bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Revelation 3
Revelation 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 4 →
1
Malaika wa wateule walioko Sarde mwandikie: Ndivyo anavyosema yeye aliye mwenye zile roho saba za Mungu na mwenye zile nyota saba. Nayajua matendo yako, unalo jina la kuwa unaishi, lakini u mfu.
2
Amka, uyashupaze masao yanayotaka kufa nayo! Kwani sikuyaona matendo yako, ya kuwa yametimilika mbele ya Mungu wangu.
3
Kumbuka, uliyoyapokea! Nayo uliyoyasikia, yashike, upate kujuta! Usipokesha, nitakuja kama mwizi, usiitambue saa, nitakayokujia wewe.
4
Lakini unayo majina machache huko Sarde wasiozichafua nguo zao. Ndio watakaoenenda pamoja nami wenye nguo nyeupe, kwani zimewapasa.
5
Mwenye kushinda atavikwa naye nguo nyeupe, nalo jina lake sitalifuta katika kitabu cha uzima. Nami nitaliungama jina lake mbele ya Baba yangu na mbele ya malaika zake.
6
Mwenye masikio na asikie, Roho anayowaambia wateule!
7
Malaika wa wateule walioko Filadelfia mwandikie: Ndivyo, anavyosema yeye Mtakatifu aliye mwenye kweli, aliye hata mwenye ufunguo wa Dawidi. Atakapofungua, hatakuwako awezaye kupafunga tena; atakapofunga, hatakuwako awezaye kupafungua.
8
Nayajua matendo yako, tazama mbele yako nimekupa mlango ulio wazi, tena hakuna awezaye kuufunga. Kweli nguvu, ulizo nazo, ni ndogo, lakini umelishika Neno langu, hukulikana Jina langu.
9
Tazama, nitakupa wanafunzi wa Satani wanaojisema kuwa Wayuda, lakini sio, ila husema uwongo. Tazama, nitawaleta hao, waje, wakuangukie penye miguu yako, watambue, ya kuwa mimi nimekupenda wewe.
10
Kwa sababu umelishika Neno langu la uvumilivu, nitakulinda nami, nikuokoe katika saa ya majaribu itakayopafikia pote panapokaa watu kwamba: Wakaao nchini wajaribiwe.
11
Ninakuja upesi. Shikamana nayo, uliyo nayo, mtu asikitwae kilemba chako!
12
Mwenye kushinda nitamfanya kuwa nguzo Jumbani mwa Mungu wangu, asitoke tena nje. Nami nitamwandika Jina la Mungu wangu na jina la mji wa Mungu wangu, la Yerusalemu mpya, utakaoshuka toka mbinguni kwake Mungu wangu. Nitamwandika hata Jina langu jipya.
13
Mwenye masikio na asikie, Roho anayowaambia wateule!
14
Malaika wa wateule walioko Laodikia mwandikie: Ndivyo, anavyosema yeye Amin aliye shahidi mwelekevu na mkweli, aliye wa kwanza wa viumbe vyote vya Mungu.
15
Nayajua matendo yako, wewe huzizimiki, wala huzizimuki. Ungefaa ukiwa mwenye kuzizimika au mwenye kuzizimuka.
16
Lakini sasa, kwa kuwa u mwenye kuvuvuwaa, usiwe mwenye kuzizimika wala mwenye kuzizimuka, nitakutema kinywani mwangu.
17
Kwani unasema: Mimi niko na mali, ninayo malimbiko yangu, hakuna, nilichokikosa. Nawe hujui, ya kuwa wewe u mnyonge, unapaswa na kugawiwa, u maskini na kipofu na mwenye uchi.
18
Nakuonyesha mzungu, ndio huu: nunua kwangu dhahabu iliyong'azwa na moto, upate kuwa mwenye mali! Nunua nazo nguo nyeupe, upate kuvaa, uchi wako usionekane, ukakutia soni! Nunua nayo mafuta ya macho, uyapake macho yako, upate kuona!
19
Wote, ninaowapenda mimi, nawaonya na kuwapiga. Kwa hiyo jikaze, ujute!
20
Tazama, nimesimama mlangoni nikipiga hodi. Mtu atakayenisikia sauti yangu, akaufungua mlango, basi, nitaingia mwake, nile pamoja naye, naye ale pamoja nami.
21
Mwenye kushinda nitampa kukaa pamoja nami kitini pangu pa kifalme, kama mimi nami nilivyoshinda, nikakaa pamoja na Baba yangu kitini pake pa kifalme.
22
Mwenye masikio na asikie, Roho anayowaambia wateule!
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22