bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Nehemiah 11
Nehemiah 11
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 12 →
1
Wakuu wa watu wakaja kukaa Yerusalemu, lakini watu wengine wakapiga kura, katika kila watu kumi wapate mmoja wa kumpeleka kukaa Yerusalemu ulio mji mtakatifu; wale wengine tisa wakae mijini.
2
Watu wakawabariki hao waume waliojipa mioyo ya kukaa Yerusalemu.
3
Hawa ndio wakuu wa mitaa waliokaa Yerusalemu namo mijini mwa nchi ya Yuda; wakakaa kila mtu mahali palipokuwa mali yake katika miji yao: Waisiraeli, watambikaji, Walawi, watumishi wa Nyumbani mwa Mungu na wana wa watumwa wa Salomo.
4
Yerusalemu wakakaa wengine wao wana wa Yuda na wana wa Benyamini. Wana wa Yuda walikuwa: Ataya, mwana wa uzia, mwana wa Zakaria, mwana wa Amaria, mwana wa Sefatia, mwana wa Mahalaleli wa wana wa Peresi.
5
Na Masea, mwana wa Baruku, mwana wa Koli-Hoze, mwana wa Hazaya, mwana wa Adaya, mwana wa Yoyaribu, mwana wa Zakaria, mwana wa Msiloni.
6
Wana wote wa Peresi waliokaa Yerusalemu walikuwa waume wenye nguvu 468.
7
Hawa ndio wana wa Benyamini: Salu, mwana wa Mesulamu, mwana wa Yoedi, mwana wa Pedaya, mwana wa Kolaya, mwana wa Masea, mwana wa Itieli, mwana wa Yesaya,
8
nyuma yake Gabai-Salai; ni watu 928.
9
Yoeli, mwana wa Zikiri, alikuwa msimamizi wao, naye Yuda, mwana wa Hasenua, alikuwa msimamizi wa pili wa mji.
10
Watambikaji walikuwa: Yedaya, mwana wa Yoyaribu, Yakini,
11
Seraya, mwana wa Hilkia, mwana wa Mesulamu, mwana wa Sadoki, mwana wa Merayoti, mwana wa Ahitubu, aliyekuwa msimamizi mkuu wa Nyumba ya Mungu;
12
pamoja na ndugu zao walioifanyia Nyumba ya Mungu kazi, walikuwa watu 822. Tena Adaya, mwana wa Yerohamu, mwana wa Pelalia, mwana wa Amusi, mwana wa Zakaria, mwana wa Pashuri, mwana wa Malkia;
13
pamoja na ndugu zake walio wakuu wa milango walikuwa watu 242. Tena Amasai, mwana wa Azareli, mwana wa Azai, mwana wa Mesilemoti, mwana wa Imeri;
14
pamoja na ndugu zao waliokuwa wenye nguvu walikuwa watu 128; msimamizi wao alikuwa Zabudieli, mwana wa Hagedolimu.
15
Walawi walikuwa: Semaya, mwana wa Hasubu, mwana wa Azirikamu, mwana wa Hasabia, mwana wa Buni,
16
na Sabutai na Yozabadi waliokuwa wenye kazi za nje ya Nyumba ya Mungu, nao waliokuwa miongoni mwao wakuu wa Walawi.
17
Tena Matania, mwana wa Mika, mwana wa Zabudi, mwana wa Asafu, kiongozi wao walioimba shangilio la kushukuru, watu walipoomba. Tena Bakibukia aliyekuwa miongoni mwa ndugu zake; tena abuda, mwana wa samua, mwana wa Galali, mwana wa Yedutuni.
18
Walawi wote katika mji mtakatifu walikuwa watu 284.
19
Walinda malango walikuwa: Akubu na Talmoni na ndugu zao; ndio walioyangoja malango, walikuwa watu 172.
20
Waisiraeli wengine, nao watambikaji na Walawi wakakaa katika miji yote ya nchi ya Yuda, kila hapo palipokuwa fungu lake.
21
Lakini watumishi wa Nyumbani mwa Mungu wakakaa Ofeli; Siha na Gisipa walikuwa wasimamizi wao watumishi wa Nyumbani mwa Mungu.
22
Msimamizi wa Walawi mle Yerusalemu alikuwa Uzi, mwana wa Bani, mwana wa Hasabia, mwana wa Matania, mwana wa Mika wa wana wa Asafu waliokuwa waimbaji, akawasaidia kutumikia Nyumbani mwa Mungu.
23
Kwani mfalme aliagiza kazi zao na mshahara wao hao waimbaji, ndio waupate siku kwa siku.
24
Petaya, mwana wa Mesezabeli, wa wana wa zera, mwana wa Yuda, alikuwa amewekwa na mfalme kuyatengeneza mambo yote ya watu.
25
Nako mashambani kwenye viwanja vya kale wakakaa Wayuda wengine Kiriati-Arba na katika vijiji vyake, tena Diboni na katika vijiji vyake na Yekabuseli na katika viwanja vyake,
26
tena Yesua na Molada na Beti-Peleti,
27
Hasari-Suali na Beri-Seba na katika vijiji vyake,
28
Siklagi na Mekona na katika vijiji vyake,
29
Eni-Rimoni na Sora na Yarmuti,
30
Zanoa, Adulamu na katika viwanja vyao. Lakisi na mashambani kwake, Azeka na katika vijiji vyake; basi, wakatua toka Beri-Seba hata bonde la Hinomu.
31
Lakini wana wa Benyamini wakakaa kuanzia Geba: Mikimasi na Aya na Beteli na katika vijiji vyake,
32
Anatoti, Nobu, Anania,
33
Hasori, Rama, Gitaimu,
34
Hadidi, Seboimu, Nebalati,
35
Lodi na Ono na Bondeni kwa Mafundi.
36
Walawi wengine, ambao kwao kulikuwa kwa Wayuda, wakakaa kwa Wabenyamini.
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 12 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13