yule mtu, akamwuliza: Wewe ndiwe yule mtu aliyesema na huyu mwanamke? Akasema: Ni mimi.
12
Manoa akauliza: Sasa neno lako litakapotimia, yatakayompasa huyo kijana ndio nini? Tena kazi yake itakuwa nini?
13
Malaika wa Bwana akamwambia Manoa: Huyu mwanamke sharti ayaangalie yote, niliyomwambia, ayafanye!
14
Yote yatokayo katika mzabibu asiyale, wala asinywe mvinyo wala kileo cho chote! Wala asile chakula cho chote chenye mwiko! Yote, niliyomwagiza, sharti ayaangalie.
15
Kisha Manoa akamwambia malaika wa Bwana: Tunataka kukushika, tukuandalie mwana mbuzi.
16
Lakini malaika wa Bwana akamwambia Manoa: Ijapo unishike, sitakila chakula chako; lakini ukitaka kutoa ng'ombe ya tambiko, mtolee Bwana ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima. Kwani Manoa hakujua, ya kuwa yeye ni malaika wa Bwana.
17
Ndipo, Manoa alipomwuliza malaika wa Bwana: Jina lako nani, tupate kukuheshimu, neno lako litakapotimia?
18
Malaika wa Bwana akamwambia: Unaniuliziaje jina langu? nalo ni la kustaajabu.
19
Ndipo, Manoa alipochukua mwana mbuzi na kilaji cha tambiko, akamtolea Bwana juu ya mwamba hivyo vipaji vya tambiko; naye akafanya jambo la kustaajabu, nao Manoa na mkewe wakawa wanalitazama:
20
Ikawa hapo pa kutambikia, miali ya moto ilipopanda mbinguni, ndipo, malaika wa Bwana naye alipopaa katika miali ya moto uliokuwapo hapo pa kutambikia; nao Manoa na mkewe walipoviona, ndipo, walipoanguka kifudifudi chini.
21
Kisha malaika wa Bwana hakumtokea tena Manoa wala mkewe; ndipo, Manoa alipojua, ya kuwa ndiye malaika wa Bwana.
22
Naye Manoa aakamwambia mkewe: Hatuna budi kufa, kwa kuwa tumemwona Mungu.
23
Lakini mkewe akamwambia: Kama Mungu angependa kutuua, asingalipokea mikononi mwetu ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima pamoja na kilaji cha tambiko, wala asingalituonyesha hayo yote, wala asingalitupasha habari hizo zote wakati huo.
24
Yule mwanamke alipozaa mtoto mwanamume akamwita jina lake Samusoni; huyu kijana alipokua, Bwana akambariki.
25
Roho ya Bwana ilipoanza kumhimiza, alikuwa kambini kwao Wadani katikati ya Sora na Estaoli.
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 14 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21