bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Judges 14
Judges 14
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 15 →
1
Samusoni alipotelemka kwenda Timuna akaona huko Timuna mwanamke kwao vijana wa kike wa Wafilisti.
2
Alipopanda kwao akamwambia baba yake na mama yake kwamba: Nimeona mwanamke huko Timuna kwao vijana wa kike wa Wafilisti, sasa mchukueni, awe mke wangu!
3
Baba yake na mama yake wakamwambia: Kumbe kwetu hakuna mwanamke kwao vijana wa kike wa ndugu zako walio ukoo wetu, wewe ukienda kuchukua mwanamke kwao Wafilisti wasiotahiriwa? Lakini Samusoni akamwambia baba yake: Huyo mchukue, awe mke wangu! Kwani ndiye apendezaye machoni pangu.
4
Lakini baba yake na mama yake hawakujua, ya kuwa shauri hili limetoka kwa Bwana, ya kuwa yeye alitafuta njia ya kuwajia Wafilisti, maana wakati huo Wafilisti waliwatawala Waisiraeli.
5
Samusoni alipotelemka kwenda Timuna pamoja na baba yake na mama yake, hapo, walipofika kwenye mizabibu ya Timuna, mara mwana wa simba akamkingia njiani na kumngurumia.
6
Mara roho ya Bwana ikamjia kwa nguvu, akamrarua, kama ni kurarua mwana mbuzi, lakini hakuwa na mata mkononi mwake. Lakini baba yake na mama yake hakuwasimulia, aliyoyafanya.
7
Kisha akaenda Timuna kuongea na yule mwanamke, naye akapendeza zaidi machoni pake Samusoni.
8
Siku zilipopita, akarudi kumchukua. Alipotoka njiani, aende kuutazama ule mzoga wa yule simba, akaona, nyuki wengi wa porini wamo ndani ya mzoga wa simba, hata asali imo.
9
Akaitwaa mikononi mwake, akaendelea njiani akiila. Kisha akaenda kwao baba yake na mama yake, akawapa nao, nao wakaila, lakini hakuwaambia, ya kuwa asali hii ameitwaa katika mzoga wa simba.
10
Baba yake alipotelemka kwenda kwa yule mwanamke, Samusoni akafanya huko karamu, kwani ndivyo, vijana walivyofanya.
11
Ikawa, walipomwona wakachukua wenzake 30 wa kuwa naye.
12
Samusoni akawaambia: Na niwategee kitendawili! Kama mtaniambia maana yake siku hizi saba za karamu kwa kuitambua maana, basi, nitawapa ninyi kanzu 30 na mavazi mengine 30.
13
Lakini msipoweza kuniambia maana yake, ninyi mtanipa kanzu 30 na mavazi mengine 30. Wakamwambia: Kitege kitendawili chako, tukisikie!
14
Akawaambia: Kwa mlaji kikatoka chakula, kwa mwenye nguvu kikatoka kitamu. Siku tatu hawakuweza kumwambia maana ya hicho kitendawili.
15
Ikawa siku ya saba, wakamwambia mkewe Samusoni: Mnyege mumeo, atuambie hicho kitendawili, tusikuchome moto pamoja na nyumba ya baba yako! Je? Mmetualika kuja huku, mpate kuzichukua mali zetu! Au sivyo?
16
Ndipo, mkewe Samusoni alipomlilia na kumwambia: Kumbe unachukizwa na mimi, hunipendi! Wana wao walio ukoo wangu umewategea kitendawili, lakini mimi hujaniambia. Akamwambia: Tazama, hata baba yangu na mama yangu sikuwaambia, wewe nitawezaje kukuambia?
17
Alipomlilia hizo siku saba za karamu yao, basi, siku ya saba akamwambia maana, kwani alimsumbua sana, naye akawaambia hicho kitendawili wale wana wa ukoo wake.
18
Kwa hiyo watu wa ule mji wakamwambia siku ya saba, jua lilipokuwa halijachwa bado: Kiko kitamu kuliko asali? Yuko mwenye nguvu kuliko simba? Naye akawaambia: Kama hamngalimtumia ndama wangu, hapo mlipolima, hicho kitendawili changu hamngaliona maana.
19
Kisha roho ya Bwana ikamjia kwa nguvu, akatelemka kwenda Askaloni, akaua huko watu 30, akachukua yote, waliyokuwa nayo, nayo mavazi akawapa wao waliomwambia maana ya kitendawili, lakini makali yake yakawaka moto, aliporudi nyumbani mwa baba yake.
20
Kisha mkewe Samusoni akawa mkewe mmoja wao wenzake, Samusoni aliyemchagua kuwa rafiki yake.
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 15 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21