bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
/
Hosea 6
Hosea 6
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 7 →
1
Halafu watasema: Tuende tumurudilie Yawe! Yeye mwenyewe ameturarua, lakini yeye mwenyewe atatuponyosha. Yeye mwenyewe ametuumiza, lakini yeye mwenyewe atatunza vidonda.
2
Nyuma ya siku mbili atatupatia tena uzima. Nyuma ya siku tatu atatufufua kusudi tuweze kuishi pamoja naye.
3
Basi tumutambue, tujikaze sana kumujua Yawe. Kuja kwake ni hakika kama mapambazuko, yeye atatufikia kama vile manyunyu, kama vile mvua za kwanza zinavyolowanisha udongo.
4
Lakini Yawe anasema hivi: Nitakutendea nini, ee Efuraimu? Nikufanyie nini, ee Yuda? Upendo wenu kwangu ni kama ukungu wa asubui, kama umande unaotoweka upesi.
5
Ndiyo maana ninawashambulia kwa njia ya manabii, nimewaangamiza kwa maneno yangu, hukumu yangu inajitokeza kama mapambazuko.
6
Maana kitu ninachotaka kwenu ni wema na si sadaka, kumujua Mungu na si kutoa sadaka za kuteketezwa kwa moto.
7
Lakini mulivunja agano langu kama mulivyofanya katika muji wa Adamu; kule walikosa uaminifu kwangu.
8
Gileadi ni muji wa waovu, umejaa damu.
9
Kama vile wanyanganyi wanavyomuvizia mutu katika njia, ndivyo makuhani walivyojikusanya na kuvizia. Wanaua watu katika njia yenye kuelekea Sekemu, na kutenda uovu mukubwa.
10
Nimeona jambo la kuchukiza sana kati ya Waisraeli: watu wa Efuraimu wanakimbilia miungu mingine, Waisraeli wamejichafua.
11
Nawe Yuda vilevile, nimekupangia wakati utakapovuna azabu.
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 7 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14