bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Revelation 5
Revelation 5
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 6 →
1
Nikaona mkononi mwa kuume mwake yule aliyekaa kitini mwa kifalme kitabu kilichoandikwa ndani na mgongoni, nacho kilikuwa kimetiwa muhuri saba.
2
Kisha nikaona malaika mwenye nguvu, akatangaza kwa sauti kuu: Yuko nani apaswaye na kukifungua kitabu na kuziondoa muhuri zake?
3
Hakuwako hata mmoja wala mbinguni wala nchini wala kuzimuni aliyeweza kukifungua kitabu na kukitazama.
4
Ndipo, nilipolia sana, kwa sababu hakuonekana hata mmoja apaswaye na kukifungua kitabu na kukitazama.
5
Mmoja wao wale wazee akaniambia: Usilie! Tazama, yule simba wa shina la Yuda aliye mzizi wa Dawidi, yeye ameshinda, apate kukifungua kitabu na kuziondoa muhuri zake saba.
6
Kisha nikaona mwana kondoo aliyesimama katikati penye kiti cha kifalme na wale nyama wanne na wale wazee, naye alikuwa, kama amechinjwa. Alikuwa na pembe saba na macho saba; ndio zile roho saba za Mungu zilizotumwa kwenda kuzifikia nchi zote.
7
Alipokuja akakitwaa kitabu mkononi mwa kuume mwake yeye aliyekaa kitini mwa kifalme.
8
Hapo alipokitwaa kitabu, ndipo, wale nyama wanne na wale wazee 24 walipomwangukia Mwana kondoo. Wakawa wameshika kila mmoja zeze na vyano vya dhahabu vilivyojaa uvumba, ndio maombo ya watakatifu.
9
Nao wakaimba wimbo mpya wakisema: Wewe umepaswa na kukipokea kitabu na kuziondoa muhuri zake, kwani umechinjwa, umkombolee Mungu kwa damu yako watu wa mashina yote na wa misemo yote na wa makabila yote na wa wamizimu wote,
10
ukawafanya, wawe wafalme na watambikaji wa Mungu wetu; ndio watakaozitawala nchi.
11
Kisha nikaona, nikasikia sauti ya malaika wengi waliokizunguka kiti cha kifalme na wale nyama na wale wazee. Nilipowahesabu, walikuwa maelfu na maelfu na maelfu, wakasema kwa sauti kuu:
12
Mwana kondoo aliyechinjwa amepaswa na kupokea uwezo na malimbiko na werevu wa kweli na nguvu na heshima na utukufu na mapongezo.
13
Navyo viumbe vyote vilivyoko mbinguni, navyo vilivyopo nchini, navyo vilivyoko kuzimuni, navyo vilivyomo baharini, navyo vyote vilivyomo ndani yao, nikavisikia, vikisema: Mpeni yeye aliyekaa kitini mwa kifalme naye Mwana kondoo mapongezo na heshima na utukufu na nguvu kale na kale pasipo mwisho!
14
Wale nyama wanne waliposema: Amin, ndipo, wale wazee walipoanguka chini, wakamsujudia mwenye kuishi kale na kale.
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22