bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Revelation 4
Revelation 4
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 5 →
1
Kisha nalitazama, nikaona mlango mbinguni uliokuwa wazi. Ndipo, sauti ile ya kwanza, niliyoisikia kama ya baragumu, iliyosema nami, iliposema: Panda huku, nikuonyeshe yatakayofanyika, haya yakiisha! Papo hapo nikawapo kiroho.
2
Nikaona kiti cha kifalme, kilikuwa kimewekwa mbinguni; humo kitini mlikuwamo mwenye kukikalia.
3
Huyu aliyekaa, ukimtazama, alifanana na kijiwe cha yaspi na cha sardio; hata upindi wa Mungu ulikizunguka kiti, kwa kuutazama, ulifanana na kijiwe cha sumaradi.
4
Tena viti 24 vya kifalme vilikizunguka kiti kile; nikaona wazee 24 waliokaa mle vitini, waliokuwa wamevaa nguo nyeupe na vilemba vya dhahabu vichwani pao.
5
Hapo penye kiti cha kifalme palipiga umeme na vivumo na ngurumo, tena palikuwa na mienge saba ya moto iliyowaka mbele ya kiti cha kifalme, ndio zile roho saba za Mungu.
6
Tena mbele ya kiti cha kifalme kulikuwako yenye mfano wa bahari ya kioo iliyofanana na ulanga uangazikao. Napo katikati penye kiti cha kifalme na kukizunguka kiti cha kifalme palikuwa na nyama wanne waliojaa macho mbele na nyuma.
7
Nyama wa kwanza alifanana na simba, nyama wa pili alifanana na dume la ng'ombe, nyama wa tatu alikuwa na uso kama wa kimtu, nyama wa nne alifanana na tai mwenye kuruka.
8
Kila mmoja wao hao nyama wanne alikuwa na mabawa sita yaliyojaa macho po pote, nje ndani; hawapumziki mchana wala usiku wakisema: Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu ni Bwana Mungu, yeye Mwenyezi aliyekuwapo, aliopo, atakayekuja.
9
Hao nyama walipomtukuza na kumheshimu na kumshukuru yule aliyekaa kitini mwa kifalme, aliye mwenye kuwapo kale na kale pasipo mwisho,
10
ndipo, wale wazee 24 walipomwangukia yule aliyekaa kitini mwa kifalme na kumtambikia yeye aliye mwenye kuwapo kale na kale pasipo mwisho; wakavitupa vilemba vyao mbele ya kiti cha kifalme wakisema:
11
Wewe Bwana na Mungu wetu, umepaswa na kupewa utukufu na heshima na uwezo, kwani wewe uliviumba vyote; kwa hayo, uyatakayo, vikapata kuwapo vilipokwisha kuumbwa.
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22