bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
/
Hosea 11
Hosea 11
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 12 →
1
Israeli alipokuwa mutoto, nilimupenda. Kutoka Misri nilimwita mwana wangu.
2
Lakini kadiri nilivyozidi kuwaita, ndivyo walivyozidi kwenda mbali nami; waliendelea kuyatambikia Mabali, na kuvifukizia ubani sanamu za miungu.
3
Mimi ndiye niliyemufundisha watu wa Efuraimu kutembea! Mimi mwenyewe niliwatwaa katika mikono yangu; lakini hawakutambua kwamba mimi ndiye niliyewatunza.
4
Niliwaongoza kwa huruma, nilishikamana nao kwa upendo; kama baba anavyomunyanyua mutoto mpaka kwenye shavu lake, ndivyo nami nilivyokuwa kwao. Mimi niliinama chini na kuwakulisha.
5
Basi, watarudi katika inchi ya Misri; watatawaliwa na mufalme wa Asuria, kwa sababu wamekataa kunirudilia.
6
Upanga utavuma katika miji yao, utavunjavunja miimo ya milango yake na kuwaangamiza katika kuta zao.
7
Watu wangu wamekusudia kuniacha mimi, wakiitwa kusimama wapande juu, hakuna hata mumoja anayeweza.
8
Ewe Efuraimu, ninaweza kukuacha namna gani? Ninaweza kukutupilia, ewe Israeli namna gani? Nitaweza namna gani kukufanya kama muji wa Adama? Nitaweza namna gani kukutendea kama Zeboimu! Ninazuizwa na moyo wangu; huruma yangu imezidi kuwa motomoto.
9
Nitaizuia hasira yangu kali; sitamwangamiza tena Efuraimu, maana mimi ni Mungu, wala si mwanadamu. Mimi ndimi Mutakatifu kati yenu, nami sitakuja kuwaangamiza.
10
Watanifuata mimi Yawe ninayenguruma kama simba; nitakaponguruma watanifikia toka magaribi wakitetemeka.
11
Watakuja kutoka Misri wakitetemeka kama ndege, wataruka kutoka Asuria kama njiwa nami nitawarudisha kwao. –Ni ujumbe wa Yawe.
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 12 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14